• ePaper
Thursday, June 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

MKWASA, MOGELLA, PAWASA WAIPA MCHONGO YANGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 5, 2026
in Burudani, Kitaifa, Michezo
0
MKWASA, MOGELLA, PAWASA WAIPA MCHONGO YANGA
0
SHARES
12
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

WACHEZAJI wa Yanga wamekiwa kutumia nafasi watakazopata katika mchezo dhidi ya FAR Rabat ya Morocco kushinda pambano la hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga itakuwa ugenini keshokutwa kupambana na FAR Rabat katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Stade Olympique, Rabat kianza saa 4:00 usiku.

Katika mchezo huo, Yanga inatakiwa kushinda kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano.

Kuelekea mchezo huo, baadhi ya wachambuzi wa soka wametoa maoni yao kuhusu mchezo huo.

Kiongozi na mchezaji  wa zamani wa Yanga na kocha wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa alisema kuwa anajua hautakuwa mchezo rahisi kwao lakini Yanga wanatakiwa kufanya mashambilizi ya mapema.

 “Wanatakiwa kupambana kwa jasho na damu lakini kupata mabao ya mapema katika kipindi cha kwanza, lengo  wakirejea  kipindi cha pili wazuie magoli,” alisema Mkwasa.

Naye mchambuzi wa masuala ya soka chini, Kennedy Mwaisabula alisema Yanga huo ni mchezo wa kufa au kupona hivyo wanatakiwa kutumia nguvu zao zote kupata ushindi.

 “Ni muhimu Yanga kupata ushindi katika mchezo huu, hivyo wachezaji wanatakiwa kujitoa kwa jasho na damu kupata ushindi  na wanatakiwa kila nafasi wanayoipata waitumie vizuri,” alisema Mwaisabula.

Nyota wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa alisema kwanza Yanga wanatakiwa kupongezwa kwa kazi kubwa waliyoifanya.

 “Kubwa ambalo Yanga wanatakiwa kufanya ni kushinda magoli mengi ya mapema ili kipindi cha pili wazuie magoli waliyoyapata,” alisema Pawasa.

Nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella alisema wachezaji wa Yanga wanatakiwa kufuata kile ambacho mwalimu atawafundisha.

“Sina shaka na Yanga katika suala la kupambana, ninachoweza kuwaambia wanatakiwa kufuata kile ambacho mwalimu amewafundisha kutimiza malengo waliojiwekea,” alisema Mogella.

Kwa sasa, msimamo wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaongozwa na Al Ahly yenye pointi 8, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 5 sawa na FAR Rabat huku JS Kabylie ikiwa na alama mbili.

Previous Post

HATMA YA MANGUNGU BAADA YA SIMBA, ATLETICO

Next Post

SIRI SIMBA YAVUJA

Next Post
SIRI SIMBA YAVUJA

SIRI SIMBA YAVUJA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA ATIA NENO BEI MAFUTA

RAIS DK. SAMIA ATIA NENO BEI MAFUTA

1 month ago
DK. SAMIA AMELETA MIRADI MIKUBWA LINDI – MAJALIWA

DK. SAMIA AMELETA MIRADI MIKUBWA LINDI – MAJALIWA

9 months ago

Popular News

  • WABUNGE: AMANI ISICHEZEWE

    WABUNGE: AMANI ISICHEZEWE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAKAGUZI WA CAF WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA VIWANJA VYA AFCON 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MKAKATI KUDHIBITI VIFO WAJAWAZITO WAANIKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?