• ePaper
Thursday, July 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SERIKALI KUANGALIA FURSA ZA MIKOPO KWA WANAOSOMA KOZI FUPI – WAZIRI MKUU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 30, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SERIKALI KUANGALIA FURSA ZA MIKOPO KWA WANAOSOMA KOZI FUPI – WAZIRI MKUU
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU


WAZIRI MKUU Dk. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imepokea ombi la Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) la kutoa fursa ya mikopo kwa vijana wanaosoma kozi za muda mfupi kwenye chuo hicho.

“Mkuu wa Chuo ulieleza uwepo wa hii changamoto ukisisitiza kwamba ukosefu wa mikopo unafanya idadi ya wanafunzi ipungue kwani watoto wa matajiri ndiyo wanaweza kusoma kwa kuwa wanamudu ada hizo,” amesema.

“Kozi hii inahitaji utimamu wa akili bila kujali mwanafunzi anatoka kwenye familia ipi. Mheshimiwa Rais wetu amejitambulisha kwa kutoa Samia Scholarship kwa wanafunzi wanaofanya vizuri na kupata ufaulu wa juu. Kigezo siyo mwanafunzi ametoka kwenye familia ipi bali ufaulu wake wa kidato cha sita kwa kupata alama tatu za A,” amesema Waziri Mkuu.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Julai 30, 2026) akizungumza na washiriki wa Kongamano la Chama cha Wataalamu wa Lojistiki na Usafirishaji Tanzania la Mwaka 2026 lililofanyika kwenye Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mabibo, jijini Dar es Salaam.

Ametumia fursa hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji wa sh. bilioni 70 kwenye chuo hicho. “Kupitia uwekezaji huo, nimejionea uwekezaji mkubwa unaofanyika kwenye miundombinu ya mabweni na ya kujifunzia,” amesisitiza.

Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki wa kongamano hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile alisema kuwa sekta ya uchukuzi ni kiungo muhimu katika ukuaji wa uchumi ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita sekta hiyo imechangia katika pato la Taifa kwa takribani dola za Marekani bilioni 2.8.

Naye, Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Prosper Mgaya alisema chuo hicho ni cha pili barani Afrika kikifuatia Ethiopian Aviation Academy lakini pia ni cha kwanza katika nchi za Afrika Mashariki. Alisema kimejipanga kutoa mafunzo ambayo yatatoa fursa za ajira kwa Watanzania hadi nje ya nchi.

“Kupitia mafunzo haya, tumetoa mafundi wa aircraft maintanance ambao wamepata ajira ATCL na Air Dubai. Kupitia mafunzo ya vitendo, tumesajili wanafunzi wa urubani 22. Lakini pia tayari marubani wanne wamehitimu na wanane wanaruka solo (bila uangalizi na hivyo wako tayari kuingia sokoni).”

Previous Post

ALIYEOA MWANAFUNZI KWA MAHARI MILIONI 4/- ADAKWA

Next Post

PPAA YAHIMIZA WAZABUNI KUTUMIA MODULI YA MALALAMIKO NA RUFAA KATIKA MFUMO WA NeST

Next Post
PPAA YAHIMIZA WAZABUNI KUTUMIA MODULI YA MALALAMIKO NA RUFAA KATIKA MFUMO WA NeST

PPAA YAHIMIZA WAZABUNI KUTUMIA MODULI YA MALALAMIKO NA RUFAA KATIKA MFUMO WA NeST

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA ATUMA UJUMBE WA AMANI

RAIS DK. SAMIA ATUMA UJUMBE WA AMANI

7 months ago
DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

DK. MWIGULU AWAVAA WANAOSUBIRI UTEUZI

5 months ago

Popular News

  • SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

    SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PPAA YAHIMIZA WAZABUNI KUTUMIA MODULI YA MALALAMIKO NA RUFAA KATIKA MFUMO WA NeST

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUANGALIA FURSA ZA MIKOPO KWA WANAOSOMA KOZI FUPI – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALIYEOA MWANAFUNZI KWA MAHARI MILIONI 4/- ADAKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AGGREY MWANRI NAIBU KATIBU MKUU CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?