• ePaper
Sunday, August 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MWIGULU ASISITIZA UHURU WA KUABUDU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 15, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MWIGULU ASISITIZA UHURU WA KUABUDU
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu na kuimarisha ushirikiano na taasisi za dini kwa kutambua mchango mkubwa unaotolewa na taasisi hizo katika kujenga maadili, amani, mshikamano na maendeleo ya taifa.

Dk. Mwigulu alisema hayo Mjini Kiomboi, wilayani Iramba, mkoani Singida, aliposhiriki ibada katika Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Kiomboi Christian Centre.

Ibada hiyo iliongozwa na Askofu wa Jimbo la Singida Kaskazini, Dk. Danford Obadia na Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Yona Essya.

Akizungumza na waumini hao, Waziri Mkuu, alisema serikali inatambua nafasi muhimu ya taasisi za dini katika malezi ya jamii na itaendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowezesha taasisi hizo kutekeleza majukumu yake kwa uhuru na ufanisi.

“Sisi wote tutaendelea kulinda mazingira bora ya kuendesha ibada. Serikali itaendelea kutambua na kuamini kazi inayofanywa na taasisi za dini katika kujenga taifa letu,” alisema.

Alisema taasisi za dini zimekuwa mshirika muhimu wa serikali katika kujenga maadili mema, kuhimiza uwajibikaji, kuimarisha mshikamano wa kijamii na kupambana na vitendo vinavyokinzana na utu na maendeleo ya wananchi.

Waziri Mkuu alisema Kanisa la TAG, limekuwa na mchango mkubwa katika kuelimisha jamii, kuondoa imani potofu na kuhamasisha wananchi kuzingatia maadili na misingi sahihi ya maisha.

“TAG haikusimama katika ibada pekee, bali imebadilisha hata maisha ya kila siku ya wananchi. Imechangia kuondoa baadhi ya mila na imani zilizokuwa zinarudisha nyuma maendeleo ya watu wetu,” alisema.

Wakati huohuo, Dk. Mwigulu alitoa rai kwa wananchi kuendelea kuheshimu nyumba za ibada na kuepuka kuziingiza katika shughuli

zinazoweza kuvuruga dhamira na malengo yake ya msingi.

“Ukitaka siasa anzisha chama cha siasa. Usipeleke fujo katika nyumba ya ibada. Lazima tuendelee kuheshimu utakatifu wa nyumba zetu za ibada,”alisema.

Previous Post

RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

Next Post

WASOMI, WANASIASA WAKOSHWA TOZO KUCHANGIA BIMA YA AFYA

Next Post
WASOMI, WANASIASA WAKOSHWA TOZO KUCHANGIA BIMA YA AFYA

WASOMI, WANASIASA WAKOSHWA TOZO KUCHANGIA BIMA YA AFYA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CCM YAELEZA KUONGEZEKA MBOLEA YA RUZUKU

CCM YAELEZA KUONGEZEKA MBOLEA YA RUZUKU

11 months ago
FOLZ  AKILI YOTE KWA WAMALAWI

FOLZ  AKILI YOTE KWA WAMALAWI

10 months ago

Popular News

  • KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    KIINI DABI KARIAKOO KUPIGWA ZANZIBAR

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TAMU, CHUNGU DABI YA K’KOO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TEC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AWAPA RAHA VIGOGO USHIRIKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BILIONI 30/- KUJENGA UWANJA WA KISASA SIMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?