Na ATHANAS KAZIGE
UGONJWA wa figo ni hali ambayo figo zinashindwa kufanya kazi kawaida ya kuchuja damu, kuondoa taka, kudhibiti kiwango cha maji na madini mwilini.
Hali hii inaweza kuanza ghafla (ugonjwa wa ghafla wa figo) au kuendelea na kudumu muda mrefu (ugonjwa sugu wa figo), ambapo figo hupoteza uwezo hatua kwa hatua.
Ugonjwa huu umeendelea kuwa tatizo kubwa katika nchi mbalimbali duniani ikiwemoTanzania.
Kwa kutambua madhara ya ugonja wa figo, serikali imeendelea kutoa fedha nyingi lengo likiwa ni kuboresha huduma kwa wagonjwa.
Miongoni mwa jitihada zinazofanywa na serikali nikuwasomesha wataalamu, kujenga zahanati, vituo vya afya,hospitali, kununua vifaatiba vya vya kisasa ili kupambana na ugonjwa huo.
Hivi sasa wagonjwa wanapata matibabu bora hapa nchini, badala ya kwenda nje ya nchi kupata huduma.
Awali wagonjwa walisafiri kwenda nje ya nchi na kutumia fedha nyingi kupata matibabuhayo, lakini hivi sasa kazi hiyo inafanyika kwa kiwango cha kimataifa hapa nchini.
Gazeti hili lilifanya mahojiano maalumu na daktari bingwa mwandamizi wa magonjwa ya ndani na figo, Dk. Anthony Gyunda, kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, jijini Dar es Salaam.
SWALI:
Figo ni nini?
JIBU:
Figo ni kiungo muhimu sana katika mwili wa binadamu, ni kama kiungo mchezeshajikatika mpira wa miguu ambapo asipocheza vizuri, mechi imepotea.
Hivyo hivyo figokazi yake kubwa katika mwili ni kuuweka katika hali tulivu (balanced) ili viungovingine vyote vifanye kazi sawa sawa.
Kwa mantiki hiyo karibu kila kinachoingiamwilini hupita katika figo ili kuchuja taka mwili, kudhibiti maji mwilini, kusawazishamadini joto mwilini, kutengeneza homoni na kudhibiti shikizo la damu.
Hayo yote yanategemea figo imara na yenye afya bora, ili mwili uwe imara na wenyeafya.
MATATIZO YA FIGO
Dk. Gyunda alisema matatizo ya figo yapo katika aina kuu mbili; tatizo la kutokea ghafla ambalolinaweza kuleta changamoto ya ufanyakazi.
Tatizo hilo linaweza kuchangiakupoteza maji au damu ghafla, kutapika,maambukizi yanayoleta homa kali.
Pia matumizi holela ya dawa kama miti shamba,sumu za mazao huchangia baadhi ya viungo vingine vikiwemo ini, mapafu na moyo kupata tatizo.
Ugonjwa sugu wa figo unasumbua dunia nzima na dalili zake huanza taratibu na katika hatua mbalimbali, ambapo hivi sasa zaidi ya watu milioni 800 dunia wanaugua.
Daktari huyo alisema tatizo hilo linaanza hatua ya kwanza, pili, tatu nne na tano ambayo ni yamwisho, ambapo mgonjwa anakuwa katika hali mbaya.
“Ikifika hatua hiyo figo haiwezi kufanya kazi vizuri kumsaidia mtu aishi bilashida hadi apate msaada wa uchujaji damu kwa kutumia figo bandia(dialysis),”alisema Dk. Gyunda.
Alisema barani Afrika zaidi ya watu milioni 200 wana tatizo lafigo katika hatua mbalimbali, kuanzia ya kwanza hadi ya tanona Watanzania zaidi ya milioni tisa wanaugua ugonjwa wa figo.
Alisema utafiti uliofanyika nchini unaonesha mikoa ya Kaskazini, Arusha na Kilimanjaro ina asilimia saba na idadi kubwa ya wagonjwa wakiishi vijijini.
Kwa upande wa mijini, Dk. Gyunda alisema asiliamia 15 ya Watanzania wanaoishimijini walionekanana tatizo hilo katika hatua mbalimbali. Hii ya mijini inafananana makadirio ya takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO).
SWALI:
Nini chanzo cha tatizo sugu la figo?
JIBU
Baadhi ya vyanzo vikubwani kuwepo magonjwa kamakisukari, ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.
Alisema vyanzo vingine ni unywaji holela wa dawa zikiwemo za kutuliza maumivu nadawa za mitishamba, sigara, dawa za kulevya, unywaji pombe kupindukia, tabiaya ulaji bila kuzingatia mahitaji na kusababisha uzito mkubwa.
“Ni vizuri watu wazingatie sana namba zao (shinikizo la damu, uzito, urefu, mzunguko wa kiuno) mtu anywe na kula kulingana na uzito wake,” alisema.
Dk. Gyunda alisema vijana wapunguze au waache matumizi ya vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks)kwa kuwa ni hatari na havina tofauti na dawa za kulevya.
SWALI:
Nini huduma ya ugonjwa sugu wa figo?
JIBU:
Alisema mgonjwa figo akifika hatua ya tano, anatakiwa apate huduma ya uchujaji wa damu,‘dialysis’.
“Mgonjwa anapokuwa katika hatua ya tano msaada wa kwanzakupata huduma ya uchujaji wa damuili kuondoa taka ndani ya mwili na anatakiwa kuchuja kwa wiki mara tatu na kila awamu inachukua muda usiopungua saa nne.
”Uchujaji huhusisha mgonjwa na mashine ya ‘dialysis’ damu hutolewa kupitia mipira maalumu na kupitakatika mashine ya ‘dialysis’ kabla ya hurudishwa tena kwa mgonjwa,”alisema.
Hata hivyo, daktari huyo alisema uchujaji wa damu siyo tiba ya mwisho katika tatizo sugu la figo, bali kama mgonjwa atakuwa na vigezo na uwezo kupandikizwa figondiyo tiba ya kuokoa maisha yake.
“Kwa huduma ya uchujaji damu serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (Mloganzila naUpanga), hospitali zote za kanda, zaidi ya asilimia 90 za mikoa zinatoa hudumaya uchujaji damu.
“Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imefanya kazikubwa, siku za nyuma mtu aliweza kuhama, mfano kutoka Kigoma kuja Dar esSalaam kupata huduma hii, lakini hivi sasa pale Maweni Hospitali Kigoma Ujiji huduma hiyo ipo,” alisema.
SWALI:
Je Bima ya afya inasaidia kupata huduma hiyo?
JIBU:
Daktari huyo alisema bimainasaidia kwa asilimia kubwa na hivi sasa gharama hizo zimepungua tofauti namiaka iliyopita.
“Hivi sasa huduma hizi kwa mtu mwenye Bima ya Afya inahusika na kila kitu, shidainakuwa kwa mtu asiye na bima, rai yangu kwa wananchi wenzangu wakate Bima ya Afya,”alisema.
“Unajua vipo vifurushikama vya NHIF kama Tanzanite, Mikumi na kilakifurushi kinaweza kulipia vipimo vyote na hata huduma karibu zote ikiwepo ya‘dialysis’,zinatolewa isipokuwa baadhi ya vifurushi mgonjwa atatakiwa kuchangia asilimia fulani sawa na kiasi chake cha mfuko aliochangia.
SWALI
Hapa Mloganzila kuna vifaa na watumishi wa kutoa huduma ya upandikizaji figo?
JIBU:
Serikali imefanya kazi kubwa imejengamiundombinu kwa kuwekeza wazawa, watumishi na wapo madaktari wanaotoahuduma ya upandikizaji wa figo hapa Mloganzila.
“Mloganzila huduma hiyo inatolewa katika viwango vya kimataifa na kazi hiyoimeanza kufanyika tangu Aprili, 2023,”alisema.
Dk. Gyunda alisema wagonjwa 28 wamepatiwa huduma ya upandikizajiwa figo katika Hospitali ya Mlogazila kwa mafanikio makubwa.
“Wiki iliyopita wagonjwa wannetumewaruhusu kutoka hospitali hapa baada yakupandikizwa figo na wamekwenda nyumbani kuendelea kuishi na familia zao wakishiriki ujenzi wa uchumi wa familia na taifa,”alisema.
Alisema hushirikiana na madaktari kutoka Korea Kusini wakitumiateknolojia yakutoa figo kwa tundu dogo, mchangia figo hupatakovu dogo, hutoka hospitalini baada ya siku mbili na mgojwa aliyepandikizwasiku ya saba anaruhusiwa.
Alisema gharama ya kupandikiza figo inakuwa ni takribani sh. milioni 37 ambapo awali watuwalikuwa wanasafiri kwenda nje ya nchi wakitumia zaidi ya sh. milioni 100.
SWALI:
Je wapo watu wenye uwezo mdogo wa kiuchumi wamepandikizwa figo?
JIBU:
Serikali kupitia Wizara ya Afya nataasisi zake, imekuwa na utaratibu mzuri wakuhakikisha Watanzania wanapata huduma hiyo bila ya ubaguzi.
Kuna watu ambao hawana uwezo wamepandikizwa burekwa asilimia 100hapa Mloganzila kupitiamsaada wa Mkono wa Rais Samia. Kuna mtoto kutoka Songea Mjini alishaacha shule akaja tukampandikiza bure kupitiamkono wa Rais, mama yake alimpa figo, sasa amerudi shule,ana afya njema anafanya vizuri darasani.
SWALI:
Hivi figo zinapatikana wapi?
JIBU:
Alisema figo zinapatikana kutokana na kuwepo mtu wa kuchangia figo kwenda kwamgonjwa.
“Ili mtu aweze kupandikizwa figo lazima awepo ndugu yake wa damu na mgonjwaambaye atakubali kutoa figo kumpa ndugu yake.
“Anaweza kuwa baba, mama, mtoto au mwenza wa mgonjwa, tukikosa mtu kati yahao, anaweza kuwa binamu, mjomba na lazima awe ana afya nzuri, lakini mtoaji lazima apimwe sana afya yake”alisema.
SWALI:
Sheria ikoje juu ya utoaji viungo?
JIBU:
Alisema Tanzania hakuna sheria maalumu ya kuchangia viungo hivyo, sisi bado tunaongozwana upendo wa kindugu kati ya mgonjwa na mchangiaji.
“Changamoto inaweza kuwa kama familia ya mgonjwa ina viashiria vya maradhi kama presha, lakini serikali kupitia Wizara ya Afya ipo njiani kukamilisha ili Watanzania wapate huduma,”alisema.
SWALI:
Kuna njiani ngapi za kupata figo au viungo vya mwili wa binadamu?
JIBU:
Daktari huyo alisema zipo njia mbili za kupata kiungo kwa mtu aliyefariki dunia au anayeishi.
Alisema mtu anaweza kupata kiungo hicho kutoka kwa mtu aliyefariki, dunia, lakinilazima kuwe na utaratibu maalumu kujua wakati gani mtu huyo alifariki.
Hata hivyo alisema upo utaratibu wa kupata figo kwa mtu aliyefariki dunia kwamba nani aseme viungo vivunwe, nani atavuna, nani atapewa, je mgonjwa aliacha wosia wa utayari. Hili jambo linahusisha sheria, imani za dini na familia.
“Mtu kama amekufa ubongo wake pia umekufa, lakini viungo vinafanyakazi huyo inawezekana viungo vyake vikavunwa kuchangia mgonjwa wa figo.
Dk. Gyunda alifafanua viungo vinavyoweza kupandikizwa kwa mtu aliyefariki dunia nifigo, moyo, ini, mapafu, utumbo, kongosho na viungo vya macho.
Alidokeza mtu anaweza kupewa sehemu ya ini linaloweza kukatwa sehemu akapandikizwa mgonjwa na baada ya muda litakuwa kama ilivyokuwa awali.
Pia, Dk. Gyunda alisema mgonjwa anaweza kupokea kongosho inayohusika na ugonjwa wa kisukari na mtu akapona.Mtu akiweka wosia huo anapofariki dunia anaweza kuokoa maishaya watu zaidi ya 10.
SWALI:
Kuna dhana kuhusu upandikizaji, zipo hisia mtu anaweza kushindwa kuzaa, je kuna ukweli kiasi gani?
Dk. Gyunda alisema mtu akiwekewa figoanaweza kuendelea na maisha na kufanya shughuli za uzalishaji mali kama kawaida.
“Wapo wanaosema mtu akichangia figo, atapunguza siku zake zakuishi, atapunguza kuzaa au nguvu za kiume zitakwisha, mambo hayo hayanamsingi wowote
“Wakati umefika watu wapewe taarifa sahihi, nawaomba wananchi wapende kupima afya zao, lengo ni kujua hali zao na kama kuna tatizo waanze matibabu mapema,” alisema.
SWALI:
Je unakutana nachangamoto gani katika kazi yako?
JIBU:
Mimi kwa ujumla nasikitika mgonjwa anapokuwa hafuati masharti ya matibabu.
“Baadhi ya wagonjwa wakitibiwa na kupata nafuu, wanarudia tabia zaohatarishi, kama kuvuta sigara na kunywa pombe kitu ambacho walikatazwa,” alisema.
SWALI:
Je kuna hatua gani za kupandikiza ini hapa nchini ?
JIBU:
Mimi si msemaji sana wa eneo hilo, lakini kama daktari, hudumabado hazijaanza kutolewa na mchakato unaendelea vizuri.
“Serikali inaendelea kufanya kazi hiyo kwa umakini mkubwa kupeleka wataalamu kwenda kusoma fani hiyo,”alisema.
SWALI
Je una ushauri gani kwa serikali?
JIBU:
Aliiomba serikali kupitia Wizara ya Afya kuongeza wigo kwa watu wanaochangia figo kwa wagonjwa kwa kuzingatia sheria
Alisema serikali kupitia Wizara ya Afya kuwa wamekuwa wakipandikiza figo tangu mwaka 2017 ambapo mgonjwawa kwanza alipandikizwa Hospitaliya Taifa ya Muhimbili.
Pia mwaka 2018 alipandikizwa figo mgonjwa wa kwanza Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.Wagonjwa zaidi ya 100 walipandikizwa figo nchini.
“Pale hospitali ya Benjamin Mkapa,mimi na wenzangu tuliweka msingi bora wahuduma za figo na hadi sasa zinaendelea kwa kiwango cha juu sana,” alisema Dk.Gyunda.
SWALI:
Umepata mafunzo wapi?
JIBU:
“Nimesoma fani ya afya hapa nchini, baadaye nilikwenda China na India kubobea zaidi katika huduma za figo na upandikizaji wake.
“India nilisoma zaidi jinsi ya kupandikiza figo kwa kiwango cha juu sana nilibahatika kuwa katika taasisi inayofanya upandikizaji wa ainazote, rahisi na mgumu zaidi ya 200 kwa mwaka mmoja
“Nilisoma vitu vingine vikiwemo kama vinasaba vikiwa tofauti, kama wewe upoDar na mwingineMbeya, kuna mtu anakwenda sawa na vinasaba vya ndugu wa Dar esSalaam, mnabadilishana na mwenye ndugu ambaye ana matatizoanayeishi Mbeya.Hapo mtu atapewa figo kama wanafanya vinasaba vyao, inaitwa DonorSwap,”alisema.




