• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SIKU 100 ZA KAZI NA UTU

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 11, 2026
in Habari, Kitaifa
0
SIKU 100 ZA KAZI NA UTU
0
SHARES
10
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na WANDISHI WETU

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ametimiza siku 100, tangu alipoapishwa kuongoza nchi katika awamu ya pili ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Rais Dk. Samia, alipata ushindi wa asilimia 97.66, katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, mwaka jana.

Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana, Rais Dk. Samia, alitoa ahadi ya kutekeleza mambo mbalimbali ndani ya siku 100.

Miongoni mwa ahadi hizo ni kuanzisha Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, kuajiri watumishi wa afya 5,000 na kupiga marufuku hospitali zote kuzuia miili ya marehemu kuchukuliwa na ndugu zao.

Katika sekta ya elimu, aliahidi kuanzisha mkakati wa kisayansi, kuhakikisha wanafunzi wa darasa la tatu wanajua Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) na kuajiri walimu 7,000.

Pia, Rais Samia, aliahidi kutoa sh. bilioni 200 kuwezesha mitaji na kurasimisha sekta zisizo rasmi hususani kwa vijana na wanawake. Ahadi zote ametekeleza.

Baada ya kuapishwa Novemba 3, mwaka jana, Rais Samia, alianza utekelezaji wa ahadi zake kupitia sekta mbalimbali.

Mawaziri wa kisekta, walitangaza mafanikio mengi yaliyopatikana katika wizara zao ndani ya siku 100 zilizohitimishwa jana.

Wakizungumzia utekelezaji wa ahadi za siku 100 za Rais Samia, baadhi ya wadau nchini wakimemo wanasiasa wakongwe, walisema mafanikio makubwa yamepatikana.

Wadau hao, walisema katika kipindi kifupi, Rais Samia, ametekeleza ahadi zake kwa kuwaletea maendeleo wananchi kupitia miradi mbaliambali ya kisekta.

MZEE MSEKWA

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Spika wa Bunge Mstaafu, Pius Msekwa, alisema Rais Samia, ametekeleza ahadi na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vitendo.

Msekwa, alisema Rais Samia, amefanya mageuzi katika sekta ya afya kwa kufanikisha Bima ya Afya kwa Wote, huduma ya maji na kuimarisha sekta ya elimu.

“Nampongeza Rais Samia, ametekeleza kwa vitendo ahadi zake, ameboresha sekta ya afya, elimu, ujenzi wa madarasa ameajiri walimu,” alisema.

Msekwa, alisema Rais Samia, amezifanyia kazi changamoto zilizowagusa wananchi alipokuwa akifanya kampeni, akimtaja kuwa kiongozi wa mfano wa kuigwa.

ANNA ABDALLAH

Waziri wa zamani na mwanasiasa mkongwe, Anna Abdallah, alisema uongozi wa Rais Samia ndani ya kipindi cha siku 100, umeleta matokeo makubwa  yaliyogusa moja kwa moja maisha ya wananchi.

Alisema Rais Samia, ametekeleza kwa vitendo ahadi alizotoa wakati wa kampeni, akatoa rai kwa mawaziri, wakuu wa taasisi nchini, kutekeleza majukumu ipasavyo.

“Nampongeza Rais Samia ndani ya siku 100, tumeona matokeo makubwa zaidi kila wizara imeonesha imefanikiwa kwa kiwango kikubwa.

“Natoa rai kwa watendaji mawaziri, makatibu wakuu, wafanye kazi kulingana na imani waliyopewa na Rais,” alisema.

NGEMELA LUBINGA

Naye Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Mstaafu, Kanali Ngemela Lubinga, alimpongeza Rais Samia kwa kutekeleza ahadi zake ndani ya siku 100 kwa vitendo.

“Nampongeza Rais Samia kutekeleza kwa umakini ahadi zote alizotoa ndani ya siku 100.

“Wenye dhamana ambao wapo katika utekelezaji wa ahadi zake za siku 100, wametimiza wajibu wao ipasavyo,”alisema.

Aidha, Lubinga alisema uthabiti wa Rais Samia katika utendaji, umeonekana kwa sababu, ameanza kutekeleza kwa vitendo Ilani ya CCM ya 2025/2030.

Hata hivyo, alitoa rai kwa waliopewa dhamana ya kusimamia taasisi, wizara na maeneo mbalimbali, kufanya kazi kwa bidii, kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia, kuwaletea maendeleo wananchi.

MHADHIRI DANINGA  

Mhadhiri wa Idara ya Uongozi, Maadili na Utawala wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dk. Philip Daninga, alisema sekta ya afya imepata mafanikio makubwa ndani ya siku 100.

“Tayari ajira za wataalamu wa afya, zimeshafanyika, hii ni hatua kubwa kwasababu awali sekta hii ilikuwa na changamoto ya uhaba wa wafanyakazi,” alisema.

Pia, alisema sekta ya miundombinu imepata maendeleo makubwa, ambapo ujenzi wa Soko Kuu la Kariakoo ilikuwa ni kipaumbele cha Rais Dk. Samia.

Dk. Daninga, alibainisha juhudi hizo za Rais Samia, hazina ukomo katika sekta ya uchumi pekee, zimegusa maeneo mengine muhimu ikiwemo sekta ya utalii.

“Sekta ya utalii, inaendelea kufanikishwa na jitihada zake hatua inayochangia ukuaji wa uchumi wa taifa, uimara wa sarafu yetu unazidi kuimarika chini ya uongozi wake,” alisema.

“Rais anatekeleza kwa bidii na jitihada zake kubwa za kuleta maendeleo ya kweli zinaonekana, hii ni ishara tosha kwamba taifa linaendelea kusonga mbele chini ya uongozi wake,” aliongeza.

GWIJI WA UCHUMI

Gwiji wa uchumi Profesa Samwel Wangwe, alisema ndani ya siku 100, ahadi alizotoa kwa wananchi, zimeonekana kwa utekelezaji hasa katika sekta ya afya na elimu ambazo amezipa kipaumbele.

“Walimu 7,000 na madaktari 5,000 wameajiriwa na hili ni jambo la kupongeza inaonesha dhihirisho la ahadi alizotoa Rais,” alisema Profesa Wangwe.

“Hii ni hatua muhimu ya kuhakikisha maendeleo yanayotarajiwa katika sekta hizi muhimu na kuleta tija kwa taifa,” aliongeza.

MGANGA MFAWIDHI

Naye Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Mongo la Ndege, iliyopo Halmshauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dk. Nuru Kanungila, alisema Rais Samia, ametengeneza ajira nyingi kwa vijana ndani ya sekta hiyo.

“Siku 100 ni chache lakini kwa uhodari na ushupavu alionao Rais Samia, umeleta tabasamu kubwa wa vijana, tumeona ndani ya siku 100 vituo vya afya vingi vimefunguliwa na vingine vinaendelea kufunguliwa.

“Tuna kila sababu ya kumpongeza Rais Samia kutuletea Bima ya Afya kwa Wote, hii imekuwa faraja kwa wananchi, hadi hivi sasa nikiongelea katika kituo change cha kazi nimeshaona wateja wengi wanufaika wa Bima ya Afya kwa Wote,”alisema.

MWENYEKITI SOKO LA KARIAKOO

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Soko Kuu la Kariakoo, Severin Mushi, alimpongeza Rais Dk. Samia kwa kasi kubwa aliyoanza nayo hususan utekelezaji wa ahadi za siku 100 kwa vitendo.

“Tunampongeza Rais Dk. Samia, wafanyabiashara tuko pamoja naye kwasababu ametekeleza kwa vitendo ahadi alizoahidi,”alisema.

UTEKELEZAJI

Bima ya Afya kwa Wote imeanza kutekelezwa Januari 26, 2026.

Katika awamu ya kwanza, wananchi 1,457,602, sawa na kaya 276,004 zisizo na uwezo, watasajiliwa na kugharimiwa na serikali.

Katika kundi hilo, wamo wazee 229 na watoto 267 ambao wanahudumiwa katika vituo maalumu chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu.

Jumla ya wananchi 3,695,465, sawa na kaya 931,693, wametambuliwa kutokuwa na uwezo, wakiwemo wajawazito na watu wenye ulemavu.

Desemba mwaka jana, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilivuka lengo la ukusanyaji.

Desemba mwaka jana, TRA ilivuka lengo kwa kukusanya sh. trilioni 4.130, wakati lengo lililowekwa kwa mwezi huo, lilikuwa kukusanya sh. trilioni 4.14.

MIKOPO

Katika kipindi cha siku 100, serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO), imetoa mikopo yenye thamani ya sh. milioni 821.7 kwa wajasiriamali wadogo na katika mikoa 19 nchini.

Mikopo hiyo, imezalisha ajira 546 za moja kwa moja na ajira 436 za vijana, sambamba na zaidi ya ajira 1,000 zisizo za moja kwa moja katika sekta za viwanda, kilimo, ufugaji na biashara.

VIWANDA

Serikali imeanzisha mitaa ya viwanda katika mikoa 11 ikilenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, madini na misitu. 

Mikoa hiyo Manyara, Singida, Mbeya, Iringa, Shinyanga, Ruvuma, Morogoro, Kilimanjaro, Dodoma, Tabora na Kigoma.

USAFIRI WA RELI

Katika kipindi cha siku 100, serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imeimarisha usafiri wa reli ya TAZARA.

“Mkataba wa ufufuaji na uboreshaji mkubwa wa Reli ya TAZARA ulisainiwa Septemba 29 mwaka jana baina ya serikali za Tanzania na Zambia kwa kushirikiana na Kampuni ya CCECC ya China,” alisema Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa.

Vilevile, alisema serikali imekamilisha upembuzi yakinifu kwa ujenzi wa reli ya kisasa za mijini katika Jiji la Dar es Salaam na Dodoma.

Profesa Mbarawa alisema katika kipindi cha siku 100 shirika hilo, limesafirisha abiria takribani 838,870 ambapo asilimia 89 ni abiria wa SGR na asilimia 21 ni wa MGR. Upande wa mizigo tani 85,735 zimesafirisha katika kipindi husika. 

MIRADI YA UJENZI

Pia, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, imetekeleza ujenzi wa miradi 81 yenye thamani ya sh, bilioni 500, ambayo imejumuisha ukarabati wa barabara za lami.

Pia, ujenzi wa madaraja na uwekaji taa za barabarani katika siku 100 za mafaniko ya Rais Dk, Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100.

Aidha, wizara hiyo, imepokea sh. bilioni 511 kutoka vyanzo mbalimbali ambapo sh. bilioni 280, zimetoka Hazina na sehemu ya fedha hizo, zimetumika kulipa wakandarasi wadogo katika mikoa kupitia Ofisi za Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Waziri  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,Profesa Adolf Mkenda, alisema wizara imenunua na kusambaza vifaa vya kidijitali na saidizi vyenye thamani ya sh. bilioni 5.35 kwa walimu na walimu tarajali wenye ulemavu katika halmashauri zote 184 nchini.

Aidha, Waziri huyo alisema Serikali inaendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa vyuo 64 vya Ufundi Stadi (VETA) ngazi ya wilaya, ambapo ujenzi wake umefikia wastani wa asilimia 67.

 “Vyuo hivyo vikikamilika vitakuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi takribani 33,000 kwa mwaka katika fani mbalimbali za ujuzi, jambo litakaloongeza fursa za ajira na kujiajiri kwa vijana.”amefafanua Profesa Mkenda.

MAJI

Kwa upande wa Wizara ya Maji, katika kipindi cha siku 100, miradi 16 ya maji yenye thamani ya sh. bilioni 16.28 imekamilika katika mikoa mbalimbali ikiwemo Simiyu, Njombe, Iringa, Kilimanjaro, Dodoma, Geita na Tanga.

Kukamilika kwa miradi hiyo kumewezesha wananchi zaidi ya 118,400 kupata huduma ya maji safi na salama, hivyo kupunguza umbali wa kutafuta maji na kuboresha maisha yao ya kila siku.

Previous Post

BIMA YA AFYA YAHITAJI UANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI

Next Post

ULEGA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAKANDARASI NCHINI

Next Post
ULEGA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAKANDARASI NCHINI

ULEGA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAKANDARASI NCHINI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

OMR YANAWIRI KARATA WANAWAKE MEI MOSI

OMR YANAWIRI KARATA WANAWAKE MEI MOSI

3 days ago
MWANASHERIA WA KWANZA MWANAMKE UDSM AFARIKI

MWANASHERIA WA KWANZA MWANAMKE UDSM AFARIKI

1 month ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?