• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI GHARAMA NAFUU ZA BANDO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 28, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA YASHIKA NAFASI YA PILI GHARAMA NAFUU ZA BANDO
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na FRED ALFRED, Dodoma

TANZANIA imetajwa kuwa nchi ya pili Afrika Mashariki kwa kuwa na gharama ndogo za vifurushi vinavyotumika katika mitandao ya simu.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jijini hapa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Switbert Mkama, alipojibu swali la nyongeza la Condester Sichalwe Mbunge wa Momba- CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua mkakati wa serikali kukaa na watoa huduma za intaneti kutoka taasisi binafsi kupunguza gharama za vifurushi.
Akijibu swali hilo, Dk. Mkama alisema serikali tayari ilishakaa na watoa huduma hao na kupunguza bei za vifurushi.

“Hivi sasa ukiondoa nchi ya Rwanda, Tanzania ndiyo nchi yenye vifurushi nafuu zaidi kuliko nchi nyingine zote. Tutaendelea kukaa na taasisi binafsi kuangalia namna ambavyo tunaweza kuboresha zaidi kupungua kwa gharama za vifurushi kufikia uchumi wa kidijiti,” alisema.

Katika hatua nyingine, Dk. Mkama alisema serikali inatambua umuhimu wa upatikanaji huduma za mawasiliano kwa gharama nafuu.

Alisema wizara kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), imeendelea kuchukua hatua kuhakikisha huduma za simu, intaneti na data zinakuwa na bei rafiki kwa wananchi.

“Hatua zilizochukuliwa ni kusimamia ushindani wa haki miongoni mwa kampuni za simu kuchochea ubunifu na upatikanaji vifurushi vya gharama nafuu vinavyokidhi uwezo wa wananchi, kufanya mapitio ya gharama na tozo mbalimbali kuhakikisha utozaji unazingatia gharama halisi za huduma na kumlinda mlaji wa mwisho,” alisema.

Naibu Waziri huyo alisema hatua nyingine ni kuhimiza matumizi ya miundombinu ya pamoja  kwa kupunguza gharama za uendeshaji, kuendeleza ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano maeneo ya vijijini, maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara na ujenzi wa vituo vya kuhifadhi data.

Kwa mujibu wa Naibu waziri huyo, hatua hiyo inachangia kushuka kwa gharama za huduma hususan intaneti ya faiba nyumbani na ofisini.

Previous Post

‘BIRTHDAY’ YA MAZINGIRA

Next Post

PAPA LEO AAHIDI KUIOMBEA TANZANIA AMANI, UTULIVU

Next Post
PAPA LEO AAHIDI KUIOMBEA TANZANIA AMANI, UTULIVU

PAPA LEO AAHIDI KUIOMBEA TANZANIA AMANI, UTULIVU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA 10 CBE

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA JENGO LA GHOROFA 10 CBE

1 month ago

RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

1 day ago

Popular News

  • MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    MAFANIKIO YA KISHINDO SGR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYAMBUI AFUNGUKAAMANI KATIKA MICHEZO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, MBEYA CITY KAZI IPO LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AFICHUA KUWA NA KIPAJI CHA SOKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?