• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MASHILI ATIMIZA AHADI, AKABIDHI MSAADA WA KICHOMEA TAKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 29, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MASHILI ATIMIZA AHADI, AKABIDHI MSAADA WA KICHOMEA TAKA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MKURUGENZI Mtendaji wa Mashili Company Limited, Peter Mashili, ametekeleza ahadi aliyoitoa Agosti 7, 2026 wakati alipokuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Nne ya Chuo cha Uuguzi na Ukunga Nzega, kwa kukabidhi kichomea taka (incinerator) alichokijenga kwa gharama ya shilingi Milioni 6.9 pamoja na jenereta ambalo amelinunua shilingi milioni 4.2, kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na utoaji wa mafunzo chuoni hapo.

Akikabidhi mchango huo leo Septemba 29, 2026 kwa Mkuu wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Nzega, Bw. Josephat K. Kaja, Mashili amesema utekelezaji wa ahadi hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuimarisha elimu na mafunzo ya wataalamu wa afya, sambamba na kuboresha mazingira ya wanafunzi na wakufunzi.

Mashili amesema vifaa hivyo vyote vilivyogharimu shilingi milioni 11.186 ili ni maalumu kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za umeme na kuboresha mazingira ya chuo.

Amesema kichomea taka kitasaidia kuboresha usimamizi wa taka zinazozalishwa katika mazingira ya chuo, hususani taka zinazohusiana na mafunzo na huduma za afya, wakati jenereta litasaidia kuhakikisha shughuli za mafunzo zinaendelea hata pale kunapokuwa na changamoto ya upatikanaji wa umeme.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Nzega, Zalna Dickolagwa, amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Mashili Company Limited, Peter Mashili kupitia kampuni yake inayojihusisha na uchimbaji wa madini kwa kuendelea kufanya shughuli za uwekezaji huku akitambua umuhimu wa kurudisha sehemu ya mafanikio kwa jamii kupitia Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Amesema utekelezaji wa ahadi hiyo umeongeza uaminifu kwa wananchi, kwa kuwa Mashili ameonesha kwa vitendo kwamba ahadi anazotoa anazitekeleza.

Amesema Serikali wilayani Nzega itaendelea kushirikiana na Mashili Company pamoja na sekta binafsi kwa ujumla, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kuchochea utekelezaji wa shughuli za maendeleo zitakazonufaisha jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Nzega, Josephat K. Kaja, amemshukuru Mashili kwa kutekeleza ahadi hiyo, akisema msaada huo utasaidia kukabiliana na changamoto zilizokuwa zikiathiri mazingira ya kujifunzia na uendeshaji wa shughuli za chuo.

Mchango huo unakuja ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Serikali za kuongeza idadi ya wataalamu wa afya nchini kupitia vyuo vya mafunzo, wakati Chuo cha Uuguzi na Ukunga Nzega kikiwa na wanafunzi 143, wakiwemo wasichana 93 na wavulana 50.

Previous Post

MSUKUMA AJITEKA,  ATAKA MILIONI 5 KUTOKA KWA NDUGU

Next Post

KATAMBI AOKOA JAHAZI MGOMO MADEREVA NCHINI

Next Post
KATAMBI AOKOA JAHAZI MGOMO MADEREVA NCHINI

KATAMBI AOKOA JAHAZI MGOMO MADEREVA NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

MABASI YA UMEME REKODI ZANZIBAR

3 months ago
DK. SAMIA KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA KAMPENI ZA CCM GOMBANI YA KALE

DK. SAMIA KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA KAMPENI ZA CCM GOMBANI YA KALE

1 year ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?