• ePaper
Saturday, June 20, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KIHONGOSI AWAPONDA VIONGOZI CHADEMA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 19, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KIHONGOSI AWAPONDA VIONGOZI CHADEMA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MUSSA YUSUPH

KATIBU wa NEC, Siasa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kenani Kihongosi, amekemea mwenendo mbaya wa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani, kupotosha wananchi na kuchochea vurugu.

Amesema viongozi hao waliofilisika kisiasa, wamekuwa wakiwahadaa wananchi kwa kudai hakuna kilichofanyika, hivyo kuchochea vurugu ilihali wao na familia zao wakiwa na makazi ughaibuni.

Kihongosi amesisitiza kwamba ili kukata mzizi wa fitina anahitaji mdahalo wa kisiasa na viongozi watano badala ya watatu aliowataka awali kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Aliwataja viongozi hao ni John Heche (Naibu Katibu Mkuu) na John Mnyika (Katibu Mkuu) Joseph Mbilinyi (Mjumbe wa Kamati Kuu) Godbless Lema (Mjumbe wa Kamati Kuu) na Boniface Jacob (Mjumbe wa Kamati Kuu).

Kihongosi alitoa msisitizo huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa sokoni, Kata ya Ruaha Mbuyuni, wilayani Kilolo mkoani Iringa, jana.

“Anasimama kiongozi wa chama cha siasa anaongea mambo ya ajabu lazima tuwakemee mapepo. Wao wamejikita katika vurugu na upotoshaji sisi tumejikita kwenye miradi ya maendeleo,” alieleza.

Alibainisha kuwa Rais Dk. Samia amefanya mambo mengi makubwa mengine ya kuvunja rekodi lakini yeye siyo kiongozi wa kuongea.

“Rais Dk. Samia kwa kuwa ni kiongozi mwenye upendo walimfuata kumuomba wafanye mikutano ya hadhara na mikutano ya kisiasa lakini sasa wanamsema vibaya.

“Kwa kuwa Dk. Samia amepewa dhamana ya kuliongoza taifa, wananchi wanashuhudia maendeleo makubwa. Asije mtu kuleta propaganda, waache uhuni kwenye mambo ya msingi.

Aliongeza: “Kuna watu wanasema hakuna kazi iliyofanyika. Hivi ukikaa peke yako hakuna jambo lililofanyika na ndiyo maana wale jamaa nawataka kwenye mkutano, Heche, Mnyika, Lema, Sugu na Boni Yai nimeongeza kutoka watatu hadi wawili.”

“Lazima tuambizane kwa ukweli tulikuwa na reli ya kisasa Mzee Magufuli aliiacha ikiwa asilimia 33 lakini sasa imekamilika nani aliyekamilisha?,” alisisitiza.

Kihongosi alisema Rais Dk. Samia amekamilisha miradi ya ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere na ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi.

Kihongosi alikemea watu wanaochonganisha wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vimesimama imara kuhakikisha ulinzi wa nchi, raia na mali zao.

Alisema mwananchi ndiye anayepaswa kulinda taifa kwani mambo yakiharibika, Watanzania watakuwa watumwa kwenye ardhi ya wageni.

Alisema Tanzania imeshakombolewa, hivyo kazi inayofanyika ni kusukuma mbele gurudumu la maendeleo na siyo watu wanaotaka kuvuruga nchi kwa kisingizio cha kutaka ukombozi.

Kihongosi alitoa wito kwa wananchi kushirikiana na serikali katika utekelezaji miradi ya maendeleo huku akisisitiza CCM kitaendelea kubeba ajenda za wananchi.

“Leo tunasimama hapa kwa kujiamini kuwa tunakwenda sehemu ambapo serikali imetekeleza jambo fulani na mambo hayo yanaonekana. Tumekuja kwa sababu eneo hili amani ipo na endapo amani ikitoweka mambo yataharibika na ndiyo maana CCM kinasisitiza kulinda amani, kudumisha upendo na mshikamano,” alisema.

Alisisitiza kuwa watu wanaohubiri kuharibu amani hawaishi katika maeneo ya wananchi, kwani wamekuwa wakiwashawishi wananchi kuharibu miundombinu na huduma za kijamii.

Kihongosi alisema watu werevu wanalinda nyumbani kwao, kwani kitendo cha kuchoma moto zahanati maana yake ni kuwafanya wananchi wapate shida ya kupata huduma za matibabu.

“Wasije watu waliochanganyikiwa duniani kuwataka kuchoma moto maduka, wajibu wetu kulinda nyumbani kwetu kulinda maendeleo hata kizazi kinachokuja kijivunie.

“Mara zote wanaohubiri uvunjifu wa amani hawaishi nchini, wana mahali mambo yakiharibika wanapo pa kukimbilia. Wanakuja kukwambia kamanda kunja ngumi, vunja kioo. Haya mambo mengine wasiwaponze,” alieleza.

Aliongeza: “Katika vurugu hakuna mwanasiasa anayeumia lakini wakija katika majukwaa ya kisiasa wanasema wamepigwa.”

“Tusije kuruhusu kubaguana kwa kanda, dini, kabila wala vyama vya siasa, kwani Tanzania ni taifa moja lenye wananchi walioshikamana,” alisisitiza.

Alisema ukiona mwanasiasa aliyeishiwa hoja kusema yeye wa upande fulani hafai na amefilisika kisiasa.

KAULI YA MWENYEKITI WA CCM

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daudi Yassin, alisema CCM mkoani hapa kipo imara kwani kimeweza kuibuka na ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana.

Pia, alisema kasi ya maendeleo katika Mkoa wa Iringa ni ushahidi wa utekelezaji Ilani ya uchaguzi ya CCM kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Katika hatua nyingine, Kihongosi alitoa wito kwa wananchi wilayani Kilolo kutoruhusu watu wanaotaka kuharibu amani ya nchi.

Alisisitiza kuwa endapo amani na utulivu itakapokosekana hakuna mwananchi atakayeweza kufanya shughuli za uzalishaji mali.

Kihongosi alitoa wito huo katika mkutano wa Shina Namba 10, Kata ya Ruaha Mbuyuni wilayani Kilolo mkoani Iringa.

“Msikubali kuharibu amani ya nchi na msikubali mtu aje awashawishi mfanye mambo yasiyofaa. Shirikianeni na viongozi wenu kuleta maendeleo,” alisisitiza.

ASHUSHA MAAGIZO UJENZI WA SKIMU

Kuhusu mradi wa skimu ya umwagiliaji Mgambalenga, Kihongosi aliagiza ujenzi wa skimu hiyo kwa gharama ya sh. bilioni 23.9, ukamilike kwa wakati.

Alisema Chama hakitarajii mkandarasi anayetekeleza mradi huo, China Railways 15 Bureau Group Cooparation, anaongezewe muda pindi muda wa ujenzi utakapomalizika.

Alisema mradi huo utawanufaisha wakulima zaidi ya 1,000 uliopo Kijiji cha Mtandika, Kata ya Ruaha Mbuyuni wilayani Kilolo mkoani Iringa.

Alisisitiza kuwa serikali imetoa fedha za mradi huo kwa lengo la kuwanufaisha wakulima na wananchi wilayani hapo, hivyo ni muhimu ujenzi wake ukamilike kama ulivyopangwa.

“Tumekuja hapa kufanya ukaguzi wa mradi huu unaogharimu zaidi ya sh. bilioni 23.9. Mradi huu utakwenda kunufaisha wakulima zaidi ya 1,129 na wale wa moja kwa moja zaidi ya wakulima 38,000.

Alisisitiza: “Serikali imechukua hatua kubwa kuhakikisha mradi huu unakuwa mkombozi kwa wakulima wa Kilolo. Rais Dk. Samia Suluhu Hassa ametoa fedha hizi nyingi ikiwa ni mapenzi makubwa kwa wananchi wa wilaya hii.”

“Tuendelee kuitenda hii kazi kwa uaminifu ili Watanzania waendelee kuona matunda ya kodi yao. Matarajio yetu mkandarasi hatoongezewa muda, Chama tunatarajia mradi ukamilike kwa wakati kwa sababu wakulima wanategemea kilimo,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Ritha Kabati, alisema serikali imedhamiria kukamilisha mradi huo.

Alisema amekubaliana na Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo kufika katika eneo mradi kuangalia hatua  za utekelezaji.

Awali, Mhandisi Mkazi wa mradi huo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) Mhandisi Gerald Kapukutu, alisema lengo la mradi huo ni kupanua mashamba ya umwagiliaji.

Alisema upanuzi huo utahusisha mashamba kutoka hekta 150 hadi hekta 1,700 ili kuongeza uzalishaji mazao, kuongeza usalama wa chakula na kuboresha maisha ya wananchi wa vijijini.

Previous Post

DHAHABU BoT HAIJAUZWA – PM MWIGULU

Next Post

OFISI YA WAZIRI MKUU YATHIBITISHA NYENZO MUHIMU ZA KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI

Next Post
OFISI YA WAZIRI MKUU YATHIBITISHA NYENZO MUHIMU ZA KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI

OFISI YA WAZIRI MKUU YATHIBITISHA NYENZO MUHIMU ZA KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA YANG’ARA MKUTANO MKUU WA KUPAMBANA NA RUSHWA JIJINI DOHA, QATAR

TANZANIA YANG’ARA MKUTANO MKUU WA KUPAMBANA NA RUSHWA JIJINI DOHA, QATAR

6 months ago
KIBU DENIS, MANULA WATEMWA STARS

KIBU DENIS, MANULA WATEMWA STARS

10 months ago

Popular News

  • OFISI YA WAZIRI MKUU YATHIBITISHA NYENZO MUHIMU ZA KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI

    OFISI YA WAZIRI MKUU YATHIBITISHA NYENZO MUHIMU ZA KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA NCHINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIHONGOSI AWAPONDA VIONGOZI CHADEMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DHAHABU BoT HAIJAUZWA – PM MWIGULU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PACOME, DEPU  WAIPA JEURI YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WABUNGE: AMANI ISICHEZEWE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?