• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

KATAMBI AOKOA JAHAZI MGOMO MADEREVA NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 29, 2026
in Habari, Kitaifa
0
KATAMBI AOKOA JAHAZI MGOMO MADEREVA NCHINI
0
SHARES
22
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WAANDISHI WETU DAR, MIKOANI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ameagiza kusikitishwa mara moja mfumo wa pointi, huku akiwasihi madereva kuwa wavumilivu na kuendelea kuiamini serikali.

Akizungumza na madereva katika mkutano uliofanyika Stendi Kuu ya Mabasi, Magufuli jijini Dar es Salaam, Katambi alisema Septemba 19, mwaka huu, alielekeza vyombo vya dola, visimkamate dereva yeyote katika masuala ya pointi.

Alisema suala hilo la pointi, alishatoa ufafanuzi, tayari vyombo vya dola na usalama vinatambua maelelezo aliyotoa.

“Kama kuna mtu aliyekatwa pointi, nileteeni majina haraka sana ofisini kwangu,  hilo jambo lishughulikiwe, hakuna dereva hata mmoja ambaye alikatwa pointi.

“Leo mniambie kama kuna dereva yeyote amefanyiwa hivyo, maana yake ameonewa, nitataka kujua ambaye amefanya jambo hilo na hatua tutazichukua, jambo la pointi lisitishwe mara moja,”alisema.

Aidha, alisema malalamiko ya madereva ameyachukua, huku akiweka wazi kuwa, suala la pointi halijaanza na wala halitekelezwi, isipokuwa ni vyema kufanya tathmini masuala ya elimu na uelimishaji.

Pia, alisisitiza mawazo ya wadau yanapaswa kuzingatiwa kwa kina na kuangalia mifumo ya nchi mbalimbali namna inavyotekeleza masuala ya usalama barabarani.

“Nilisema tangu Septemba 19, mwaka huu, jambo hili lisitekelezwe na kwa yeyote aliyetendewa hivyo, inamaana maelekezo niliyoyatoa hayajafuatwa, msiwe na wasiwasi madereva, serikali yenu ni sikivu na Rais Dk. Samia anajua umuhimu wenu,”alisema.

Akizungumzia suala la ‘kuovateki,’ alisema kumekuwa na baadhi ya madereva kuonesha ushindani wa kuendesha magari kwa kasi, hivyo, aliwasihi kuacha kufanya kazi kwa kutegana au kuviziana.

Alisema kufanya hivyo, kuna hatari kubwa ya kusababisha ajali kutokea, akaliagiza Jeshi la Polisi, kuweka utaratibu wa kubaini na kufuatilia mienendo ya usalama barabarani.

KAMISHNA WA OPERESHENI

Awali, kabla ya Katambi na madereva, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadh Haji, aliwataka makamanda wa polisi mikoani, kuendelea kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya atakayebainika kuhusika katika vitendo vya kuzuia mabasi na malori kuendelea na safari.

Haji alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu vuguvugu la mgomo wa madereva wa mabasi na malori, lililoibuka jana asubuhi na kuzua taharuki kwa wananachi.

Alisema kuwa, kitendo cha mtu au kikundi kuzuia magari yasitembee barabarani ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Alisema Jeshi la Polisi, halitasita kuchukua hatua dhidi ya watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

““Makamanda wa mikoa yote nchini, tumewaelekeza waendelee kufuatilia na kuchukua hatua kwa mtu yeyote atakayebainika kuhusika katika vitendo vya kuzuia mabasi na malori kuendelea na safari zao

“Kwa yeyote anayefanya hivyo, kuzuia magari anapaswa kufahamu ni kosa kwa mujibu wa sheria.

“Jeshi la Polisi linatoa onyo kali na halitasita kuchukua hatua kali sana kwa mtu yeyote atakayebainika kuzuia magari, mabasi au malori kutembea barabarani,” alisema.

Alisema hatua hizo, hazitaishia kwa wanaozuia magari pekee, zitawahusu watakaofanya vitendo vya hujuma, uharibifu au uvunjifu mwingine wa sheria dhidi ya mabasi, malori na magari mengine yanayotumia barabara.

Pia, alisema baadhi ya mabasi yanaendelea na safari, ingawa yanapofika katika baadhi ya maeneo hukutana na watu wanaowatisha madereva kwa kuwapa taarifa wasiendelee na safari kwa kuwa, magari yao yatafanyiwa vitendo vya uharibifu.

Alisema Jeshi la Polisi, limejipanga kuhakikisha usalama wa mabasi, malori na magari mengine unaendelea kuwepo, huku akiwataka wamiliki na madereva kuendelea na safari bila hofu.

DC MSANDO

Mapema asubuhi, akiwa Stendi ya Magufuli, Mkuu wa Wilaya Ubungo, Albert Msando, aliwataka abiria waliokuwa tayari kwa safari maeneo tofauti, kupanda mabasi yao na kusubiri utaratibu ulioandaliwa.

NENO LA ABIRIA

Monica Salehe alisema amesikitishwa madereva kuwakatisha tiketi huku wakifahamu hawatafanya safari.

“Nipo hapa tangu saa 12 asubuhi nataka kwenda Songea, lakini sijui mwafaka wangu kwa sababu, hata dereva wa basi langu simuoni,”alisema.

KAULI YA TABOA

Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), kimewasihi madereva kuendelea na shughuli za usafirishaji kama kawaida wakati serikali ikiendelea kushughulikia changamoto zao.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mkuu wa TABOA,  Priscus Joseph, alisema madereva waligoma kutokana na madai yao mbalimbali.

MADEREVA

Dereva wa basi la Sai baba Express yanayofanya safari kati ya Arusha na Dar es Salaam, Halfan Hakimu, alisema mgomo umetokana na changamoto zao za barabarani.

Alisema changamoto hizo ni kukatwa pointi na kufungiwa leseni zao jambo ambalo limewakosesha amani.

“Hatutaki kugoma, imetubidi kugoma tuna njaa na familia zetu wanatutegemea, imetubidi kugoma ili tuweze kusikilizwa,”alisema.

Dereva wa basi ya Oveoili linalofanya safari Dar es Salaam kwenda Kigoma, Abdul Kasonda, alidai kukatwa pointi katika leseni zao, ndiyo chanzo kikubwa cha mgomo.

MKOANI SIMIYU

Kutoka mkoani Simiyu, madereva wa mabasi walisema hawakufanya safari zao kutokana na mgomo unaendelea nchi nzima, wakishinikiza kutokatwa pointi katika leseni zao.

Dotto Kingi wa basi za Ally Star, alisema mabasi yote yanayoanzia safari zake katika Stendi ya Somanda (Bariadi) kwenda mikoani hayajafanya safari kutokana na mgomo unaoendelea hadi watakapotatuliwa kero zao.

MKOANI KILIMANJARO

Akizungumza kuhusu sababu za mgomo huo, dereva Emmanuel Singine, alisema mfumo wa faini na kukatwa pointi unawaweka katika mazingira magumu kiuchumi.

Singine alisema dereva anapofanya kosa na kutozwa faini sh. 30,000, pia hukatwa pointi licha ya kuwa na majukumu ya kifamilia.

Msimamizi wa Stendi ya Mabasi Kilimanjaro, Samuel Mlay, alisema tangu asubuhi, kituo hicho kilikumbwa na changamoto baada ya madereva wa mabasi yanayofanya safari zao mikoani kugoma.

HUKO MOROGORO

Akizungumza na gazeti hili, dereva Augostino Andrew, alisema utaratibu ulioanzishwa wa uwakatwaji pointi madereva, hawauafiki.

“Mimi ni dereva wa basi, ninafanya safari kati ya Mbeya na Dar es Salaam, kuna siku nikiwa njiani maeneo ya Mikese Morogoro, trafiki aliingia kwenye gari na kukuta abiria wanne hawajafunga mikanda, aliamua kukata alama tano,” alisema Anderw.

JIJINI ARUSHA

Mmoja wa madereva wa mabasi mkoani hapa ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema mfumo huo siyo rafiki kwa upande wao.

“Hatujaridhika na mfumo, kama wanataka uwajibikaji uzingatie pia wamiliki wa magari, hasa pale ukiukaji wa baadhi ya masharti ya usalama unapotokana na ubovu wa chombo, yakiwemo magurudumu yaliyochakaa au taa zisizofanya kazi,”alisema.

MKOANI TANGA

Mamia ya abiria walikwama katika Kituo Kikuu cha Mabasi Kange jijini Tanga kufuatia hatua ya madereva wa mabasi  kusitisha safari ghafla.

Mgomo huo, uliotokana na kile kinachoelezwa madai yao ya muda mrefu dhidi ya mamlaka za usalama barabarani.

Mwakilishi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Tanga, Michael Kimia, alikiri kuwepo changamoto hiyo na kueleza mgomo huo una muunganiko.

JIJINI MWANZA

Madereva wa mabasi katika Stendi ya Nyegezi, jana jioni walianza kutoa magari yao baada ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa, kuzungumza nao na kutoa ufafanuzi kuhusu mfumo wa ‘Drivers Points System’ ambao umekuwa ukitajwa kuwa chanzo cha malalamiko.

Akizungumza na madereva na abiria katika stendi hiyo jana, Mutafungwa alisema mfumo huo haujaanza kutekelezwa.

Alisema serikali imetoa ufafanuzi kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Katambi kuwa, suala hilo liko katika mchakato.

MWENYEKITI WAMILIKI MALORI

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Malori Tanzania (TAMSTOA), Chuki Shabani, aliwashauri madereva kuondoa hofu kwa kuwa changamoto zao zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi.

Alisema madereva wanapaswa kuwa watulivu na kuvumilia kwani serikali ipo kwa ajili yao.

Habari imeandikwa na Rehema Maigala, Ziana Bakari, Costantine Mathias, Willium Paul, Warioba Igombe, Lilian Joel, Mashaka Mhando, Baltazar Mashaka na Sauma Mwanshuli (OUT)

Previous Post

MASHILI ATIMIZA AHADI, AKABIDHI MSAADA WA KICHOMEA TAKA

Next Post

TANZANIA YAENDELEA KUJIIMARISHA KATIKA USIMAMIZI WA MAAFA

Next Post
TANZANIA YAENDELEA KUJIIMARISHA KATIKA USIMAMIZI WA MAAFA

TANZANIA YAENDELEA KUJIIMARISHA KATIKA USIMAMIZI WA MAAFA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WALIOTAJWA UBADHIRIFU RIPOTI YA CAG KIKAANGONI

WALIOTAJWA UBADHIRIFU RIPOTI YA CAG KIKAANGONI

6 months ago
DK. NCHIMBI ATOA KAULI UBORESHAJI WA MITAALA

DK. NCHIMBI ATOA KAULI UBORESHAJI WA MITAALA

7 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?