• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WASIRA : MAENDELEO YALIYOPO, UTHIBITISHO WA UONGOZI MAHIRI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 15, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
WASIRA : MAENDELEO YALIYOPO, UTHIBITISHO WA UONGOZI MAHIRI

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira

0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ESTA MALIBICHE, 

Iringa 

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amesema maendeleo makubwa yaliyopo nchini ni uthibitisho wa uongozi mahiri uliofanywa na serikali chini uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Wasira aliyasema hayo mjini Iringa, wakati akizindua kampeni Jimbo la Iringa Mjini, iliyoambatana na kumnadi Mgombea wa Ubunge Jimbo la Iringa Mjini, kupitia CCM, Fadhir Ngahilo.

Akitaja baadhi ya Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2025, katika Jimbo la Iringa Mjini, Wasira alisema kwa miaka mitano, CCM imefanikiwa kujenga shule mpya nne na madarasa 114 bila wananchi kuchangia chochote.

Alisema hatua hiyo, imechangia kwa kiasi kikubwa, kuongezeka ufaulu kutokana na wanafunzi kujifunza katika mazingira rafiki.

Pia, alieleza katika kipindi cha mitano, shule nne mpya za sekondari zilijengwa, zikiwa na vyumba vya madarasa 134.

Alisema serikali ya CCM, imetekeleza ilani yake kwa kiwango kikubwa katika sekta ya afya, zahanati tatu zimejengwa, vituo vya afya vitatu na kuboresha hospitali, lengo likiwa kupunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata matibabu.

Alitaja mradi mwingine ya kisekta uliotekelezwa kipindi cha miaka mitano, ni maji ambayo hivi yanapatikana kwa uhakika.

Alisema matarajio ya CCM kupitia Ilani yake ya 2025-2030, imeweka mpango kabambe wa kujenga shule mpya za msingi na sekondari 22, zahanati saba.

JIMBONI KALENGA

Akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Kalenga wilayani Iringa, Wasira alisema CCM kupitia Ilani yake ya mwaka 2025-2030, imeainishwa kulenga kuwakomboa mwananchi na kumwinua kiuchumi  kwa kuweka mazingira rafiki na wezeshi katika sekta mbalimbali.

Katika mkutano huo, uliofanyika Kijiji cha Nzihi, Wasira alisema idadi kubwa ya Watanzania, pato lao linategemea kilimo, serikali itaanzisha vituo vya zana za kilimo.

Alitolea mfano maeneo mengine ambayo  ardhi yake ni kame likiwemo Jimbo la Isimani, Wasira alisema kuwa, Ilani ya mwaka 2025-2030, itaendelea kuweka nguvu  zaidi katika kilimo cha umwagiliaji ili wakulima waweze kulima mara mbili kwa mwaka.

Wakati akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Jackson Kiswaga, Wasira aliwapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo hilo, kumpitisha katika kura za maoni.

Previous Post

DK. MWINYI ATANGAZA NEEMA WAZEE ZANZIBAR

Next Post

MRATIBU ACT ATOBOA SIRI KUJIUNGA CCM

Next Post
MRATIBU ACT ATOBOA SIRI KUJIUNGA CCM

MRATIBU ACT ATOBOA SIRI KUJIUNGA CCM

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

CCM YAONESHA KUKUBALIKA, MAELFU WAMIMINIKA

7 months ago
MAYWEATHER, PACQUIAO, KUZICHAPA TENA SEPTEMBA

MAYWEATHER, PACQUIAO, KUZICHAPA TENA SEPTEMBA

2 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?