• ePaper
Friday, October 23, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

YANGA YAIDUWAZA CFFA 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 17, 2026
in Burudani, Michezo
0
YANGA YAIDUWAZA CFFA 
0
SHARES
2
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

YANGA iiliiduwaza timu ya CFFA ya Madagascar kwa kuichapa mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Pambano hilo la raundi ya pili ya kufuzu hatua ya mtoano , lilipigwa  kuanzia saa 9:00 alasiri  katika Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, mabao ya ushindi yalipachikwa wavuni na Cheikh Toure, Albert Kangwanda, Mudathir Yahya na Max Nzengeli.

Kufuatia ushindi huo, Yanga imejiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mashindano hayo makubwa Barani Afrika, siku chache baada ya Jumamosi iliyopita kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa watani wao wa jadi, Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Yanga itabidi kusubiri kucheza mchezo wa marudiano kati yake na CFFA unatarajiwa kuchezwa Oktoba 21, mwaka huu katika Uwanja wa Azam Complex,Dar es Salaam na mshindi wa jumla baada ya dakika 180 ataingia rasmi katika hatua ya makundi ya timu 16 bora barani Afrika.

Baada ya mchezo huo, baadhi ya wachezaji wa timu hiyo walionekana kukaa chini uwanjani na wengine wakiwa benchi wakijishika kichwa, wakionekana kutoamini kipigo hicho walichokipata.

Timu hizo zinatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano Oktoba 21 mwaka huu mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza kwa kasi huku timu zote zikionekana kupatambana kupata ushindi,dakika ya 11 Yanga ilikosa bao baada ya mchezaji wake, Albert Kangwanda kupiga shuti kali na mpira kutoka nje, Kangwanda alimalizia pasi safi kutoka kwa Mudathir Yahya.

Yanga waliendelea kufanya mashambulizi, dakika ya 25, Peter Shalulile alipiga shuti kali na kipa wa CFFA aliokoa mpira huo, akimalizia pasi safi kutoka kwa Kangwanda.

Timu hizo ziliendelea kufanya mashambulizi kwa zamu na dakika ya 30, Kangwanda alikosa bao baada ya kupiga shuti kali na mpira kutoka nje, Kangwanda alipokea pasi kutoka kwa Shalulile.

Yanga ilipata bao la kuongoza dakika ya 40 ya mchezo baada ya Cheikh Toure kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa CFFA na kuingia kambani, kufuatia kipa huyo kuutema mpira uliopigwa.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza kwa bao hilo 1-0, kipindi cha pili kilianza kwa kasi.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi, Yanga ilipata bao la pili dakika ya 47 kupitia kwa mchezaji wake, Kangwanda baada ya kupiga shuti kali na mpira kuingia kambani, mchezaji huyo alipokea pasi kutoka kwa kwa Toure.

Timu hiyo ilionekana na kiu ya upata ushindi, dakika ya 54 Mudathir Yahya alifunga bao la tatu baada ya kupiga shuti kali nje ya 18 na kuingia kambani, Mudathir alipokea mpira kutoka kwa Kangwanda.

Kasi ilizidi kuongezeka, Yanga ilipata bao jingine katika dakika ya 59, baada ya Maxi Nzengeli kupiga shuti kali na mpira kuingia kambani, Maxi alimalizia pasi safi kutoka kwa Juma Abushiri.

Timu hizo ziliendelea kupambana na dakika ya 80, Maxi alikosa bao baada ya kupiga shuti kali na mpira kugonga mwamba, Nzengeli alipokea pasi safi kutoka kwa Mohamed Hussein.

Yanga ilifikia hatua hiyo baada ya kuitoa Gaborone United ya Botswana kwa jumla ya mabao mabao 3-2.

Katika mchezo wa kwanza waliocheza ugenini, Yanga walipata sare ya bao 1-1 kabla ya kurejea nyumbani na kushinda mabao 2-1.

Kikosi cha Yanga: Abutwalibu Mshery, Yao Kouassi, Mohamed Hussein, Ibrahim Bacca, Farouk Komara, Fred Ngoma, Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya, Peter Shalulile, Albert Kangwanda na Cheikh Ibrahima Toure.

Previous Post

‘PAREDI’ LA JIHAN LAFUNIKA

Next Post

NDEJEMBI AWEKA MSIMAMO

Next Post
NDEJEMBI AWEKA MSIMAMO

NDEJEMBI AWEKA MSIMAMO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

SERIKALI KUZALISHA MAELFU YA AJIRA KWA VIJANA KUPITIA MRADI WA UCHIMBAJI WA VISIMA VYA UMWAGILIAJI

3 months ago
SIKUKUU YA BURUDANI

SIKUKUU YA BURUDANI

1 year ago

Popular News

  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKURASA MPYA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIKOMO BEI ZA MAFUTA ZINAVYO MLINDA MWANANCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DOUMBIA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA IFAD

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?