• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
June 13, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ATHNATH MKIRAMWENI

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amezibana taasisi za fedha nchini kwa kuzitaka kuhakikisha mikopo inapatikana kwa wananchi na masharti yanayoendana na hali halisi ya wafanyabiashara wadogo.

Pia, amesisitiza kuwa, malalamiko ya wananchi kuhusu gharama kubwa za mikopo yanapaswa kusikilizwa na kufanyiwa kazi.

MAAGIZO YA RAIS

Akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam, Rais Dk. Samia alisema tathmini ya gharama za mikopo haipaswi kuishia katika viwango vya riba pekee, bali izingatie gharama nyingine zinazomkabili mkopaji zikiwemo za bima, masharti ya dhamana na muda unaotumika kupata mkopo. 

Rais Samia alisema wananchi wengi wanaolalamikia mikopo hawazungumzii riba pekee; bali mzigo mzima wa masharti yanayoambatana na huduma hiyo, jambo linalowafanya wengi kushindwa kufikia huduma rasmi za kifedha.

Hivyo, aliitaka BoT na taasisi za fedha kuimarisha uwazi kwa kuwapa wananchi taarifa sahihi, rahisi na kueleweka kuhusu gharama zote za mikopo kabla ya kufanya uamuzi wa kukopa.

Pia, alizitaka taasisi za fedha kuongeza ushindani katika utoaji wa mikopo na kuacha kutegemea aina zilezile za dhamana, ambazo wananchi wengi hususan wanawake na vijana, hawana uwezo wa kuziwasilisha.

Alisema ipo haja ya kutambua kuwa, watu wengi wana historia nzuri ya biashara, mauzo na miamala ya kifedha ambayo inaweza kutumika kuthibitisha uwezo wao wa kurejesha mikopo badala ya kutegemea umiliki wa nyumba, viwanja au magari pekee.

“Uaminifu ni mali kubwa kuliko hata mali inayoonekana, hivyo taasisi za fedha mbuni mifumo mipya itakayowezesha wananchi wengi kupata mikopo rasmi,”alisema.

Alitoa mfano wa mamalishe, anayefanya biashara kwa miaka mingi kwa mafanikio na hana hati ya nyumba, mtu wa aina hiyo, anapaswa kuwa na njia rahisi ya kuthibitisha ustahili wake wa kupata mkopo.

 Pia, alisema hatua hiyo, itafungua milango kwa mamilioni ya Watanzania waliopo nje ya mfumo rasmi wa mikopo licha ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na biashara.

 MFUMO WA FEDHA 

Kuhusu mfumo wa fedha, Rais Dk. Samia alisema maendeleo ya mfumo huo yanapaswa kwenda pamoja na ustawi wa mwananchi; badala ya kutegemea takwimu za ukuaji wa uchumi pekee. 

Alisema kipimo cha mafanikio hakipaswi kuwa, idadi ya watu waliounganishwa katika huduma za kifedha, bali ni kuona kama huduma hizo zimeongeza mitaji, kupanua biashara na kuinua vipato vya wananchi.

Rais Samia alisisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika safari ya maendeleo ya uchumi, kwani upatikanaji wa mitaji kwa wakati na kwa gharama nafuu ndio msingi wa kuongezeka kwa uwekezaji, ajira na uzalishaji. 

Dk. Samia alisema takwimu zinaonyesha mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka kutoka asilimia 6.6 ya Pato la Taifa mwaka 1994, hadi takriban asilimia 16 mwaka 2025, ingawa kiwango hicho, bado ni kidogo kikilinganishwa na malengo ya taifa. 

Alibainisha, Tanzania inalenga kujenga uchumi wa dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050, jambo linalohitaji mfumo wa fedha unaokusanya akiba na kuelekeza mitaji katika shughuli za uzalishaji.

MZIGO KWA WALIPA KODI

Rais Dk. Samia aliagiza matumizi ya mifumo ya malipo ya kidijitali yaendelezwe kupanua wigo wa kodi, uwazi na kupunguza matumizi ya fedha taslimu.

Alionya kuwa, mifumo hiyo isitumike kuongeza mzigo kwa walipakodi waliopo tayari katika mfumo rasmi, bali itumike kuvutia wananchi wengi zaidi kuingia katika mfumo wa ulipaji kodi.

Kwa mujibu wa Rais, bado kuna kundi kubwa la wananchi wanaofanya shughuli za kiuchumi katika sekta isiyorasmi ambao mchango wao haujaonekana kikamilifu katika mapato ya taifa.

AIPONGEZA BOT

Vilevile, Rais Dk. Samia aliipongeza BoT kwa mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 60, tangu kuanzishwa kwake, ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei na kuimarisha uthabiti wa mfumo wa fedha.

Pia, aliipongeza kwa mpango wa ununuzi wa dhahabu ya ndani na kuwa, hadi Mei, mwaka huu, ilikuwa imekusanya tani 27.5 zenye thamani ya takribani sh. trilioni 10 na kuimarisha akiba ya taifa.

Alitaja matarajio yake ni kuona BoT ikiendelea kuwa zaidi ya msimamizi wa fedha na kuwa, taasisi yenye uwezo wa kubaini mapema hatari na fursa za kiuchumi, kulinda ustawi wa taifa na wananchi wake katika miaka 60 ijayo.

WAZIRI WA FEDHA

Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, aliitaka BoT kujipanga upya, kuendana na mahitaji ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kufanikisha mageuzi ya kiuchumi yanayolengwa na nchi. 

Balozi Omar alisema Dira 2050 imeweka malengo makubwa ya maendeleo, ambayo hayawezi kufikiwa kwa kuendelea na mifumo ya zamani ya utendaji, hivyo taasisi muhimu za kiuchumi zinapaswa kubadilika na kuendana na mwelekeo mpya wa maendeleo.

Aliongeza kuwa, BoT ina jukumu kubwa katika kuhakikisha sera za fedha, usimamizi wa sekta ya fedha na maendeleo ya mfumo wa kifedha vinachangia kukuza uchumi wa kisasa na shindani, hivyo ukuaji wa uchumi unahitaji benki kuu yenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi na teknolojia yanayoendelea duniani.

GAVANA TUTUBA

Kwa upande, Gavana wa BoT, Emmanuel Tutuba, alisema benki hiyo itaendelea kusimamia sera ya fedha, kuimarisha sekta ya fedha na mifumo ya malipo; kuchangia kikamilifu utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na maendeleo ya uchumi wa nchi kwa ujumla.

Gavana Tutuba alisema mageuzi ya sekta ya fedha kwa miaka 60, yameiwezesha Tanzania kufikia viwango vya benki kuu bora duniani katika usimamizi wa sera za fedha na uthabiti wa mfumo wa kifedha.

Alisema katika miaka mitatu iliyopita, wastani wa mfumuko wa bei umebakia asilimia 3.5, ndani ya lengo la asilimia tatu hadi na uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa asilimia 6.2.

Pia, alisema sekta ya benki imepanuka  kutoka benki tatu hadi 42, mikopo kwa sekta binafsi imeongezeka kutoka asilimia 6.6 ya Pato la Taifa mwaka1994 hadi asilimia 16 mwaka 2025, hali inayoonyesha kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za kifedha.

Gavana Tutuba alisema ubora wa mali za benki, umeendelea kuimarika huku kiwango cha mikopo chechefu kikishuka hadi asilimia 2.9 Februari, mwaka huu, kiwango ambacho kiko chini ya ukomo wa kimataifa wa asilimia tano.

Vilevile, huduma za kibenki za kidijitali, mawakala wa benki na mifumo ya malipo ya kielektroniki zimeongeza ufanisi na kupunguza gharama za miamala kwa wananchi na taasisi.

Katika upande wa sekta ya nje, Gavana Tutuba alisema Tanzania, imeendelea kuwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni inayoweza kugharamia uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa miezi 4.8, kiwango kinachozidi sharti la kisheria la miezi minne.

Alisema hali hiyo, imechangiwa na hatua mbalimbali za BoT za kuimarisha usimamizi wa akiba za fedha za kigeni.

“Mpango wa ununuzi wa dhahabu ulioanzishwa umeongeza nguvu katika akiba ya taifa na hadi kufikia Juni 10, mwaka huu, BoT ilikusanya tani 27.5 za dhahabu zenye thamani ya takribani sh. trilioni 10, hatua iliyoimarisha uthabiti wa sekta ya fedha na kuongeza uwezo wa nchi kukabiliana na misukosuko ya kiuchumi,” alisema.

Alisema BoT imeanza kujiandaa na mageuzi ya teknolojia kwa kuanzisha kitengo cha Akili Unde na kusaini mikataba ya ushirikiano na vyuo vikuu sita nchini, kwa matumizi ya teknolojia hiyo katika uchambuzi wa takwimu, kufanya uamuzi na kuimarisha usalama wa mifumo ya malipo dhidi ya mashambulizi ya mtandao.

Tutuba aliongeza kuwa, BoT itaendelea kudhibiti mfumuko wa bei, kusimamia sekta ya fedha, kuimarisha thamani ya shilingi ya Tanzania, kukuza huduma jumuishi za kifedha na kuhimiza ubunifu wenye uwajibikaji kuhakikisha mfumo wa fedha unabaki imara na kuchochea maendeleo endelevu ya uchumi.

Previous Post

AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

Rais Samia atoa maelezo kuhusu maendeleo ya uchumi

10 months ago
TANZANIA MFANO BORA SEKTA YA MAJI DUNIANI

TANZANIA MFANO BORA SEKTA YA MAJI DUNIANI

3 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?