• ePaper
Thursday, June 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

UWEKEZAJI NSSF WA MZIZIMA TOWERS KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA NA UTALII DAR

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
March 17, 2026
in Habari, Kitaifa
0
UWEKEZAJI NSSF WA MZIZIMA TOWERS KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA NA UTALII DAR
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI imesema mradi wa uwekezaji wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi la Mzizima Towers unaotekelezwa jijini Dar es Salaam na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umefikia asilimia 91 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika rasmi ifikapo Desemba 31, 2026.

Taarifa hiyo imetolewa Machi 16, 2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, alipowasilisha taarifa ya maendeleo ya mradi huo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii.

Kwa mujibu wa Waziri Sangu, mradi huo wa uwekezaji unahusisha ujenzi wa minara miwili, ikiwemo mnara wa biashara wenye ghorofa 35 na mnara wa makazi wenye ghorofa 32, ukiwa na jumla ya eneo la ujenzi la mita za mraba 95,018.15.

Amesema majengo hayo yamebuniwa kwa kuzingatia viwango vya kisasa vya usanifu wa kimataifa ili kukidhi mahitaji ya biashara, makazi na huduma za utalii katika jiji la Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utakuwa na hoteli ya hadhi ya nyota tano itakayoendeshwa na Radisson Hotel Group, yenye jumla ya vyumba 156 vya kulala pamoja na vyumba 132 vya makazi ya muda mfupi (hotel apartments).

Sangu alisema mradi huo unatekelezwa kwa asilimia 100 na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kama sehemu ya mkakati wa Mfuko huo kuwekeza katika miradi mikubwa ya kimkakati yenye tija kwa wanachama na taifa kwa ujumla.

Alibainisha kuwa uwekezaji huo unalenga kuongeza thamani ya mali za Mfuko pamoja na kuimarisha uwezo wake wa kulipa mafao kwa wanachama.

Akizungumza baada ya ziara ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Hawa Mchafu Chakoma, alisema wajumbe wa kamati wanamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuamua mradi huo uendelee kutekelezwa ili uweze kuleta tija kwa Mfuko na Taifa kwa ujumla.

“Sisi kamati tumefika hapa na kujionea kazi inayofanyika katika mradi huu. Kazi ni nzuri sana na inaonesha kuwa uongozi wa NSSF chini ya Mkurugenzi Mkuu, Bw. Masha Mshomba, umekuwa mfano wa kuigwa katika usimamizi wa miradi,” alisema Hawa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba, aliwashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa kufanya ziara ya kikazi na kujionea maendeleo yaliyofikiwa katika mradi huo.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo akiwemo Mhe. Kafiti Kafiti waliipongeza NSSF kwa uwekezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa taifa na jamii kwa ujumla.

Naye, Kangi Lugola alisema mradi wa Mzizima Towers ni uwekezaji muhimu wenye tija kubwa kwa Mfuko na Taifa kwa ujumla, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kwa usimamizi mzuri wa Mfuko na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mradi wa Mzizima Towers unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kiuchumi ikiwemo kuongeza mapato ya Mfuko na Serikali, kuimarisha sekta ya biashara na utalii jijini Dar es Salaam pamoja na kuongeza ajira, ambapo zaidi ya wafanyakazi 300 wameajiriwa wakati wa ujenzi wa mradi huo, huku ajira zaidi ya 250 zikitarajiwa kupatikana mara baada ya kuanza kwa shughuli za hoteli na biashara ndani ya jengo hilo.

Previous Post

MELI KUBWA NNE ZA MIZIGO KUIFUNGUA TANZANIA KIUCHUMI

Next Post

SABABU SARE AZAM, YANGA SC IKO HAPA

Next Post
SABABU SARE AZAM, YANGA SC IKO HAPA

SABABU SARE AZAM, YANGA SC IKO HAPA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA ATUMA UJUMBE WA AMANI

RAIS DK. SAMIA ATUMA UJUMBE WA AMANI

6 months ago
MPINZANI WA MWAKINYO HADHARANI

MPINZANI WA MWAKINYO HADHARANI

6 months ago

Popular News

  • WABUNGE: AMANI ISICHEZEWE

    WABUNGE: AMANI ISICHEZEWE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE WAIPONGEZA NSSF NA PSSSF KWA KUANZISHA SKIMU YA HIFADHI KWA WALIOJIAJIRI NA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA NGOZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE WAPONGEZA UWEKEZAJI KLICL

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAKAGUZI WA CAF WARIDHISHWA NA MAENDELEO YA VIWANJA VYA AFCON 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MKAKATI KUDHIBITI VIFO WAJAWAZITO WAANIKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?