• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TANZANIA YAENDELEA KUJIIMARISHA KATIKA USIMAMIZI WA MAAFA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 29, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TANZANIA YAENDELEA KUJIIMARISHA KATIKA USIMAMIZI WA MAAFA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu – Ankara Uturuki

SERIKALI ya Tanzania imesema inaendelea kujenga uwezo wa kukabiliana na maafa nchini kwa kutumia teknolojia za kisasa, ikiwamo satelaiti na akili unde (AI), ili kuimarisha tahadhari za mapema, mipango ya kujiandaa, kukabili na urejeshaji hali pindi maafa yanapotokea.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi, wakati wa ziara yake ya kikazi mjini Ankara, Uturuki iliyolenga kuimarisha uwezo wa kitaasisi, kuongeza maarifa ya kiufundi na kukuza ushirikiano katika kupunguza vihatarishi vya maafa, kukabiliana na dharura na mifumo ya kurejesha hali kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kiteknolojia.

Dkt. Yonazi ametembelea na kujionea namna Taasisi ya Turksat inavyotekeleza majukumu yake ikiwemo ya huduma za satelaiti, mawasiliano na teknolojia za anga ambayo inamilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Uturuki.

Turksat ndiyo mwendeshaji pekee wa satelaiti za mawasiliano nchini humo na hutoa huduma za data, interneti na mawasiliano kwa shughuli za kila siku za taasisi za umma na binafsi za ndani na nje ya nchi pamoja na maeneo ambayo miundombinu ya kawaida ni hafifu.

Katika kubadilishana uzoefu ameeleza kuwa, Tanzania inaendelea kuangalia namna ya kuongeza uwezo wa kutumia taarifa za satelaiti pamoja na teknolojia ya akili unde, hatua ambayo itasaidia kutoa taarifa za mapema kuhusu maeneo hatarishi na kuwezesha mamlaka kupanga namna bora ya kuzuia na kupunguza madhara ya majanga na kukabiliana na maafa.

Kwa mujibu wa Dkt. Yonazi, Ofisi ya Waziri Mkuu inalichukulia suala la kuzuia na kukabiliana na maafa kama jambo la kitaifa linalohitaji kujengewa uwezo wa kutosha katika maeneo yote ya nchi na si kuwa na uwezo wa kuokoa watu pekee wakati wa majanga, bali kuhakikisha usimamizi wa maafa unakuwa sehemu ya usalama wa nchi.

Akizungumzia matumizi ya teknolojia hiyo katika kukabiliana na mafuriko, Dkt. Yonazi alisema uwezo wa satelaiti unaweza kusaidia kutambua kina cha maji katika mito na maeneo yenye vihatarishi, pamoja na kutathmini ukubwa wa madhara yanayoweza kujitokeza.

Aidha, amesema kuwa taarifa hizo zitasaidia kuwezesha Serikali kupanga mapema rasilimali zitakazohitajika katika kuzuia na kupunguza madhara pamoja na kuandaa rasilimali ikiwemo vifaa na timu kwenye maeneo yanayoweza kuathirika.

Akitoa maelezo kuhusu taasisi ya Turksat, Mkurugenzi wa huduma za satelaiti na mauzo Bw. Fuat Eroglu amesema taasisi hiyo ina sateliti sita angani na imeendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi yaliyogawanyika katika maeneo makuu matatu yanayohusu mawasiliano ya Satelaiti, huduma za mawimbi ya luninga na redio na data za interneti na Mifumo ya Teknolojia ya Habari kwa ajili ya Serikali Mtandao (e-Government).

Alisema pia taasisi hiyo inasambaza vifaa kwa ajili ya vituo vya huduma ya data za intaneti na mawimbi ya televisheni na redio kupitia satelaiti wakati wa maafa ili kuwezesha mawasiliano ya dharura pale ambapo minara ya simu na mkongo wa mawasiliano umeathirika.

“Kwa upande wa Mawasiliano ya Dharura na Kimkakati Turksat inatoa miundombinu salama ya mawasiliano kwa sekta za kimkakati kama vile usalama wa umma, jeshi, usafiri wa baharini, usafiri wa anga na mifumo ya mawasiliano wakati wa majanga ya asili au dharura,” alisema Eroglu

Previous Post

KATAMBI AOKOA JAHAZI MGOMO MADEREVA NCHINI

Next Post

RAIS DK. SAMIA ATEUA MA-DC 22

Next Post
RAIS DK. SAMIA ATEUA MA-DC 22

RAIS DK. SAMIA ATEUA MA-DC 22

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA

WAZIRI MKUU ARIDHISHWA UJENZI BANDARI YA UVUVI KILWA

10 months ago
YANGA, SIMBA TAMBO TUPU

YANGA, SIMBA TAMBO TUPU

7 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?