• ePaper
Thursday, October 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

NDEJEMBI AWAOMBA WANANCHI KUMCHAGUA NDILITO KWA KISHINDO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 16, 2026
in Habari, Kitaifa
0
NDEJEMBI AWAOMBA WANANCHI KUMCHAGUA NDILITO KWA KISHINDO
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi ameshiriki ufunguzi wa Kampeni za mgombea Ubunge wa Jimbo la Chamwino kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Nettho Ndilito, zilizofanyika katika Kijiji cha Dabalo Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, leo tarehe 16 Oktoba 2026.

Katika ufunguzi wa kampeni hizo, Ndejembi amewasihi wananchi wa Jimbo la Chamwino kumchagua kwa kishindo Dk. Ndilito, ili aweze kuendeleza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika jimbo hilo hususani huduma za kijamii kama vile maji, umeme, miundombinu ya barabara, shule, vituo vya afya na zahanati.

Amesema kupitia Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imetekeleza miradi muhimu ya huduma za kijamii katika jimbo hilo, hivyo shukrani pekee zinazofaa  ni kumchagua Dkt. Ndilito ili aendelee kuisimamia vema Ilani ya CCM katika Jimbo hilo.

Ndejembi amewataka wagombea wote walioshiriki mchakato wa ndani wa Chama Cha Mapinduzi kuungana kwa pamoja na wana CCM wengine kuhakikisha Dk. Ndilito anapata ushindi wa kishindo.

Makamu wa Rais Ndejembi ambaye awali alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo, amewaahidi wananchi wa Chamwino kuendelea kushirikiana nao vema kuhakikisha jimbo hilo linapata maendeleo yaliyokusudiwa.

Amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye ni Rais Dk. Samia kwa maendeleo makubwa yaliyopatikana katika Jimbo hilo, huku akiwasisitiza wananchi wa Jimbo hilo kuendelea kumuombea Mhe. Rais katika utekelezaji wa majukumu yake.

Ndejembi ametumia nafasi hiyo, kuwashukuru wananchi wa Jimbo la Chamwino kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote alichohudumu akiwa Mbunge wa Jimbo hilo. Amesema daima anathamini mchango wa kila mwananchi wa Chamwino alioutoa kuhakikisha maendeleo yanapatikana.

Hafla ya uzinduzi ya wa Kampeni za Ubunge wa Jimbo la Chamwino kupitia CCM, zimehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Wabunge, Madiwani na Wananchi mbalimbali.

Previous Post

WAZIRI ULEGA AAGIZA UKAGUZI WA MAHABUSU NCHINI

Next Post

‘PAREDI’ LA JIHAN LAFUNIKA

Next Post
‘PAREDI’ LA JIHAN LAFUNIKA

‘PAREDI’ LA JIHAN LAFUNIKA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWINYI: SITAKI KUACHA DENI

DK. MWINYI: SITAKI KUACHA DENI

1 year ago
FIFA YADHAMIRIA KUWEKA NGUVU TANZANIA

FIFA YADHAMIRIA KUWEKA NGUVU TANZANIA

9 months ago

Popular News

  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKURASA MPYA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIKOMO BEI ZA MAFUTA ZINAVYO MLINDA MWANANCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DOUMBIA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA IFAD

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?