• ePaper
Thursday, April 23, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

WADAU MICHEZO WAMTUMIA SALAMU WAZIRI MAKONDA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
January 10, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
WADAU MICHEZO WAMTUMIA SALAMU WAZIRI MAKONDA
0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

SIKU moja baada ya Paul Makonda kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, wadau wa michezo nchini wamemtumia salamu na kusisitiza kufurahishwa na uteuzi wake.

Makonda aliteuliwa kuwa Waziri wa wizara hiyo akichukua nafasi ya aliyekuwa Waziri Profesa Palamangamba Kabudi, ambapo awali alikuwa Naibu Waziri akisaidiana na Hamis Mwinjuma.

Makonda anachukua nafasi ya Kabudi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalumu).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau wa soka walisema wanamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Makonda kushika wizara hiyo kwani wanaamini atapambana kuipaisha sekta ya michezo kwa ujumla.

Kocha wa zamani wa Yanga na mchambuzi wa masuala ya michezo, Kennedy Mwaisabula ‘Mzazi’, alisema kuwa amefurahi kuona wizara hiyo imepata kiongozi kijana.

Alisema, Makonda ni mtu sahihi kwani anaamini kuwa atawaamsha waliolala kutokana na kauli zake huwa zimenyooka na anajua kutimiza majukumu yake.

“Niseme ukweli katika michezo kwa hivi sasa ameingia jembe, kwanza ni kijana, anaweza kukimbia hivyo ninaamini uwepo wa Makonda katika nafasi hiyo utachagiza maendeleo ya nchini.

“Ninampongeza Rais Dk. Samia kwa kumteua Makonda kwani kila mmoja aliona alivyokuwa akihamasisha wachezaji wa Taifa Stars walipokuwa wakishiriki michuano ya Mataifa Afrika (AFCON) na kufika hatua ya 16 bora,” alisema Mzazi.

Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Bakari Malima alisema kuwa kwanza anampongeza Rais Dk. Samia kwa uteuzi huo, kwani Makonda ni mwanamichezo kindakindaki, hivyo anaamini ataleta maendeleo katika michezo kwa ujumla.

Malima alisema kuwa Makonda anajua mpira lakini pia kuna Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba ni mwanamichezo hivyo wakikaa meza moja watafanya jambo zuri la maendeleo na kuifikisha mbali sekta hiyo nchini.

“Sisi wanamichezo kilio chetu kimesikika na Rais Dk. Samia kwa kutuletea waziri anayependa michezo, Makonda akikaa meza moja na Dk. Mwigulu tutafikia malengo katika sekta ya michezo,” alisema.

Naye promota wa ngumi za kulipwa, Meja Selemani Semunyu alisema kuwa aliyetoka ni mtu na aliyeingia ni mtu kabisa, hivyo anaimani kutokana na ujana wake ataisaidia michezo ikiwemo kuipaisha sekta ya ngumi.

“Ombi letu kwake tunajua nguvu kubwa imewekwa katika soka, mchezo ambao ni pendwa kabisa, lakini tunaomba pia atazame katika ngumi ili kuwawezesha kuendelea kufanya vizuri ndani na nje ya nchi.

“Tumeona Rais Dk. Samia alivyoweka nguvu katika michezo yote ikiwemo ngumi kwa mabondia wanaoshinda mapambano ya kimataifa, tunaamini tutafika mbali kwa muda mfupi tofauti na tulivyotarajia,” alisema Meja Semunyu.

Promota huyo alisema kuwa kutokana na ujana aliokuwa nao anaimani kubwa ataweza kuhudhuria katika matamasha yote ya mchana na usiku.

Semunyu alisema anampongeza Rais Dk.Samia kwa uteuzi huo na wataendelea kushirikiana bega kwa bega na serikali ili kuendelea kukuza ngumi hapa nchini.

Previous Post

SIMANZI WATOTO WAKIFIA NDANI YA SWIMMING POOL

Next Post

KOCHA SIMBA AJITETEA, MASHABIKI WACHARUKA

Next Post
KOCHA SIMBA AJITETEA, MASHABIKI WACHARUKA

KOCHA SIMBA AJITETEA, MASHABIKI WACHARUKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SEKTA YA UCHUKUZI YAPAA

SEKTA YA UCHUKUZI YAPAA

2 months ago
YANGASC YAIFUATA KABYLIE KIBABE

YANGASC YAIFUATA KABYLIE KIBABE

5 months ago

Popular News

  • NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

    NDEJEMBI ATAJA VIPAUMBELE 10 SEKTA YA NISHATI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU ATOA MAAGIZO ALAT

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RIPOTI YA KUPONYA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWANDAAJI MISS WORLDTZ AITAJA AMANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, MAFUNZO HAPATOSHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?