• ePaper
Thursday, October 22, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

WAZIRI ULEGA AAGIZA UKAGUZI WA MAHABUSU NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 15, 2026
in Habari, Kitaifa
0
WAZIRI ULEGA AAGIZA UKAGUZI WA MAHABUSU NCHINI
0
SHARES
8
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Abdallah Hamis Ulega, ameelekeza utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Jaji Chande pamoja na maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Serikali, akiwemo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuendelea kufanya kaguzi  katika maeneo ya Mahabusu  na  Magereza kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za kijinai  ili kuendelea kuhakikisha hakuna  msongamano wa Mahabusu na pamoja na kuwawezesha watuhumiwa wanaostahili kupata dhamana kwa mujibu wa sheria.

Waziri Ulega ametoa maelekezo hayo leo, wakati wa kikao cha kujitambulisha katika Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Njedengwa jijini Dodoma, ambapo amesisitiza umuhimu wa watendaji kutekeleza majukumu yao kwa bidii, weledi na ufanisi ili kuimarisha upatikanaji wa haki nchini.

“Ni lazima tufanye kazi usiku na mchana kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume ya Jaji Chande na maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Serikali, ili kuhakikisha kesi zinashughulikiwa na kufikishwa mahakamani kwa wakati, na watuhumiwa wanaostahili wanapata dhamana kwa mujibu wa sheria. Lengo letu ni kupunguza msongamano wa mahabusu na kuhakikisha haki inapatikana kwa wakati,” amesema Waziri Ulega.

Amesisitiza kuwa ukaguzi wa mahabusu unapaswa kufanyika kwa kasi na ufanisi nchini kote ili kubaini changamoto zinazochangia msongamano huo, kufuatilia hatua za kesi za watuhumiwa na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

Aidha, ameelekeza kesi zinazostahili kufikishwa mahakamani ziwasilishwe kwa wakati, huku watuhumiwa wanaokidhi vigezo vya kupata dhamana wakipatiwa haki hiyo bila ucheleweshaji usio wa lazima, kwa kuzingatia masharti ya sheria husika.

Waziri Ulega ameeleza kuwa utekelezaji wa maelekezo hayo utasaidia kupunguza msongamano wa mahabusu, kupunguza malalamiko ya wananchi na kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Waziri Ulega ameeleza kufurahishwa na ongezeko la watendaji kutoka 630 hadi 1,200, akisisitiza kuwa ongezeko hilo linapaswa kuendana na kuimarika kwa kasi ya utendaji, weledi na ufanisi katika kutekeleza majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ili kuleta matokeo yanayotarajiwa katika mfumo wa utoaji haki nchini.

Vilevile, amevitaka vitengo vinavyohusika na elimu kwa umma kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya dhamana, ili waelewe vigezo na taratibu za kisheria zinazotumika katika utoaji wa dhamana na haki za watuhumiwa.

Amesema elimu hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki zao, kupunguza malalamiko yanayotokana na kutofahamu taratibu za kisheria na kuimarisha imani ya umma katika mfumo wa utoaji haki nchini.

Previous Post

NYERERE ANAISHI

Next Post

NDEJEMBI AWAOMBA WANANCHI KUMCHAGUA NDILITO KWA KISHINDO

Next Post
NDEJEMBI AWAOMBA WANANCHI KUMCHAGUA NDILITO KWA KISHINDO

NDEJEMBI AWAOMBA WANANCHI KUMCHAGUA NDILITO KWA KISHINDO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAMBO YAZIDI KUNOGA AFCON 2027

MAMBO YAZIDI KUNOGA AFCON 2027

6 months ago
HALI YA USALAMA MKOA WA ARUSHA NI SHWARI – RC MAKALLA

HALI YA USALAMA MKOA WA ARUSHA NI SHWARI – RC MAKALLA

12 months ago

Popular News

  • SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA URATIBU WA MAFUNZO TARAJALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UKURASA MPYA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KIKOMO BEI ZA MAFUTA ZINAVYO MLINDA MWANANCHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DOUMBIA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI MKUU ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA IFAD

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?