• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 18, 2025
in Habari, Kitaifa
0
MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba

0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuzinduliwa Januari mwakani.

Aidha, Dk. Mwigulu, amezitaka hospitali zote nchini, zijiandae na bima ya afya kwa wote, wakiwemo, watoto, wanawake hususan wajawazito na wazee.

Alitoa maagizo hayo, alipozungumza na wananchi baada ya kukagua uharibifu wa miundombinu mbalimbali, ukiwemo mzani wa magari (Mpemba), Mahakama ya Mwanzo Tunduma na Soko la Machinga, katika ziara ya kikazi mkoani Songwe.

Dk. Mwigulu, alisema hatua hiyo ni sehemu ya ahadi za Rais Samia Suluhu Hassan, alizodhamiria kutekeleza katika kipindi cha siku 100 akiwa madarakani.

Alisema ahadi hizo, zinapaswa kuanza mara moja kama utoaji ajira za wahudumu wa afya 5,000, wauguzi na wakunga.

Alisema usaili wa wataalamu hao wa afya, ulianza Desemba 10, mwaka huu na unatarajiwa kukamilika wiki hii katika kila mkoa, ifikapo Januari, mwakani, wataalamu hao, watakuwa tayari katika majukumu yao.

“Ndani ya siku 100, walimu 7,000 watakuwa wameajiriwa, hivi tunavyoongea, usaili unaendelea kila mkoa kuajiri walimu hao, wakiwemo wa masomo ya sayansi, ifikapo Januari mwakani, walimu watakuwa wameajiriwa na kuendelea na majukumu ya kazi,”alisema.

Aidha, alitoa maelekezo kwa wasimamiaji wa usaili huo kuwa, hawapaswi kubagua mtu kwa itikadi ya udini, ukabila au kuwaweka ndugu zao katika ajira hizo, badala yake, wazingatie wenye sifa na uwezo wa fani hizo.

Vilevile Dk. Mwigulu, alisema kuanzia ndani ya siku 100 alizosema Rais Dk. Samia, kusiwe na hospitali inayozuia mwili wa marehemu kwa sababu ya ndugu kutokuwa na fedha za kulipa gharama.

“Naelekeza kila mkoa kufuatilia utekelezaji uliotolewa na Rais Dk. Samia na pasiwepo mtu anakataliwa matibabu kwa sababu, hajatoa fedha, nimesema mama mjamzito akifikia uchungu, aanzie kwanza na matibabu.

“Mtu yeyote aliyeletwa kwa dharura hospitalini, anapaswa kuanza kupatiwa matibabu, mambo ya uandikishaji yatakuja baadaye, lazima tuokoe maisha kwanza,”alisema.

Pia, Dk. Mwigulu, aliwatoa hofu wananchi kuwa, serikali itaendelea kutoa mitaji kwa vijana, wanawake na makundi maalumu, kufanya biashara kujikwamua kiuchumi.

Previous Post

BALOZI KUSILUKA ATAKA TAARIFA POTOFU ZIJIBIWE

Next Post

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA

Next Post
WAZIRI MKUU ARIDHISHWA UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAZIRI CHONGOLO AELEKEZA MIFUMO TOSCI ISOMANE

WAZIRI CHONGOLO AELEKEZA MIFUMO TOSCI ISOMANE

7 months ago
SERIKALI YAITA WADAU KUISAPOTI TAIFA STARS

SERIKALI YAITA WADAU KUISAPOTI TAIFA STARS

6 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?