• ePaper
Friday, May 15, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

SABABU SARE AZAM, YANGA SC IKO HAPA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 17, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
SABABU SARE AZAM, YANGA SC IKO HAPA
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAKATI Kocha wa Azam FC, Florent Ibenge akiweka wazi hatua ya kikosi chake kushindwa kutengeneza nafasi za kufunga ndiyo sababu ya kutoshinda, Pedro Goncalves wa Yanga amesema uchovu wa wachezaji wake ni miongoni mambo yaliyochangia kukosa pointi tatu dhidi ya wapinzani wake hao juzi.

Azam FC na Yanga zilitoka sare juzi katika mchezo wa dabi ya Ligi Kuu Tanzania Bara maarufu Dar es Salaam Dabi uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mtanange huo uliokuwa na ushindani wa aina yake, asilimia kubwa ya mpira ulikuwa ukichezwa katikati ya uwanja huku timu zote zikishindwa kutengeneza nafasi za wazi kuandika mabao.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Kocha Ibenge alisema Azam FC ilianza vyema kipindi cha kwanza kwa kutawala mechi lakini sababu kubwa ya kutoandika bao ni kukosa umakini wa kutengeneza nafasi za wazi.

Ibenge alisema lengo lake lilikuwa ni kuvuna pointi tatu, lakini kushindwa kutengeneza nafasi za wazi ilikuwa sababu tosha ya kutofunga bao.

“Tulianza vizuri na tulikaa vyema na mpira, lakini bahati mbaya tulishindwa kutengeneza nafasi za mabao.

Hongera kwa Yanga kwa kutulazimisha sare nyumbani, lakini sasa tuna kazi kuhakikisha tunakwenda Kigoma (dhidi ya Mashujaa) kuwania pointi tatu,” alisema.

Kocha wa Yanga, Pedro alisema ilikuwa mechi ngumu, lakini uchovu wa wachezaji wake baada ya kucheza mechi mfululizo, ilichangia kutokuwa bora uwanjani.

“Ilikuwa mechi ngumu, tulikuwa na ratiba ngumu, kama tungepata muda wa kupumzika zaidi kabla ya mechi hii, ninafikiri tungekuwa bora zaidi.

Tunachukua pointi moja tuliyopata, najua siyo tulichokuwa tunapambania lakini tunaichukua hii na kujielekeza zaidi katika mechi ya Jumatano (kesho),”  alisema.

Kuanzia Februari 22 hadi juzi ambapo ni sawa na siku 22, Yanga imecheza jumla ya mechi sita za Ligi Kuu Bara ambazo ni sawa siku nne kila baada ya mechi moja (ukiondoa mechi za FA).

Katika siku hizo, Yanga ilishinda mechi nne dhidi ya Namungo (1-0), JKT Tanzania (5-0), Singida Black Stars (3-0) na Tanzania Prisons (1-0) na kutoka sare dhidi ya Simba (0-0) na Azam FC (0-0).

Yanga ndiyo kinara wa ligi hiyo ikiwa na pointi 36 baada ya kushuka dimbani mara 14 ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 28 katika mechi 14.

Previous Post

UWEKEZAJI NSSF WA MZIZIMA TOWERS KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA NA UTALII DAR

Next Post

HAPATOSHI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Next Post
HAPATOSHI LIGI YA MABINGWA ULAYA

HAPATOSHI LIGI YA MABINGWA ULAYA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MANNY PACQUIAO KUTUA BONGO NA MAMBO MAWILI

MANNY PACQUIAO KUTUA BONGO NA MAMBO MAWILI

4 months ago
MABAO 104 YAFUNGWA LIGI KUU BARA

MABAO 104 YAFUNGWA LIGI KUU BARA

5 months ago

Popular News

  • MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

    MTIFUANO MKALI NNE BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI KISASI SIMBA QUEENS,YANGA LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA YAGEUZA KIBAO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NEEMA YAWASHUKIA WAVUVI NA WAFUGAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIHONGOSI AKEMEA ‘WANAOVIMBA’ CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?