• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TRILIONI 2.46/- ZATENGWA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO YA NISHATI – HOMERA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 7, 2026
in Habari, Kitaifa
0
TRILIONI 2.46/- ZATENGWA KWA AJILI YA MIRADI YA MAENDELEO YA NISHATI – HOMERA
0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nishati, Dk. Juma Zuberi Homera, amesema Serikali imetenga Shilingi trilioni 2.46, sawa na asilimia 97.5 ya bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/27, kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta ya nishati.

Amesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha nchi inakuwa na nishati ya uhakika, ya kutosha na inayokidhi mahitaji ya wananchi pamoja na shughuli za kiuchumi.

Homera amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuweka msukumo katika kukuza sekta ya nishati ili iwe kichocheo cha ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.

Ametoa kauli hiyo leo, Oktoba 7, 2026, akifungua Maonesho ya 10 ya Kimataifa ya Biashara ya Nishati ya Umeme na Nishati ya Jua (Power and Solar Energy International Trade Event), yanayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Expo Centre, jijini Dar es Salaam, kuanzia Oktoba 7 hadi 10, 2026.

Amesema kupitia bajeti hiyo, Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme kwa Maji wa Julius Nyerere pamoja na Mradi wa Umeme wa Jua wa Kishapu, ambapo megawati 50 tayari zimeunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na awamu ya pili inatarajiwa kuongeza megawati 100.

Kwa mujibu wa Mhe. Homera, bajeti hiyo pia inalenga kuharakisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kitaifa, ikiwemo Ajenda ya Mission 300 inayolenga kuunganisha wateja wapya wa umeme milioni 1.7 kila mwaka na kufikisha jumla ya wateja milioni 8.3 ifikapo mwaka 2030.

Aidha, amesema Serikali inaendelea kutekeleza Mkakati wa Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024–2034, wenye lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Ametaja pia Mradi wa Umeme Vijijini kupitia mpango wa kupeleka umeme katika vitongoji 9,009 ifikapo mwaka 2030, kwa gharama ya Shilingi trilioni 1.2, pamoja na kuimarisha mchanganyiko wa vyanzo vya nishati (Energy Mix) kwa kuongeza mchango wa nishati jadidifu kutoka asilimia 61.8 hadi asilimia 75 ifikapo mwaka 2030.

Waziri Homera amesisitiza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unahitaji ushiriki mkubwa wa sekta binafsi, hususan wawekezaji na wadau wenye teknolojia, mitaji na ujuzi wa kisasa, ili kuongeza kasi ya maendeleo ya sekta ya nishati na kuendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Maonesho hayo yamewakutanisha wawekezaji, wazalishaji na wasambazaji wa teknolojia za nishati ya umeme na nishati ya jua kutoka nchi 48 duniani, kwa lengo la kuonesha teknolojia na suluhisho mbalimbali zinazoweza kuchangia katika maendeleo ya sekta ya nishati.

Homera amewahimiza Watanzania kutembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo ili kujionea teknolojia zinazotumika katika sekta ya nishati, kujifunza na kuongeza uelewa kuhusu fursa na ubunifu unaoendelea katika sekta hiyo.

Previous Post

TANZANIA U-23 BAHATI MBAYA

Next Post

UN YAIPA MAUA YAKE TANZANIA KWA AMANI

Next Post
UN YAIPA MAUA YAKE TANZANIA KWA AMANI

UN YAIPA MAUA YAKE TANZANIA KWA AMANI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DIARRA MTEGONI TUZO KIPA BORA

DIARRA MTEGONI TUZO KIPA BORA

6 months ago
SERIKALI KUANGALIA FURSA ZA MIKOPO KWA WANAOSOMA KOZI FUPI – WAZIRI MKUU

SERIKALI KUANGALIA FURSA ZA MIKOPO KWA WANAOSOMA KOZI FUPI – WAZIRI MKUU

2 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?