• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SEKTA YA VIWANDA MHIMILI UJENZI WA UCHUMI WA KATI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 20, 2025
in Habari, Kitaifa
0
SEKTA YA VIWANDA MHIMILI UJENZI WA UCHUMI WA KATI

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga

0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

DIRA ya Maendeleo ya Taifa 2050 kupitia sekta ya viwanda na biashara, imeelezwa kuwa, mhimili mkuu wa kuijenga Tanzania ya uchumi wa kati, wa juu, shirikishi na yenye ajira nyingi.

Aidha, serikali imesisitiza kuwa, vijana ni nguvu kazi muhimu na walengwa wakuu wa mageuzi ya kiuchumi.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema Dira ya 2050, inaweka mkazo katika maendeleo ya viwanda kama msingi wa kuongeza thamani ya rasilimali, kupanua wigo wa ajira, kupunguza uagizaji bidhaa kutoka nje na kuongeza mauzo ya bidhaa za Tanzania katika masoko ya kikanda na kimataifa.

Alifafanua kuwa, kupitia sekta ya biashara, Dira hiyo inalenga kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika masoko ya nje, ambapo thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi, imeendelea kuongezeka, pamoja na jitihada za kupunguza nakisi ya biashara kwa kuongeza uzalishaji wa ndani na uongezaji thamani wa bidhaa.

Waziri huyo, alisema Dira ya 2050, inatambua sekta binafsi kama injini ya ukuaji wa uchumi, huku serikali ikiendelea kuwa mwezeshaji kupitia sera rafiki, sheria zinazochochea uwekezaji na miundombinu imara, kwa kuzingatia ushiriki wa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Akizungumzia utekelezaji wa Serikali ya Awamu ya Sita, waziri alisema katika kipindi cha miaka minne iliyopita, imefanya maboresho makubwa ya sera na sheria, kuboresha mazingira ya biashara, ikiwemo kuhuisha Sera ya Taifa ya Biashara, Sera ya Maendeleo Endelevu ya Viwanda na sera za kuendeleza wajasiriamali wadogo na wa kati.

Alisema maboresho hayo, yameanza kuleta matokeo chanya ikiwemo kuongezeka kwa mauzo ya nje ya bidhaa na huduma, hususan bidhaa za viwandani na kilimo zilizoongezwa thamani, sambamba na kupanuka kwa masoko ya kikanda kupitia Soko Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).

Kwa mujibu wa waziri, sekta ya viwanda, imeendelea kuimarika, mchango wake katika pato la taifa umeongezeka, hali inayoonesha uimara wa uzalishaji wa ndani na ongezeko la thamani ya bidhaa zinazozalishwa viwandani.

Aliongeza kuwa, serikali imeendelea kufungua masoko mapya barani Afrika, Ulaya na Asia, hatua inayotoa fursa kubwa kwa Watanzania, hususan vijana, kushiriki katika biashara za kuuza nje bidhaa za kilimo, viwandani, mavazi na bidhaa nyingine zilizoongezwa thamani.

Katika kuboresha mazingira ya biashara, waziri alisema serikali imeimarisha mifumo ya kidijitali ya usajili na utoaji leseni kupitia BRELA na taasisi nyingine, hatua iliyorahisisha urasimishaji wa biashara na kuongeza idadi ya kampuni, majina ya biashara, leseni na hataza nchini.

Alieleza kuwa, juhudi hizo zimechangia kuongezeka kwa viwanda vipya, akitolea mfano Mkoa wa Pwani ambako ndani ya miaka minne viwanda vimeongezeka kwa zaidi ya 200, hali iliyoambatana na ongezeko la ajira.

Judith alibainisha kuwa, utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati kama Mchuchuma na Liganga, Magadi Soda Engaruka, Maganga Matitu na Katewaka unatarajiwa kuzalisha maelfu ya ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, huku vijana wakiwa wanufaika wakuu.

Aidha, serikali imeendelea kuwekeza katika kongani za viwanda nchi nzima, zikiwemo Kwala na Mlandizi, ambazo zitatoa nafasi kubwa za ajira, ubunifu na biashara, pamoja na kuimarisha minyororo ya thamani ya uzalishaji.

Katika kuimarisha ujasiriamali, waziri alisema taasisi kama SIDO, TIRDO, TEMDO na CAMARTEC, zimeendelea kutoa mafunzo, teknolojia na huduma za uatamizi kwa vijana, sambamba na kuwaunganisha na masoko, viwango vya ubora na mitaji.

Alisema serikali imeongeza upatikanaji wa mikopo nafuu kupitia mifuko mbalimbali na benki za biashara kwa lengo la kuwawezesha vijana kuanzisha na kukuza viwanda vidogo, biashara za uzalishaji na ubunifu wa teknolojia.

Previous Post

KICHEKO WAKANDARASI WANAWAKE

Next Post

VIJUE VIGOGO SABA VITAKAVYOTIKISA AFCON NA KOMBE LA DUNIA

Next Post
VIJUE VIGOGO SABA VITAKAVYOTIKISA AFCON NA KOMBE LA DUNIA

VIJUE VIGOGO SABA VITAKAVYOTIKISA AFCON NA KOMBE LA DUNIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA ATAJA SABABU MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

RAIS DK. SAMIA ATAJA SABABU MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

4 months ago
YANGA, SIMBA TAMBO TUPU

YANGA, SIMBA TAMBO TUPU

2 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?