• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

‘POLICE SERVICE’ GUMZO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 29, 2025
in Habari, Kitaifa
0
‘POLICE SERVICE’ GUMZO
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

UAMUZI wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kulifanyia maboresho Jeshi la Polisi kutoka katika ‘Police Force’ kwenda ‘Police Service’ umekuwa gumzo zuri nchini.

Mwaka 2023, Rais Dk. Samia aliunda Tume ya Haki Jinai chini ya Jaji Mkuu mstaafu, Othman Chande kupitia mambo mbalimbali ukiwemo muundo wa Jeshi la Polisi na namna bora ya kuboresha utendaji wake.

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene alitangaza kuagizwa na Rais Dk. Samia kuhakikisha mabadiliko hayo yanafanyika ndani ya Jeshi la Polisi, ambalo linafanya kazi nzuri, hivyo ili kuboresha zaidi utendaji wake linapaswa kuhamia katika Jeshi la Polisi la huduma zaidi.

WADAU WASIFU

Uamuzi huo uliwaibua wadau haki za binadamu nchini, ambao waliipongeza serikali kwa kuendelea kuchukua hatua madhubuti za kushughulikia changamoto za kijamii, hususan katika eneo la ulinzi na usalama wa raia.

Pia, walisema msisitizo wa serikali wa kuliboresha Jeshi la Polisi na kulifanya kuwa la huduma kwa wananchi badala ya kutumia nguvu kupita kiasi, ni hatua muhimu ya kuimarisha utawala bora, amani na mshikamano wa kitaifa.

Akizungumza na UHURU Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Wateteziwa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Ole Ngurumwa, alisema mageuzi yaliyotangazwa yanaendana na mapendekezo ya muda mrefu ya wadau wa haki za binadamu.

Ole Ngurumwa alisema, uamuzi huo wa Rais unaonyesha utayari wa serikali kusikiliza na kutekeleza hoja zilizobainishwa katika ripoti mbalimbali.

Alisisitiza utekelezaji wa vitendo, mafunzo endelevu na mifumo ya uwajibikaji ni nguzo muhimu za kufanikisha mageuzi hayo.

Kwa mujibu wa Ole Ngurumwa, upatikanaji wa Katiba Mpya utaweka misingi imara ya mfumo wa haki jinai na kuimarisha ulinzi wa haki za binadamu nchini.

Mhadhiri Mwandamizi wa Masuala ya Uchumi na Uongozi kutoka Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere, Dk. Philip Daninga, alisema mageuzi hayo ni msingi wa kujenga uhusiano mzuri kati ya vyombo vya dola na jamii, jambo litakaloongeza imani ya wananchi kushirikiana na polisi katika masuala ya usalama.

Dk. Daninga alisema askari polisi wa hivi sasa ni wasomi wenye elimu na uwezo wa kutosha kutumia mbinu za kisasa na kitaalamu katika utekelezaji wa majukumu yao, hivyo aliwahimiza kuzingatia ukubwa wa kosa na mazingira husika wakati wa utekelezaji wa sheria, kuhakikisha haki, utu na usawa vinazingatiwa kwa kila mwananchi.

“Hatua hizi zitasaidia kuponya majeraha ya kisaikolojia na kijamii yaliyowahi kujitokeza katika baadhi ya vipindi vilivyopita, hususan pale wananchi wapohisi kutengwa au kuogopa polisi. Kwa kulikaribisha Jeshi la Polisi karibu na wananchi, serikali inalenga kujenga mshikamano na ushirikiano utakaosaidia kudumisha amani ya kudumu,” alisema.

Dk. Daninga aliitaka jamii kuendelea kuiunga mkono serikali katika jitihada zake za kuimarisha utawala bora, amani, maendeleo na kuipongeza inapofanya vizuri kwani ni sehemu ya kujenga taifa imara na lenye taasisi zinazoaminika.

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fulgence Massawe, alisema maelekezo ya Rais Dk. Samia ya kulifanya Jeshi la Polisi kuwa la huduma, ni hatua muhimu iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu na wadau wa haki za binadamu.

Massawe alisema matumizi ya nguvu kupita kiasi yanasababisha malalamiko ya wananchi, hali inaweza kudhoofisha uhusiano kati ya polisi na jamii.

“Mageuzi haya yatarejesha heshima ya Jeshi la Polisi na kujenga tena uaminifu kwa wananchi, hasa yakisindikizwa na mafunzo ya kitaalamu na mifumo thabiti ya uwajibikaji,”alisema.

Massawe alisisitiza umuhimu wa mafunzo kwa askari polisi na kusema mageuzi hayo hayapaswi kubaki katika kubadilisha majina au kauli tu, bali yajikite katika mafunzo ya kitaalamu ya utoaji huduma mambo ambayo yameshauriwa na Tume.

Alifafanua, kulikuwepo juhudi za kuliwezesha Jeshi la Polisi lionekane kama sehemu ya jamii, jambo lililosaidia wananchi kuliona kama chombo cha msaada badala ya hofu.

KAULI YA WAZIRI

Juzi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Simbachawene aliweka wazi maelekezo ya Rais Dk. Samia yanayolenga kufanya mabadiliko makubwa kwa Jeshi la Polisi nchini.

Mabadiliko hayo ni pamoja na kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo na kurejesha uhusiano mzuri kati yake na wananchi.

Katika maelekezo hayo ya Rais, Simbachawene alisema , yanahusu pia mabadiliko kutoka matumizi ya nguvu, kuwa la kutoa huduma na urekebishaji wa sheria katika ukamataji wa watuhumiwa wa makosa mbalimbali.

Previous Post

MKULIMA MBARONI AKITUHUMIWA KUUA 

Next Post

MADHARA YA MVUA

Next Post
MADHARA YA MVUA

MADHARA YA MVUA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAHITAJI YA UMEME YAONGEZEKA KWA WASTANI WA 10-15% KILA MWAKA

MAHITAJI YA UMEME YAONGEZEKA KWA WASTANI WA 10-15% KILA MWAKA

3 weeks ago
FEI TOTO AAHIDI MAKUBWA CAFCC

FEI TOTO AAHIDI MAKUBWA CAFCC

5 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?