• ePaper
Wednesday, September 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 2, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Cde SHAKA HAMDU SHAKA

AGOSTI 26, 2026, ilikuwa siku ya kihistoria. Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, ilifanya uamuzi mgumu wenye dhamira ya kubeba maslahi mapana ya Taifa.

Maamuzi hayo, yakapata baraka na kukamilika Jumamosi, Agosti 29, 2026 siku ambayo vizazi vijavyo, vitaisoma kwenye vitabu vya kumbukumbu ya nchi yetu.

Lakini kubwa kuliko yote, ni siku iliyojibu swali la vijana wengi: “Je, Taifa letu linatuona?”

Ninaandika haya siyo kama mwanasiasa, bali kama mtoto na kijana wa nchi hii. Ninaandika kutoa shukrani, pongezi na kutoa matumaini kwa vijana na Watanzania kwa ujumla, kufuatia uteuzi wa Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

SHUKRANI KWA RAIS SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Watanzania na dunia, tumetambua kazi yako. Tumeona utulivu wako wakati wa dhoruba, tumeona hekima yako katika diplomasia na tumeona upendo wako kwa maskini, mwanamke na mtoto.

Kama ilivyokuwa mwaka 1964 na Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano, umeongeza ukurasa mpya kwenye historia. Umeonesha kuwa, wewe ni kiongozi anayesikiliza, anayejifunza na anayebadilika kulingana na mahitaji ya wakati.

Kwa kumteua  Makamu wa Rais, Deo Ndejembi,  umefanya mambo  manne makubwa:

Moja, umeimarisha Umoja:  umeonesha kwa vitendo kuwa, Tanzania ni ya wote – wazee, vijana na rika zote.

Mbili, umejenga matumaini; umeonesha kuwa kila kijana ana nafasi ya kulitumikia Taifa lake.

Tatu; umeongeza kasi, umeleta nguvu mpya serikalini ambayo itakuwa chachu ya maendeleo endelevu.

Jambo la nne, umeonesha Dira: umethibitisha kwa vitendo kuwa unafikiria Tanzania ya 2050, siyo 2026 tu.

Rais Samia, wewe ni mama wa taifa na mama wa matumaini ya vijana. Historia itakukumbuka kama kiongozi uliyethubutu. Tunakushukuru.

PONGEZI KWA KAKA YETU

Mheshimiwa Deo Ndejembi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa niaba ya vijana wa mitaani, vyuo, mashamba na masoko – Hongera sana!

Wewe ni mmoja wetu. Umeota na sisi, umeumia na sisi. Dhamana hii siyo bahati. Ni matokeo ya kazi, nidhamu na uaminifu wako kwa Taifa.

Tunajua mzigo ni mzito. Lakini tuna imani una nguvu ya kuubeba. Jukumu letu ni kukuombea wewe na Mheshimiwa Rais na kuwasaidia pale inapohitajika.

Matumaini ya vijana kwako, yapo katika maeneo matatu:

Moja kuwa sauti yetu, tukumbushe kwenye vikao vya juu kuwa, kuna kijana anataka mtaji, kuna mhitimu anataka ajira.

Mbili, kuwa kioo: Onyesha vijana kuwa nidhamu na kazi ndiyo ufunguo. Kama alivyosema Mheshimiwa Rais: _”Tumeamua kuwamini tena vijana. Nenda kafanye kazi.”_

Tatu kuwa msaada: Msaidie Mheshimiwa. Rais kutimiza ahadi zake kwa kasi.

Mheshimiwa Ndejembi, usiogope wala kujiona mgeni. Taifa zima lipo nyuma yako. Mhe. Rais ni mstari wako wa mbele.

KWANINI NI “TURUFU YA MAENDELEO”

Kihesabu ni rahisi: Dk. Samia + Ndejembi = Turufu ya maendeleo.

Gari kubwa kama Tanzania, haliendi kwa gurudumu moja. Linahitaji turufu yenye nguvu:

Silinda ya Kwanza: Uzoefu na ustawi – Dk. Samia

Uzoefu wa serikalini, mahusiano na dunia, utulivu na moyo wa huruma.

Silinda ya Pili, Nguvu na ubunifu – Mheshimiwa Ndejembi 

Uelewa wa lugha ya vijana, kasi ya kufika mashinani, mawazo ya uchumi wa kidijitali na ujasiri wa kuuliza “kwa nini tusifanye tofauti?”

Pamoja, turufu hii italeta matokeo katika:

1.  AJIRA:  Kuunganisha sera za viwanda + mawazo ya ‘startup’

2.  MIRADI MIKUBWA: SGR, Bandari, Nishati – uangalizi wa karibu

3.  KILIMO: Teknolojia + Masoko ya Kimataifa

4.  ELIMU NA AFYA: Ubunifu wa kidijitali ufike shule na zahanati

5.  UMOJA: Kiongozi Mwanamke + Kiongozi Kijana = Tanzania Moja

MWITO KWA TAIFA

Kijana acha kulalamika, tumia fursa. Nchi imefungua mlango.

Kwa Wafanyabiashara; Nchi ni shwari njooni muwekeze serikali ipo.

Viongozi wa Dini: ombeeni na muwe mabalozi wa amani.

Vyombo vya habari: vieneze ukweli na matumaini.

Kila Mtanzania ailinde Tanzania kwa wivu, maendeleo kwa kuwa bila amani ni ndoto kufanikiwa.

Kama vijana tunasema kwa sauti moja: “Mheshimiwa Rais Samia, Mheshimiwa Makamu wa Rais, Ndejembi, tuko tayari kufanya kazi nanyi.

Mwenyezi Mungu, wape msaada katika kuwatumikia Watanzania, nyoosha hatua zao, wape hekima Luqman, uvumilivu wa Ayubu, na nguvu za Suleiman. Wabariki na uwape afya ili taifa liendelee kusonga mbele.

Tumefunga ukurasa wa matumaini na kufungua wa Kazi, Matumaini na Maendeleo.

Asante Dk. Samia Suluhu Hassan kwa ujasiri,  

Hongera Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi kwa dhamana uliyoaminiwa. Wananchi wajibu uko kwetu.

Kazi na Utu Tunasonga Mbele.

Previous Post

WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UBINGWA LIGI KUU WAWATEGA BARKER, PEDRO 

UBINGWA LIGI KUU WAWATEGA BARKER, PEDRO 

6 months ago
MAKONDA AJITOSA MABADILIKO SIMBA

MAKONDA AJITOSA MABADILIKO SIMBA

7 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    RAIS DK. SAMIA, NDEJEMBI TURUFU YA MAENDELEO KWA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI AONYA, ATOA SIKU 60 WENYE SILAHA HARAMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NDEJEMBI MZIGONI RASMI, AKEMEA KAZI KWA MAZOEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUME MIPANGO, NIRC WAJADILI UBORA MIRADI YA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AANIKA UMAHIRI WA TANZANIA INAVYOLINDA UDONGO, MATUMIZI MBOLEA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?