• ePaper
Thursday, July 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

AGGREY MWANRI NAIBU KATIBU MKUU CCM

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
July 30, 2026
in Habari, Kitaifa
0
AGGREY MWANRI NAIBU KATIBU MKUU CCM
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Emmanuel Mohamed

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimefanya mabadiliko ya sekretarieti ngazi taifa, kwa kumteua Aggrey Mwanri kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, akichukua nafasi ya John Mongella, huku Abdi Mohamed Abdi akiwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, akimrithi Dk. Mohammed Said Mohammed ‘Dimwa’.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa mikutano Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Unguja,  Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Kenani Kihongosi,  alisema katika mabadiliko hayo, Paul Chacha amekuwa Katibu wa NEC Oganaizesheni akimrithi Issa Haji Ussi ‘Gavu,’ na Jamal Kassim amekuwa Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, akichukua nafasi ya Joshua Mirumbe.

Katika nafasi moja ya Mjumbe wa Kamati Kuu, Rahma Kassim Ali ameteuliwa kujaza nafasi ya  Leila Ngozi, ambaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’.

PONGEZI KWA MARAIS SAMIA, MWINYI

Katika hatua nyingine,  Kihongosi alisema CCM imempongeza Mwenyekiti wake, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi imara, madhubuti, unaojali maendeleo ya Watanzania na kusisitiza: “Chama kinajionea kasi ya maendeleo ndani ya Jamhuri ya Tanzania.

“Kazi inafanyika kwa weledi, sekta zote zikiwemo afya, miundombinu ya barabara, sekta ya maji, elimu na nishati, hivyo CCM inampongeza mwenyekiti kwa kuonyesha uongozi imara ambao una matokeo chanya.”

Alifafanua, “CCM inampongeza Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akiifanya Zanzibar, leo tumeona mabadiliko makubwa, barabara zinajengwa kwa kasi, Chama kinazipongeza serikali zake zote mbili,” alisema.

Alisema serikali zinafanya vizuri katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025-2030, kwa kuhakikisha mambo yaliyoahidiwa yanatekelezwa.

UCHAGUZI WA KIDEMOKRASIA

Kihongosi alisema katika kikao cha Halmashauri Kuu, wajumbe walijadili maandalizi ya uchaguzi mkuu wa CCM na jumuiya zake, ambao unatarajiwa kufanyika mwakani, baada ya kikao hicho kupitisha ratiba na miongozo ya uchaguzi huo.

“Tunataka uchaguzi wa kidemokrasia, uchaguzi huru na wa heshima kama ambavyo CCM imekuwa ikijitanabaisha kuwa na uwezo mkubwa wa kusimamia uchaguzi wake wa ndani, katika hali ya utulivu na amani, ”alifafanua.

REKODI

Mwanri aliwahi kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi wa CCM, nafasi ambayo aliteuliwa mwaka 2006, wakati sekretarieti mpya ya CCM ilipoundwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Chama wakati huo, Rais mstaafu Jakaya Kikwete. Pia aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Chacha, hadi uteuzi wake unafanyika jana, alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abdi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Zanzibar huku Jamal akiwahi kushika nafasi ya Waziri wa Fedha Zanzibar.

Previous Post

MVUTANO MAZISHI YA WAMBURA WAFIKA KORTINI, DALILI ZA MARIDHIANO ZACHOMOZA

Next Post

ALIYEOA MWANAFUNZI KWA MAHARI MILIONI 4/- ADAKWA

Next Post
ALIYEOA MWANAFUNZI KWA MAHARI MILIONI 4/- ADAKWA

ALIYEOA MWANAFUNZI KWA MAHARI MILIONI 4/- ADAKWA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TUME YA JAJI CHANDE KUIMARISHA DEMOKRASIA

TUME YA JAJI CHANDE KUIMARISHA DEMOKRASIA

5 months ago
CCM NDIYO BABA WA DEMOKRASIA – KIHONGOSI

CCM NDIYO BABA WA DEMOKRASIA – KIHONGOSI

5 months ago

Popular News

  • SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

    SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • PPAA YAHIMIZA WAZABUNI KUTUMIA MODULI YA MALALAMIKO NA RUFAA KATIKA MFUMO WA NeST

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUANGALIA FURSA ZA MIKOPO KWA WANAOSOMA KOZI FUPI – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALIYEOA MWANAFUNZI KWA MAHARI MILIONI 4/- ADAKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AGGREY MWANRI NAIBU KATIBU MKUU CCM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?