Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi kimesema kitashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu kwa mujibu wa sheria na taratibu za kidemokrasia kwani hakuna sababu ya CCM kushindwa Visiwani Zanzibar .
Katibu wa Kamati Maalum ya Nec Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ,Khamisi Mbeto Khamis, ameeleza hayo baada ya mgombea Urais wa CCM, Rais Dk Hussein Ali Mwinyi alipohutubia maelefu ya wana CCM na Wananchi.
Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za CCM kwa Zanzibar ,zimezinduliwa katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Mwenyekiti Mao Tse Tung, Kisiwani Unguja.
Mbeto amesema Ushindi wa CCM hauna kizuizi chochote baada ya serikali ya Awamu ya Nane kutimiza wajibu wa kuwatumikia wananchi chini ya serikali ya Rais Dk Mwinyi.
Amesema haiba ya Ustawi wa Maendeleo inayoonekana Unguja na Pemba ,ni tiketi itakayokipatia Ushindi wa kishindo CCM Mwaka 2025-2030.
“CCM hakina sababu ya kushindwa Uchaguzi huu . Kimetekeleza kwa vitendo Sera zake kwa ufanisi na viwango stahili ” Alisema Mbeto