• ePaper
Wednesday, September 23, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA, SIMBA, WADAU WAMLILIA FATMA KARUME

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 23, 2026
in Burudani, Habari, Kitaifa, Michezo
0
YANGA, SIMBA, WADAU WAMLILIA FATMA KARUME
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na VICTOR MKUMBO

UONGOZI wa Klabu za Yanga, Simba na wadau wa soka nchini wamesikitishwa na taarifa za msiba wa Mama Fatma Karume, mjane wa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati, Sheikh Abeid Aman Karume.

Msiba wa Mama Fatma Karume, ulitokea juzi na kuzikwa jana visiwani Zanzibar ambapo ulihudhuriwa na watu mbalimbali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo.

Alisema uongozi, umepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga, Fatma Karume.

“Tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Mama Fatma Karume ambaye alikuwa mmoja wa Wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa Yanga.

“Huu ni msiba mkubwa kwetu, tumepoteza kiongozi mkubwa mwenye busara, hekima na mapenzi na klabu yetu, tutamkumbuka kwa mengi mazuri aliyoyafanya kipindi cha uhai wake.

“Tutamkumbuka kwa mengi aliyoyafanya ikiwemo upatikanaji wa ardhi ya jengo la Makao Makuu, Jangwani, Dar es Salaam, hakika tumepoteza mwanachama na moja ya nembo ya klabu hii,” alisema.

Hersi aliongeza kuwa uongozi unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, na wadau wa michezo nchini.

“Tunawaombea familia yote, Mungu awape nguvu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu,” alisema.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alisema wamepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

Alisema Simba inaungana na Watanzania wote katika kipindi hiki cha maombolezo ya kuondokewa na mpendwa wao ambaye alikuwa mmoja wa wadau wakubwa wa michezo nchini.

“Tuumepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa kwani tunamjua Mama Fatma Karume alikuwa mmoja wa wadau wakubwa wa michezo hasa soka, tunaungana na Watanzania wote katika kipindi hiki cha maombolezo,” alisema Ahmed.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Klabu ya Yanga, Mohamed Msumi alisema marehemu Mama Fatma Karume enzi za uhai wake alikuwa mwanachama wa klabu hiyo kwa miaka mingi.

Alisema kuwa mume wake alifariki mwaka 1972, lakini yeye aliendelea kuwa bega kwa bega na Yanga ikiwemo kuanzisha bonanza la Pasaka ambapo wachezaji walikuwa wakitembeleana na kucheza mechi Zanzibar na Tanzania Bara.

“Alikuwa kiungo kikubwa cha kuwapokea walitokea Bara na kwenda Zanzibar kushiriki bonanza la michezo,”alisema.

Msumi alisisitiza kwamba hadi alipokuwa akifariki, alikuwa bado yupo ndani ya Yanga na alishawahi kuisaidia kwa mambo mbalimbali.

Alisema Wanayanga wanatakiwa kuwa wakweli na kujifunza mengi kutoka kwa Mama Fatma Karume, kuondoa dosari zao kwani nguzo aliyokuwa akiikimbia mara nyingi.

“Tumesikitishwa na msiba huu, ninatoa wito kwa Wanayanga kushikamana na kuwa wamoja wa kweli ikiwemo kutimiza kauli yetu ya Daima Mbele Nyuma Mwiko, kwani tuliyekuwa tukimtegemea ameondoka tuendelee kumwombea kwa Mungu,” alisema Msumi.

Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula ‘Mzazi’ alisema kuwa amesikitishwa na taarifa za msiba wa Mama Fatma Karume.

Alisema kipindi akiwa kocha wa Yanga aliwahi kupata mwaliko mwaka 2005 ikiwemo kwenda kwake.

“Ukweli alikuwa na mapenzi makubwa na timu hiyo katika kipindi chote cha uhai wake,”alisema.

Alifafanua kuwa Yanga ilipogawanyika makundi, Mama Fatma Karume alikuwa akihusika kwa kiasi kikubwa kuwaleta katika mstari japokuwa kuna muda alipitia matokeo yasiyoridhisha.

Aliongeza kuwa Mama Fatma Karume  alishawahi kusisitiza Simba na Yanga siyo sehemu ya uhasama na kwamba timu zinatakiwa kuendelea kushikamana katika nyakati zote.

“Nilimfahamu Mama Fatma Karume kipindi kile mimi ni kocha wa Yanga na alishawahi kutualika kwake, ninamkumbuka kwa mambo mengi alitusaidia katika vipindi vya mpito ikiwemo kutusisitiza kwamba Simba na Yanga siyo sehemu ya uhasama, tutamkumbuka kwa mengi mazuri aliyowahi kutupatia kipindi cha uhai wake,” alisema.

Mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ alisema kuwa amesikitishwa na taarifa hizo kwani Mama Fatma Karume alikuwa mmoja wa viongozi waliowaunganisha wachezaji wote.

Alisema ni msiba mkubwa kwani Mama Fatma Karume alishaisaidia timu ikiwa katika kipindi kigumu ikiwemo kuwatembelea kambini na kuwapatia hata posho.

Alisema mara kwa mara alikuwa na Yanga bega kwa bega kuhakikisha inafanya vizuri, kitu ambacho kiliwaongezea morali walipokuwa uwanjani.

“Mama Fatma Karume alishanishauri mambo mengi, pia alikuwa mtu wa karibu na timu hata tukipitia kipindi kigumu, alitutuliza ikiwemo kututembelea kambini, tumeondokewa na mtu muhimu,” alisema.

Previous Post

NGORONGORO HEROES YAFUZU AFCON

Next Post

NYOTA TAIFA STARS MZUKA UMEPANDA

Next Post
NYOTA TAIFA STARS MZUKA UMEPANDA

NYOTA TAIFA STARS MZUKA UMEPANDA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

YANGA, SIMBA KAZI KAZI UBINGWA LIGI KUU

YANGA, SIMBA KAZI KAZI UBINGWA LIGI KUU

3 months ago
‘TUMUOMBEE KARDINALI PENGO’

‘TUMUOMBEE KARDINALI PENGO’

9 months ago

Popular News

  • TANZANIA YATOA WITO WA KUIMARISHWA UMOJA WA MATAIFA

    TANZANIA YATOA WITO WA KUIMARISHWA UMOJA WA MATAIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYOTA TAIFA STARS MZUKA UMEPANDA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA, WADAU WAMLILIA FATMA KARUME

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NGORONGORO HEROES YAFUZU AFCON

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA MAMBO MOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?