• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 8, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

HAWA NGADALA Na SYLVIA SEBASTIAN

ZIKIWA zimepita siku sita tangu mkazi wa Bunju A, Dar es Salaam, Laurent Kweka, kudaiwa kumuua kwa risasi mkewe Jenipher  Urassa, viongozi wa eneo hilo wamedai baadhi ya mambo yaliyochangia kutokea mkasa huo.

Inadaiwa Oktoba Mosi, mwaka huu, saa 11 alifajiri, Kweka alimpiga mke wake risasi kichwani na baadaye kujisalimisha Kituo cha Polisi Kawe, kabla ya kupelekwa Polisi Mabwepande na kuhamishiwa Kituo cha Oysterbay.

Akizungumza na waandishi wa UHURU kuhusiana na tukio hilo, Mtendaji wa Kata ya Bunju A, Theophil Mwinuka, alidai alipata taarifa za mauaji hayo kupitia simu aliyopigiwa na kiongozi wa serikali ya mtaa.

Alidai baada ya katika tukio hilo, alikuta mwili wa Jenipher  uko chini jambo lililomlazimu kutoa taarifa polisi, huku mtuhumiwa akitoweka.

Mwinuka alidai dada wa kazi wa nyumbani kwa wanandoa hao, alimueleza mauaji hayo yalifanyika saa 11 alfajiri muda mfupi baada ya kumfungulia geti Kweka na kuingia ndani na kuanza kubishana na Jenipher  kwa sauti kubwa.

“Dada huyo wa kazi alidai baadaye alisikia mlio mkubwa na kumuona Kweka anatoka ndani akiwa amebeba begi huku akizungumza: “tayari nishamaliza kazi”, mtendaji huyo alinukuu.

Hata hivyo, Mwinuka alikiri kufahamu alichodai kiini cha mgogoro kati ya wanandoa hao, akifafanua Jenipher  alikwenda katika ofisi hiyo ya kata kutoa taarifa ya matatizo yao na Kweka alipopewa wito afike katika shauri hilo hakufanya hivyo.

“Mgogoro wa wanandoa hao ninaufahamu, ulipelekwa dawati la jinsia Jenipher  akawa anafika, lakini Kweka hakuitikia wito,” alidai.

Aliendelea kudai, pia kulikuwa na mgogoro wa umiliki wa kiwanja uliotokana na Kweka kutaka kubadilisha hati ya kiwanja kilichonunuliwa na Jenipher .

MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkoani, Asha Miraji, alidai alipigiwa simu na mjumbe wa shina saa 12 asubuhi na kuchukua usafiri wa pikipiki kwenda eneo la tukio, ambako alikuta askari wamefika na kuanza uchunguzi baada ya kukuta ganda la risasi.

“Ndugu na askari walieleza hakuna kitu kilichopaswa kutolewa ndani ya nyumba hiyo isipokuwa gari la Kweka ambalo lilikuwa nje ya nyumba,” alidai Asha.

Akiendelea kusimulia, mwenyekiti huyo alidai alianza kumfahamu Kweka Julai, mwaka huu, ambapo alifika ofisini kwake kudai hati ya mauziano ya eneo hilo la nyumbani kwake iliyokuwa imepotea na kuomba apewe nyingine.

Asha alidai Kweka alikuwa na picha yake na mkewe, lakini mjumbe wa eneo hilo alikataa kutia saini nyaraka zilizowasilishwa baada ya kubaini mhusika hakuwa mnunuzi wa awali na miongoni mwa mashahidi waliowekwa kwenye mkataba huo alikuwa ndugu yake Kweka.

Vilevile, Kweka aliwasilisha malalamiko mengine akidai kuna mtu aliyekuwa anajenga katika eneo lenye barabara, jambo lililofuatiliwa na wataalamu wa ardhi na kuelezwa ujenzi huo ulikuwa sahihi, huku jirani huyo akishauriwa kufuatilia vibali vya ujenzi.

KATIBU WA SHINA

Katibu wa Shina Namba 20, Zoni ya Senzele, Bunju, Shabani Simba, akizungumzia hali ya familia hiyo, alidai wanandoa hao walihamia eneo hilo miezi tisa iliyopita na hawakuwa wakifahamu migogoro ya ndani, bali walichokifahamu ni Kweka kugombana na majirani zake sababu ya mipaka ya maeneo yao.

”Mwanamke (Jenipher ) alikuwa siyo wa kujichanganya sana na watu wa mtaa huu, lakini mume  wake tunamfahamu kwa kiasi hii familia haina muda mrefu tangu wamehamia wana takriban miezi tisa na kwa muda walioishi hapa, Kweka ameshagombana na baadhi ya majirani zake kutokana na mipaka,

“Anaingia katika maeneo ya wenzake hadi wenye mamlaka (serikali) walifika kupima ikaonekana Kweka ameingia eneo la wenzake baada ya wapimaji kufika,” alidai.

KUHUSU HALI ILIVYOKUWA

Aidha, ndugu aliyekataa kutaja jina lake, alidai Septemba 30, mwaka huu, Jenipher  aliyekuwa ameondoka katika nyumba hiyo kutokana na msuguano na mumewe, aliuawa katika nyumba hiyo baada ya kwenda kuwaona watoto na kuwanunulia vyakula ambavyo vilikuwa vimeisha, huku baba yao akiwa hayupo.

“Jenipher  baada ya kufika kwa watoto aliamua kulala na ilipofika asubuhi alijiandaa kwenda kazini, ambapo saa 11 alfajiri kabla hajatoka, alishtuka kuona Kweka ameshaingia ndani baada ya kufunguliwa geti na dada wa kazi,” alidai ndugu huyo.

Alizidi kudai: “Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa dada wa kazi, baada ya Kweka kuingia ndani, yeye (dada wa kazi) alishuka ghorofani kwenda kuendelea na kazi za usafi ndipo ghafla alisikia mlio wa risasi. Alipopanda juu alikutana na Kweka akiwa amebeba begi jeusi na bastola huku akimwambia ameshamaliza kazi.”

Alidai dada huyo wa kazi alikwenda chumbani alikomkuta Jenipher  amefariki dunia, hivyo alianza kuwaita majirani lakini hawakusikia kwa sababu ilikuwa bado hakujapambazuka vizuri.

Dada wa kazi alipoona majirani hawasikii, aliwapigia simu ndugu wa marehemu na bahati nzuri mjomba wao alikuwa anatoka safarini mkoani Kilimanjaro, alipata ujumbe akiwa maeneo ya Bunju, hivyo aliwataarifu polisi kilichojiri.

Alidai wakati mwili wa marehemu unapelekwa hospitali kuhifadhiwa, walipata taarifa Kweka alikuwa ameshajisalimisha polisi Kawe.

Ndugu huyo aliongeza wakati mauaji hayo yanatokea, watoto walikuwa bado wamelala, ambapo walipata taarifa baada ya majirani na polisi kufika eneo la tukio.

KUZIKWA KESHO KILIMANJARO

Taarifa rasmi iliyotolewa na Allan Urassa, ilieleza mwili wa marehemu utaagwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Tangi Bovu, Dar es Salaam leo na baadaye kusafirishwa kwenda Machame, mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika kesho.

Previous Post

TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

Next Post

KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

Next Post
KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

KUDUMISHA SERA YA CHINA MOJA NA KUIMARISHA URAFIKI KATI YA CHINA NA TANZANIA

5 months ago
ANNA ABDALLAH, LUBINGA, KHATIB WAUTETEA MUUNGANO

ANNA ABDALLAH, LUBINGA, KHATIB WAUTETEA MUUNGANO

2 months ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?