• ePaper
Friday, October 23, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Burudani

‘PAREDI’ LA JIHAN LAFUNIKA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 17, 2026
in Burudani, Habari, Kimataifa, Kitaifa, Michezo
0
‘PAREDI’ LA JIHAN LAFUNIKA
0
SHARES
9
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NASRA KITANA

PAREDI  la kumpokea Jihan Dimack, mshindi wa Miss Grand International 2026, limefunika na kuweka rekodi ya kuwa Miss wa kwanza kurudi nchini na kupokelewa kwa paredi iliyofanyika kwa zaidi ya saa nne.

Rekodi hiyo imewekwa baada ya mrembo huyo kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  hadi Dar Village, mashabiki wengi walijitokeza kumpokea akitokea Bangkok nchini Thailand.

Jihan ameweka historia ya kuwa Miss wa kwanza kurudi nchini na kupokelewa kwa paredi iliyofanyika kwa zaidi ya masaa manne kuanzia saa kutoka Uwanja wa Ndege hadi Dar Village.

Msafara wa mwanadada huyo ulianzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa, kupitia Tazara, Kariakoo Msimbazi, Fire, Posta, Daraja la Tanzanite, Coco Beach na kufikia Dar Village kwa ajili ya kuendelea na sherehe, ambapo kulikuwa na vinywaji vya bure.

Mrembo huyo alishinda mashindano ya Miss Grand International 2026 yaliyofanyika katika jijini la Bangkok, Thailand, ambapo Jihan Dimack aliibuka mshindi na kutwaa taji hilo katika fainali zilizofanyika Oktoba 10, mwaka huu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuchukua taji hilo ambalo lilianzishwa rasmi mwaka 2013 nchini Thailand na mshindi wa kwanza alikuwa Janelee Chaparro kutoka nchini Puerto Rico huku Jihan akipokea kijiti kutoka kwa Emma Tiglao kutoka nchini Filipino ambaye alishinda taji hilo, mwaka 2025.

Katika mapokezi hayo, wananchi wengi walifika uwanja wa ndege mapema kuanzia saa 2:00 asubuhi kwa ajili ya kumpokea shujaa huyo wa nchi.

Hadi kufika saa 4:00 asubuhi, watu walifurika huku mvua ikinyesha lakini walivumilia kumsubiri shuja wa nchi.

Mlibwende huyo alitua nchini Tanzania majira ya saa sita kamili mchana na kupokelea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa na Mwanamuziki Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’.

Pia, walikuwepo warembo wenye mataji mbalimbali waliojitokeza kumpokea mshindi huyo wa Miss Grand International, wakiwemo Elizabeth Makune, Miss Universe Tanzania 2026 na Sandra, Miss Cham 2026.

Nje ya Uwanja wa ndege kulikuwa na burudani mbalimbali za asili ikiwemo ngoma za asili, burudani za  muziki na jamii ya wamasai ambao walikuwa wakitumbuiza.

Licha ya ngoma hizo kulikuwa na matarumbeta ambayo yalikuwa yanapigwa kila mahala katika uwanja huo wa ndege huku baadhi ya Watanzania wakiwa wamevalia fulana zilizosomeka ‘karibu nyumbani Jihan’.

Jihan amewasili nchini akifuatana na Rais wa Miss Grand International, Nawat Itsaragrisil ambapo wote wawili walipokewa kwa shangwe na Watanzania waliofika uwanjani hapo.

Baada ya kuwasili, mrembo huyo alipanda gari maalum aliloandaliwa huku likiwa limepambwa na vinyago vya asili.

Pia, katika gari hilo, kulikuwa na picha za wanyama kama, Simba, Chui na Pundamilia.

KARIAKOO YASIMAMA

Shangwe na nderemo zilitanda Kariakoo, jijini Dar es Salaam, huku wananchi na wafanyabiashara wakijitokeza kumlaki mshindi huyo wa Miss Grand International 2026, baada ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika jukwaa la kimataifa.

MSIGWA ATOA NENO

Akizungumza baada ya kumpokea Miss huyo, Msemaji wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa alisema serikali ipo tayari kumuunga mkono mtu yeyote atakayeipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano na shughuli mbalimbali nje ya nchi.

Alifafanua kuwa Watanzania wanapaswa kuendeleza umoja na mshikamano walioonyesha kwa Jihan Dimack, aliyeshinda taji la Miss Grand International 2026 kwani ushirikiano huo unaweza kuleta mafanikio makubwa zaidi kwa nchi.

“Watanzania tukiendeleza umoja huu kwa Jihan, basi tutafanya makubwa zaidi, kwani keki ya nchi ni kubwa,” alisema.

Aidha Msigwa aliwataka Watanzania kujiandaa na mashindano ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika nchini mwakani.

Pia, aliwahimiza wadau wa sekta mbalimbali kuonesha ubunifu wao ili kutumia fursa zitakazojitokeza katika mashindano hayo.

JIHAN ASHANGAZWA NA MAPOKEZI HAYO

Jihan Dimack alisema hakutarajia kupata mapokezi makubwa kama hayo, hivyo aliwashukuru Watanzania wote kwa kujitokeza kwa pamoja kumpokea ni jambo kubwa sana kwake.

Aliongeza kuwa hakutarajia kukutana na umati mkubwa kama huo. ameamini Watanzania wana upendo na hatokuja kuwasahau.

Alisema ushindi huo siyo wa kwake peke yake, bali ni wa Tanzania nzima.

“Kiukweli nashukuru sana kwa mapokezi makubwa ya leo, sikutarajia hali hii kwa kweli, na wala sikujua kama kutakuwa na umati mkubwa kama huu kiukweli huu ni upendo mkubwa sana kwangu, nawapenda wote na huu ni ushindi wetu wote siyo wangu peke yangu,” alisema Jihan.

Hata hivyo, Jihan alisema anaishukuru serikali kwa sapoti kubwa waliomuonyesha tangu alipokuwa katika mashindano hadi kufikia hapa alipo.

Pia, alisema anawashukuru Watanzania wote waliomuonyesha upendo mkubwa hadi kufikia hapo alipo.

SABABU YA JIHAN KUBEBWA KATIKA GARI MAALUMU

Muhamasishaji Jenifer Jovin maarufu  ‘Niffer’ alisema kila kitu kilichokuwepo katika gari hilo, kilikuwa na maana yake ya kutambulisha utalii nchini.

“Tulitaka kutumia wanyama halisi, tukaona itakuwa kasheshe hapa yupo Chui, Simba na Pundamilia, tulikuwa na uwezo wa kuweka maua Lakini yanamaanisha nini?, hivyo tumeamua kuweka hii ili kutangaza utalii wetu. Kila kitu tunachofanya kina maana kwa ajili ya Miss wetu na nchi yetu,” alisema Niffer.

Mwanadada huyo alisema umati wa watu waliojitokeza kumpokea mwanadada huyo umemdhihirishia ni kwa namna gani Watanzania wana upendo na nchi yao na kutoa sapoti kwa kila anayeleta mafanikio hapa nchini.

WAREMBO WAMPONGEZA JIHAN

Miss Cham, Sandra Giovinazzo, Mtanzania wa kwanza kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Miss Cham yatakayofanyika mwezi Desemba, mwaka huu, alisema ushindi wa Jihan umeonesha jinsi sekta ya ulimbwende inavyoweza kufungua fursa za ajira na kuboresha maisha ya watu.

Sandra alisema awali mashindano ya ulimbwende yalionekana kama mashindano ya kawaida yaliyohusishwa na uvunjifu wa maadili, lakini kwa sasa yamepata heshima kubwa nchini na duniani kwa ujumla.

Miss Universe Elizabeth Makune ni miongoni mwa warembo walioenda kumpokea Jihan alisema anampongeza mrembo huyo na kusema kuwa amewapa hamasa na moyo wa mapambano ili kufanya vizuri zaidi katika mashindano mengine.

Naye aliyewahi kushinda taji la Miss Tanzania mwaka 2020, Rose Manfere, alisema Watanzania kwa sasa wamekuwa wakiunga mkono tasnia ya ulimbwende tofauti na ilivyokuwa hapo awali, jambo ambalo amelipongeza sana.

WANANCHI WALIOJITOKEZA WATOA NENO

Wananchi mbalimbali waliojitokeza kumpokea Jihan wamesema kuwa wamefurahi kwa mafanikio makubwa aliyoyapata Jihan na ndio maana wamejitokeza kwa wingi ili kumsapoto leo.

Fatuma Kitasa alisema hiyo ni furaha ya Watanzania wote ndio maana wamejitokeza kwa wingi kuhakikisha wanampokea kwa mbwembe na bashasha kubwa.

Naye mfanyabiashara maarufu Twalib Bakari maarufu kama Anko T alisema siku zote katika mambo mazuri, Watanzania wanatakiwa kuungana kwa pamoja katika jambo la kujenga taifa.

Previous Post

NDEJEMBI AWAOMBA WANANCHI KUMCHAGUA NDILITO KWA KISHINDO

Next Post

YANGA YAIDUWAZA CFFA 

Next Post
YANGA YAIDUWAZA CFFA 

YANGA YAIDUWAZA CFFA 

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WATANZANIA 37,647,235 KUPIGA KURA LEO

WATANZANIA 37,647,235 KUPIGA KURA LEO

12 months ago
ANNA ABDALLAH, LUBINGA, KHATIB WAUTETEA MUUNGANO

ANNA ABDALLAH, LUBINGA, KHATIB WAUTETEA MUUNGANO

3 months ago

Popular News

  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKURASA MPYA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIKOMO BEI ZA MAFUTA ZINAVYO MLINDA MWANANCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DOUMBIA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA IFAD

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?