• ePaper
Monday, November 2, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

PROF. MBARAWA AMPA ONYO  MKANDARASI MRADI WA SGR TABORA- ISAKA 

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 27, 2026
in Habari, Kitaifa
0
PROF. MBARAWA AMPA ONYO  MKANDARASI MRADI WA SGR TABORA- ISAKA 
0
SHARES
11
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Uchukuzi  Prof. Makame  Mbarawa amesemakua Shirika la Reli Tanzania (TRC) linastahili pongezi kwa kazi kubwa ya kiusimamizi na kitaalamu kuhakikisha kipande cha nne cha SGR (Tabora-Isaka),Ujenzi wake unaendelea vizuri.

Aidha, Prof. Mbarawa, amempa onyo  mkandarasi kampuni ya Yapi Merkezi kwa  kushindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati na kuipongeza kampuni saidizi (subcontractor) CCECC, ambayo imetekeleza mradi huo kwa asilimia 5 katika kipindi cha miezi miwili Septemba na Oktoba 2026 sawa na miaka minne iliyotekeleza kampuni ya Yapi Merkezi.

Kutokana na uchelewezashaji uliofanywa na Kampuni ya Yapi Merkezi Prof. Mbarawa, amesema Serikali haitavumilia uzembe wa wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza miradi kwa kasi inayotakiwa, huku akilipongeza Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa namna lilivyotumia mkakati mbadala kurejesha kasi ya ujenzi wa reli ya SGR katika kipande cha Tabora–Isaka, chenye urefu wa kilomita 165

“Baada ya tathmini kufanyika, Serikali ilibaini kuwa kumwondoa moja kwa moja Mkandarsi huyu  kungeweza kuongeza ucheleweshaji na changamoto za kifedha, hivyo akashauriwa kutafuta mkandarasi mdogo mwenye uwezo wa kumsaidia” Alisema Mbarawa.

Profesa Mbarwa, amesema kitendo cha TRC kutia nguvu  kiusimamizi na kitaalamu kumesaidia kuongeza nguvu utekelezaji wa mradi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha nne ( Tabora–Isaka,) huku kasi ya ujenzi ikiongezeka na kuimarisha matumaini ya kukamilika kwa wakati mwaka mnamo mwaka 2028.

“TRC, chini ya Mkurugenzi Mkuu wake, Mhandisi Machibya Shiwa, imefanya kazi kubwa kuweka mazingira wezeshi yaliyomuwezesha mkandarasi kuendelea na utekelezaji wa mradi huo, ambao umekuwa ukisuasua na sasa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, Watanzania wanashuhudia hali ya mambo katika mradi huo”, amesema Prof. Mbarawa.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa TRC  Mhandisi Machibya Shiwa alisema TRC inaendelea kusimamia mradi kwa karibu, ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa vifaa muhimu na udhibiti wa matumizi ya fedha ili kuongeza kasi ya utekelezaji.

Kipande cha Tabora–Isaka kina urefu wa kilomita 165 na kina thamani ya dola za Marekani milioni 909.1, ikijumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

Previous Post

TPDC : TUNAPIMA MAFANIKIO YA MIRADI YA MAFUTA NA GESI KWA MANUFAA YA WANANCHI

Next Post

MAGEREZA: LISSU  HAJAGOMA KULA, YUPO SALAMA

Next Post
MAGEREZA: LISSU  HAJAGOMA KULA, YUPO SALAMA

MAGEREZA: LISSU  HAJAGOMA KULA, YUPO SALAMA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

KATIBA MSINGI WA HAKI – DK. NCHIMBI

3 months ago
DK. SAMIA, AHIMIZA WAKULIMA WAJISAJILI KATIKA MFUMO WA RUZUKU YA MBEGU, PEMBEJEO

DK. SAMIA, AHIMIZA WAKULIMA WAJISAJILI KATIKA MFUMO WA RUZUKU YA MBEGU, PEMBEJEO

1 year ago

Popular News

  • WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    WAZIRI MKUU AAGIZA MPANGO WA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA TAASISI ZA DINI KATIKA ELIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI WA NYERERE AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUANGALIE MUSTAKABALI WA VIJANA WETU – WAZIRI MKUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYAMA VYA SIASA VYAMPONGEZA RAIS DK. SAMIA UJENZI MJI WA SERIKALI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA, ANGOLA ZAFUNGUA FURSA MPYA ZA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?