• ePaper
Sunday, May 10, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, USTAHIMILIVU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 17, 2025
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA AHIMIZA AMANI, USTAHIMILIVU
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuwasisitiza Watanzania waendelee kuliombea Taifa, amani, upendo, ustahimilivu na mshikamano viendelee kudumu nchini.

Kauli hiyo ilitolewa mkoani Dodoma na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, alipowasilisha salamu za Rais Dk. Samia kwa waumini na viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kisasa.

“Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anawasalimu sana. Yuko pamoja nanyi na rai yake kwa Watanzania wote ni kuendeleza maombi kwa Taifa letu kuwa watulivu na kuiombea amani iendelee kudumu,”alisema.

Aidha, Waziri Mkuu, alisema kuwa, ni wajibu kwa kila Mtanzania, kuhakikisha amani ya nchi, inaendelea kulindwa na kuenziwa, kwa sababu pasipo amani, Taifa halitoweza kutekeleza majukumu yake, ikiwemo kufanya ibada na shughuli nyingine za kijamii.

“Pasipo amani, hatuwezi kutekeleza majukumu mengine yoyote, pasipo amani, hatuwezi kuendesha ibada. Hivyo, ni wajibu wa kila Mtanzania kuiombea nchi yetu.

“Pakiwa na amani, tunaweza kutekeleza yale yaliyo katika matarajio yetu, tunaweza hata kutatua yale tunayoyaona kuwa ni magumu,”alisema.

Ibada hiyo, iliongozwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Dk. Christian Ndossa, ambaye alitumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania waishi kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu na wawe na matumaini kwake na wajiepushe na maovu.

Waziri Mkuu aliambatana na mkewe, Neema Nchemba, katika ibada hiyo.

Viongozi wengine waliohudhuria ibada hiyo ni Naibu Spika wa Bunge, Daniel Sillo, Mbunge wa Kilolo, Ritha Kabati, Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya, Mbunge wa Viti Maalumu, Balozi Dk.. Pindi Chana, Mbunge wa Itigi, Yohana Msita na Mbunge wa Kalenga, Jackson Kiswaga.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA AWAKOSHA VIONGOZI WA DINI NCHINI

Next Post

BARAZA LA MAWAZIRI

Next Post
BARAZA LA MAWAZIRI

BARAZA LA MAWAZIRI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

KAULI UN YAWAKOSHA MABALOZI, WAHADHIRI

5 months ago
DK. KIKWETE ATEULIWA KUWA MWAKILISHI WA NGAZI YA JUU WA MWENYEKITI WA KAMISHENI YA AU

DK. KIKWETE ATEULIWA KUWA MWAKILISHI WA NGAZI YA JUU WA MWENYEKITI WA KAMISHENI YA AU

2 months ago

Popular News

  • MTIHANI MZITO KWA MOALIN

    MTIHANI MZITO KWA MOALIN

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ATAJA MWAROBAINI MAFURIKO DARAJA LA DUMILA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA ATIA NENO BEI MAFUTA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?