• ePaper
Sunday, June 14, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

ULEGA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAKANDARASI NCHINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 11, 2026
in Habari, Kitaifa
0
ULEGA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAKANDARASI NCHINI
0
SHARES
21
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU, Same

WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ameagiza wakandarasi nchini kuwalipa watumishi kwa mujibu wa sheria za nchi.

Waziri huyo ametoa maelekezo kayo jana, akikagua maendeleo ya barabara ya Same- Kisiwani- Mkomazi yenye urefu wa kilometa 100.5 ambayo inajengwa na mkandarasi M/S China Communication Construction Companya Ltd.

Katika tukio hilo alipata malalamiko kuwa wafanyakazi katika ujenzi huo wanalipwa fedha kidogo tofauti na kinachokubalika kisheria. 

“Hii haikubaliki. Kuna viwango ambavyo tumekubaliana kwa mujibu wa sheria zetu, ni lazima wakandarasi wote wafuate viwango hivyo. Hilo halina mjadala; alisema Ulega.

Ingawa msimamizi wa kampuni hiyo alimuahidi Ulega suala hilo litafanyiwa kazi, lakini alisema atalifikisha suala hilo kwa Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, ili wamiliki wa kampuni hiyo waitwe nchini na kukubali rasmi kufuata sheria za Tanzania katika malipo. 

Katika hotuba yake baada ya ukaguzi huo, Ulega pia alieleza kutofurahishwa na kusuasua kwa mradi huo ulioanza  kutekelezwa tangu mwezi Januari, mwaka jana. 

” Nilimkabidhi mwenyewe  mradi huu mkandarasi mwaka jana, nimetembelea na kuuona, ukweli ni kwamba bado mkandarasi kasi yake ni ndogo hairidhishi na haifurahishi”, alisema Ulega. 

Aliongeza kuwa serikali inataka kuona  kuwa  barabara hiyo inakamilika kwa wakati na ubora ili isaidie kurahisisha shughuli za kijamii na kiuchumi.

Aliwahakikishia wananchi wa Same kuwa ujenzi wa barabara hiyo utaenda sambamba na ujenzi wa vituo na uwekaji wa taa za barabarani kuleta mwanga ili kuchochea shughuli za kibiashara katika  maeneo yao. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu alisema kiu ya wananchi wa Same ni kuona barabara hiyo inakamilika ili kuweza kurahisisha shughuli za kiuchumi na kuleta maendeleo katika wilaya hiyo na taifa.

Mradi huo umefika asilimia saba na unagharimiwa na serikali.

Previous Post

SIKU 100 ZA KAZI NA UTU

Next Post

SIKU 100 ZA KUFUNGUA ANGA, RELI NA BANDARI

Next Post
SIKU 100 ZA KUFUNGUA ANGA, RELI NA BANDARI

SIKU 100 ZA KUFUNGUA ANGA, RELI NA BANDARI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

RAIS DK. SAMIA AWAPA TABASAMU WAPIGANAJI

4 weeks ago
AELEZA CCM ITAKAVYO JENGA UCHUMI JUMUISHI

AELEZA CCM ITAKAVYO JENGA UCHUMI JUMUISHI

9 months ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    RAIS DK. SAMIA ATAKA MIKOPO ISIWE MZIGO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • AFRIKA KUCHOCHEA UTUNZAJI MAZINGIRA KUPITIA NISHATI SAFI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO AOMBA RADHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • YANGA, SIMBA NI KIVINGINE ZAIDI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MEXICO YAANZA KWA KISHINDO WC, KADI ZATEMBEA HATARI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?