• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 19, 2025
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI MKUU ARIDHISHWA UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA

WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba

0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba amesema ameridhishwa na kazi inayofanyika kwenye ujenzi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa mkoani Lindi ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 90.

“Nimefurahishwa sana na maendeleo ya mradi huu ambao ni mmojawapo ya miradi mingi ya kimkakati ambayo ikikamilika inaacha alama kwa Watanzania,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo (Ijumaa, Desemba 19, 2025) wakati akizungumza na viongozi na wananchi mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo iliyopo Kilwa Masoko, wilayani Kilwa, mkoani Lindi.

Amesema ujenzi wa bandari hiyo ya uvuvi ni mwanzo wa safari ya miradi mikubwa iliyoandikwa kwenye DIRA 2050.

“Bandari hii ni mojawapo ya miradi mingi inayofafanua kauli za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alizozitoa baada ya kuapishwa kwamba atasimamia utekelezaji wa miradi inayotoa majibu ya kero za Watanzania,”

“Tanzania inakwenda kuandika historia mpya kwenye sekta ya uvuvi, Rais Dk. Samia aliahidi kuendeleza miradi iliyoanzishwa na watangulizi wake na mmojawapo ni huu wa bandari ya uvuvi uliopo wilayani Kilwa.”

Amesema kukamilika kwa mradi huo, kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato na kubadili maisha ya Watanzania pamoja na kuongeza pato la Taifa.

“Rais Dk. Samia ni kiongozi ambaye anatekeleza miradi inayotoa majawabu ya kero za Watanzania. Ili kuhakikisha mradi huo unafanya vizuri, Rais Dkt. Samia ameahidi kununua meli tano za uvuvi ili kuharakisha ukuaji wa sekta ya uvuvi,” amesema.

Naye, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dk. Bashiru Ally amesema watahakikisha kuwa bandari hiyo inazalisha ajira, inazalisha mapato na inaendelea kuwa kielelezo cha mafanikio ya Serikali.

“Kwa vile bandari hii ni ya kisasa, tumeanza mchakato wa kuithibitisha katika viwango vya kikanda na kimataifa.”

Ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wadau kutoka sekta binafsi kwani wana nafasi kubwa ya kuwekeza kwenye eneo la mafuta (ya boti), viwanda vya uchakataji samaki na uendeshaji wa bandari hiyo.

Mapema, akitoa maelezo ya ujenzi wa bandari hiyo, Meneja Mradi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa, Mhandisi George Kwandu alimweleza Waziri Mkuu kwamba mradi huo utagharimu sh. bilioni 280 hadi kukamilika kwake.

“Mradi huu una eneo la ekari 48. Gati iliyojengwa ina urefu wa mita 315 na ina uwezo wa kupaki meli 10 na zikashusha mzigo kwa wakati mmoja.

Jengo likikamilika, tutaweza kuhifadhi tani 1,800 za samaki kwa wakati mmoja na kuzalisha tani 100 za barafu kwa siku ambayo ni mahitaji makubwa ya wavuvi kwa sasa.”

Amesema hadi sasa ujenzi wa mradi umefikia asilimia 90 na kwamba tayari sh. bilioni 209 zimeshalipwa.

Amesema pindi utakapokamilika, mradi huo utaanza kutoa ajira kwa watu 300 na katika mnyororo wa thamani, watu 30,000 watanufaika na mradi huo.

Waziri Mkuu anaendelea na ziara yake mkoani Lindi kwa kukagua ujenzi wa madaraja na ukarabati wa barabara kuu ya Marendego – Nangurukuru – Lindi – Mingoyo na kisha kuzungumza na wananchi wa Somanga.

Previous Post

MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

Next Post

MACHO YA MASHABIKI AFCON 2025 YAPO HAPA RABAT, MOROCCO

Next Post
MACHO YA MASHABIKI AFCON 2025 YAPO HAPA RABAT, MOROCCO

MACHO YA MASHABIKI AFCON 2025 YAPO HAPA RABAT, MOROCCO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

BALOZI DK.  NCHIMBI ATAJA MISINGI YA CCM

BALOZI DK.  NCHIMBI ATAJA MISINGI YA CCM

7 months ago
DK. MIGIRO ATAJA SABABU ZITAKAZOMPA USHINDI DK. SAMIA

DK. MIGIRO ATAJA SABABU ZITAKAZOMPA USHINDI DK. SAMIA

7 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?