• ePaper
Sunday, August 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

WAMETISHA AISEE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
August 10, 2026
in Burudani, Habari, Michezo
0
WAMETISHA AISEE
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

ZIANA BAKARI Na NASRA KITANA

WAMETISHA aisee, baada ya klabu ya Yanga kufanya tamasha lao la Yanga Day kukonga nyoyo za wanachama na mashabiki wa soka nchini.

Yanga iliandaa tamasha hilo, lililofanyika katika Uwanja wa Uhru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwatalimbusha wachezaji wao wa msimu ujao wa 2026/27.

Katika tamasha hilo, lililoanza asubuhi na  ilipofika saa 12.30 jioni benchi zima la ufundi lilitambulishwa rasmi, likiongozwa na Kocha mpya wa Yanga, Manqoba Mngqithi.

PACOME

Pia, Pacôme Zouzoua alituma ujumbe kwa wanachama, mashabiki, wachezaji wenzake ambapo Msemaji wa klabu ya Yanga, Ally Kamwe alisema jana mchezaji huyo alishindwa kufika kwa vile alikwenda hospitali.

Akisoma ujumbe mfupi wa Pacome, Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto aliwashukuru mashabiki na kueleza Pacome anawapenda sana.

Baada ya hapo, walianza kutambulishwa wachezaji ambapo alianza Max Nzengeli, Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’,  Mudathir Yahya na wachezaji wengine.

Kivutio kikubwa katika utambulisho wa wachezaji wapya wa Yanga, kilikuwa nyimbo laini zilizokuwa zikitumbuizwa na wasanii wazungu.

 Hata hivyo, furaha ya mashabiki wa klabu ya Yanga iliibuka baada ya kipa Djigui Diarra kuongeza mkataba mpya ambapo amesaini miaka miwili.

Awali, kulikuwa na tetesi kuwa Diarra alikuwa aondoke kitu ambacho kimezimwa rasmi jana.

Pia, Yanga imewapandisha nyota wawili kutoka kikosi cha pili na kuingia kikosi cha wakubwa kwa ajili ya msimu ujao na kuwatambulisha rasmi.

Wachezaji hao ni Salehe na Kazimoto ambao msimu ujao wataonekana wakifanya vitu vyao dimbani.

MMACHINGA, DOMAYO WATOA NENO

Mshambulaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Mmachinga alisema amefurahi kuwa mmoja wa walioudhuria tamAsha hilo la kihistoria.

Alisema kitu anachojivunia kuwa hadi sasa rekodi yake ya kupachika mabao 26 katika Ligi Kuu Tanzania Bara, imekuwa ngumu kuvunjwa.

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Frank Domayo aliiupongeza uongozi wa klabu ya Yanga kwa kuandaa vizuri tamasha la Yanga Day.

WASANII

Katika tamasha la Yanga Day, waliongeza burudani kwa 

kuwakutanisha mastaa mbalimbali wa muziki Tanzania, huku wasanii muziki wa Bongo Fleva wakipewa nafasi ya kupanda jukwaani.

Miongoni mwa wasanii waliopamba tamasha hilo ni Mwasiti, Chid Benz, T.I.D, Madee, Chege, Q Chilla na Mr Blue ambao kila mmoja alitumia muda wake jukwaani kutoa burudani na kuwafanya mashabiki kuimba na kucheza.

Pia, T.I.D alivutia hisia, kutokana na historia yake kubwa katika muziki wa Bongo Fleva.

Msanii huyo ni miongoni mwa majina yaliyowahi kutawala anga la muziki Tanzania na bado ana uwezo wa kuwakumbusha mashabiki nyimbo enzi zilizopita.

Burudani hiyo, ilifanya tamasha hilo la Yanga Day kuwa tukio linalounganisha soka, muziki na mashabiki.

Lakini nyota wa filamu nchini, Prince Jimmy alisema alikwenda uwanjani kuishangilia timu yake kwa vile yeye ni shabiki wa Yanga.

JEZI NYEUSI ZATAWALA

Katika Uwanja wa Uhuru, jezi nyeusi zilivaliwa sana na mashabiki wa Yanga ambapo wengi walivaa jezi rangi hiyo.

WAFANYABIASHARA

Wakizungumza jana, baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali walisema biashara ilichangamka kutokana na mashabiki wengi kujitokeza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana, wafanyabiashara hao walisema ujio wa mchezo huo umeongeza idadi ya mashabiki wanaofika kununua jezi,vyakula.

Muuza jezi, Karimu Ali, alisema kuwa tangu afungue biashara yake, kumekuwa na ongezeko la wateja wanaotaka kununua jezi mpya, hasa wale wanaojiandaa kwenda kushuhudia mchezo huo.

Mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salaam, Neema Peter anayejishughulisha na shughuli za mama ntilie, alisema kuwa ujio wa tamasha hilo, umechangia kuongeza wateja na kuongeza kipato chake.

Muuza madafu, Juma Zorro, aliishukuru klabu ya Yanga kwa kuendelea kuandaa matukio yanayowakutanisha mashabiki yamesababisha kuongeza mtaji wake.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ANADI FURSA ZA TANZANIA

Next Post

BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

Next Post
BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WANANCHI KUSINI UNGUJA WAAHIDI KUIPIGIA KURA CCM

WANANCHI KUSINI UNGUJA WAAHIDI KUIPIGIA KURA CCM

11 months ago
RAIS DK. SAMIA AGEUKIA VITA DHIDI YA MALARIA 

RAIS DK. SAMIA AGEUKIA VITA DHIDI YA MALARIA 

6 months ago

Popular News

  • KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAMU, CHUNGU DABI YA K’KOO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA RAHA VIGOGO USHIRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?