• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SMZ KUTENGA TRIL. 1/- BAJETI WIZARA YA ELIMU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 29, 2025
in Habari, Kitaifa
0
SMZ KUTENGA TRIL. 1/- BAJETI WIZARA YA ELIMU
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na HANIFA RAMADHANI, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), inatarajia kutenga sh. trilioni moja kwa bajeti ijayo ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Alisema sekta ya elimu ina mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi, hivyo lazima serikali itoa kipaumbele cha kwanza.

Rais Mwinyi, alisema hayo katika  ufunguzi wa Shule ya Msingi Muungano Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, katika shamrashamra za maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Alisema fedha hizo, zitaboresha miundombinu ya elimu, ukiwemo ujenzi wa shule za ghorofa, vifaa vya kisasa vya kujifunzia, kufundishia na kuimarisha matumizi ya teknolojia shule za msingi na sekondari.

Alisisitiza uwekezaji wa elimu msingi muhimu ni kwa maendeleo ya taifa na aliwataka wadau wa elimu, kushirikiana na serikali, watoto wapate elimu bora.

Akizungumzia teknolojia, Rais Mwinyi alisema serikali inatarajia kuwaandaa watoto mapema, kuwajengea uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya dunia.

Aliridhishwa na viwango vya ubora katika shule hiyo, ikiwa ndiyo ya kwanza ya ghorofa tatu kwa shule za msingi Zanzibar.

Alisema shule hiyo ina madarasa mazuri yenye samani za kisasa, hivyo wanafunzi watajifunza vyema.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Khamis Abdallah, alisema sh. bilioni 6.1, zimetumika kwa ujenzi wa shule hiyo ulioanza Mei, 2023.

Shule hiyo, ndiyo pekee yenye ghorofa tatu, ina madarasa 42, ofisi ya mwalimu mkuu, ofisi nne za walimu, ukumbi wa mitihani, maabara mbili na chumba cha TEHAMA.

Previous Post

MADHARA YA MVUA

Next Post

STARS: TUNISIA INAKAA

Next Post
STARS: TUNISIA INAKAA

STARS: TUNISIA INAKAA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

NI ZIARA YA KIUCHUMI

NI ZIARA YA KIUCHUMI

2 months ago
RAIS DK. SAMIA ANAVYOENDELEA KUVUTIA JAMII YA KIMATAIFA

RAIS DK. SAMIA ANAVYOENDELEA KUVUTIA JAMII YA KIMATAIFA

2 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?