• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 13, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi

0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na HANIFA RAMADHANI,

Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameahidi kujenga hospitali maalumu ya kisasa ya maradhi ya saratani visiwani humo, kuwarahisishia wagonjwa wa maradhi hayo kutokwenda nje ya nchi kufuata huduma.

Dk. Mwinyi alieleza hayo, Ikulu Mjini Unguja, katika hafla ya utiaji saini wa ujenzi, ukarabati na utanuzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja.

Alisema kutakuwa hakuna haja ya wagonjwa wa maradhi ya saratani kusafirishwa nje ya nchi, badala yake watatibiwa Zanzibar baada ya serikali kujenga hospitali hiyo ya kisasa.

“Leo kama kuna maradhi yanayotuathiri hapa Zanzibar ukiacha maradhi ya moyo, ubongo na mifupa, ni maradhi ya saratani, tumesema hakuna haja ya kuendelea kuwasafirisha watu, gharama ni kubwa, tujenga hospitali ya kisasa ya maradhi ya saratani na hospitali inakuja,” alisema.

Aidha, aliahidi kujenga hospitali kubwa zaidi ya rufaa ambayo pia itakuwa ni ya kufundishia wanafunzi wa sekta ya afya katika eneo la Binguni.

Dk. Mwinyi ambaye ni Mgombea Urais Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema akipata tena ridhaa ya kuwaongoza Wazanzibari katika wamu ya pili atakamilisha kazi iliyobaki katika sekta ya afya kwa kukamilisha hospitali zilizobaki za mikoa na za rufaa ya Binguni na Mnazi Mmoja na hospitali maalumu ya maradhi ya saratani.

Akizungumzia ukarabati mkubwa wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dk. Mwinyi alisema hospitali hiyo inakwenda kuwa mpya na ina historia kubwa ya karne, huku akionesha kufurahishwa kuingia katika historia ya kuwa na mchango wa kuitengeneza hospitali hiyo.

Alisema baada ya mwaka mmoja na nusu kutoka sasa, Hospitali ya Mnazi Mmoja itakamilika na itakuwa mpya, yenye dhana za kisasa na huduma zote zitapatikana hapo.

“Tutafanya matibabu ya moyo hapa Zanzibar, tutafanya matibabu ya ubongo na uti wa mgongo, ambayo kwa sasa tunalazimika kuwapeleka wagonjwa nje ya nchi,” alisema.

Dk. Mwinyi alieleza wakati anaingia madarakani, alisema sekta ya afya kwake ina umuhimu mkubwa, kwa kuwa ni muhimu watu kuwa na afya bora, kwa kuwa ndiyo uchumi utakavyokua, pia kutokana na yeye ni mtaalamu wa sekta ya afya, lazima ahakikishe anaimarisha vizuri huduma ya afya.

Alibainish awali aliamua aanze kuimarisha sekta ya afya kuanzia huduma za msingi, alafu baadaye za wilaya na mikoa.

“Leo (jana) ninafurahi kusema kule katika huduma za msingi kuna ujenzi unaendelea wa vituo vya afya vya kisasa zaidi, hospitali za wilaya nyote mmeziona na zinatoa huduma nzuri, sasa tumejikita katika hospitali za mikoa na zabuni zimeshaanza kutolewa,” alisema.

Alieleza kutakuwa na hospitali tano mikoa yote ya Unguja na Pemba yenye hadhi ya mkoa, ambapo serikali imeanza na mkoa wa Mjini Magharibi, ambako kuna jengo zuri la hospitali, vifaa vya kutosha na huduma nzuri zinatolewa.

Aliahidi huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi zitapatikana katika hospitali zote za mikoa, watu wasilazimike kutoka mikoa mmoja kwenda mwingine kufuata huduma.

Naye, Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alimpongeza Dk. Mwinyi kwa uongozi wake imara ambao umewezesha kutiwa saini kwa mradi huo wenye umuhimu mkubwa kwa Zanzibar, hasa Hospitali ya Mnazi Mmoja ambayo imeelemewa na idadi kubwa ya wagonjwa.

Alisema sekta ya afya imepiga hatua kubwa hasa katika ujenzi wa hospitali za wilaya, vituo vya afya vya kisasa na zahanati.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mngereza Miraji Mzee alisema Hospitali ya Mnazi Mmoja imekuwa nguzo kuu ya huduma za afya kwa Zanzibar kwa muda mrefu kwa kuhudumia maelfu ya wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali za visiwa vya Unguja na Pemba na Tanzania Bara.

“Miundombinu ya sasa haiendani tena na mahitaji ya huduma za afya zinazohitajika katika karne hii ya 21, ambapo teknolojia na ubora wa huduma vinapaswa kupewa kipaumbele,” alisema.

Miraji alieleza kutokana na hilo, serikali iliona ipo haja ya dharura ya kufanya matengenezo makubwa, uboreshaji wa vifaa tiba na utanuzi wa majengo, hospitali iendelee kuwa kitovu cha huduma za afya kwa kutoa matibabu ya kisasa na kwa kuzingatia mahitaji ya jamii ya sasa na ya baadaye.

Alisema ukarabati na utanuzi huo utafanywa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Muembe Ladu na Kidongo Chekundu.

Miraji alisema mradi wa ukarabati na utanuzi unatekelezwa kwa ufadhili wa mkopo nafuu kutoka Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi Barani Afrika (BADEA), Mfuko wa Maendeleo wa Saudia (Saudi Fund) na Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (Kuwait Fund), kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema gharama za utekelezaji wa mradi huo ni dola za Marekani milioni 43.2, ambapo kazi itafanywa na Mkandarasi China Jiangxi International Economic and Technical Cooperation Co. Limited JV China IPPR International Engineering Co. Limited,

Alisema kukamilika kwa mradi huo kutaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya afya na itakuwa safari ya kuhakikisha kila Mzanzibari anapata huduma bora za afya, bila vikwazo vya aina yeyote.

Miraji alibainisha ukarabati na utanuzi wa mradi huo unatarajiwa kuanza Oktoba, mwaka huu na kukamilika Juni, 2027.

Previous Post

DK. NCHIMBI ATAJA KIPAUMBELE CCM

Next Post

DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

Next Post
DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA KUUNGURUMA MOROGORO

DK. SAMIA KUUNGURUMA MOROGORO

2 months ago
DK. NCHIMBI ATANGAZA MITAA YA VIWANDA NCHINI

DK. NCHIMBI ATANGAZA MITAA YA VIWANDA NCHINI

1 month ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.