• ePaper
Friday, May 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

 WAZIRI GWAJIMA AANIKA MIZIZI YA UKATILI NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 28, 2025
in Habari, Kitaifa
0
 WAZIRI GWAJIMA AANIKA MIZIZI YA UKATILI NCHINI

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima

0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima, amesema ukatili unaoendelea kushuhudiwa katika jamii, kwa kiasi kikubwa unatokana na mila, desturi na mitazamo kandamizi inayorithishwa kizazi hadi kizazi bila kupitiwa upya.

Pia, amesema mapambano dhidi ya ukatili siyo jukumu la serikali au wizara pekee, bali ni la jamii nzima.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Dk. Gwajima alisema bado kuna jamii zinazolazimisha ndoa kwa watoto walio chini ya umri, hususan baada ya kumaliza elimu ya msingi au kubalehe, jambo alilolitaja kuwa ukatili wa moja kwa moja unaokiuka ridhaa na haki za mtoto.

“Mtoto anamaliza darasa la saba au kavunja ungo, anaandaliwa kuolewa kwa nguvu kwa kisingizio cha mila au maslahi ya kifamilia. Huu ni ukatili. Mtoto hana ridhaa na baadaye huishi maisha ya mateso, migogoro na vurugu,” alisema.

Dk. Gwajima alifafanua kwamba athari za vitendo hivyo hujitokeza baadaye, mtoto akifikia umri wa ujana au utu uzima huanza kutambua kuwa alilazimishwa katika maisha asiyoyachagua, hali inayosababisha migongano ya kifamilia, vurugu na mzunguko mpya wa ukatili.

Aidha, alisema ukatili wa kimfumo kwa watoto yatima, akieleza kuwa jamii nyingi hushuhudia watoto wakinyang’anywa mali baada ya kufiwa na wazazi bila kuchukua hatua.

“Jamii inakaa kimya mtoto anadhulumiwa mali, anakosa malezi, elimu ya maadili, mwishowe anakimbilia mitaani ambako anakumbana na ukatili mwingine, matumizi ya dawa za kulevya na mimba za utotoni,” alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Gwajima, hali hiyo huzaa kizazi kinachokosa mwelekeo, huku jamii ileile ikija kulalamika baadaye kuhusu uhalifu na vitendo vya ukatili vinavyofanywa na vijana waliotelekezwa.

Akisisitiza mkakati wa pamoja, Dk. Gwajima aliwahimiza wananchi kutokaa kimya wanapoona dalili za ukatili, bali kutumia mifumo iliyopo kutoa taarifa mapema.

“Tuna serikali za mitaa, viongozi wa kata, madiwani, wabunge, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya na mikoa. Kuna namba za simu na hata ujumbe mfupi wa maandishi kwa simu za kawaida. Taarifa ikitolewa mapema, hatua huchukuliwa mapema,” alisema.

Alihitimisha kwa kusisitiza kuwa mapambano dhidi ya ukatili yanahitaji mabadiliko ya fikra, mapitio ya mila na desturi na ujasiri wa jamii kusema “hapana” pale haki za binadamu zinapokiukwa.

“Mikakati ya kupambana na ukatili ni mipana kuliko serikali au wizara moja. Ni wajibu wetu sote kama jamii,” alisisitiza.

Previous Post

MZEE KIMITI, HAMAD WAASA WANANCHI KUSHIRIKI KIKAMILIFU TUME YA JAJI CHANDE

Next Post

MKULIMA MBARONI AKITUHUMIWA KUUA 

Next Post
MKULIMA MBARONI AKITUHUMIWA KUUA 

MKULIMA MBARONI AKITUHUMIWA KUUA 

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MASAUNI ATAKA WANAHABARI KUELIMISHA MUUNGANO

MASAUNI ATAKA WANAHABARI KUELIMISHA MUUNGANO

5 months ago
MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

MAMBO SAFI BIMA YA AFYA KWA WOTE

5 months ago

Popular News

  • YANGA MBELE KWA MBELE

    YANGA MBELE KWA MBELE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WATAALAMU WAFUNGUKA MITAZAMO YA MIKATABA 8

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?