• ePaper
Thursday, April 30, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SIKU 100 ZA KUFUNGUA ANGA, RELI NA BANDARI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 11, 2026
in Habari, Kitaifa, Makala
0
SIKU 100 ZA KUFUNGUA ANGA, RELI NA BANDARI
0
SHARES
17
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na FRED ALFRED, Dodoma

KATIKA kipindi cha siku 100 za uongozi wa Awamu ya Sita, Serikali chini ya Rais Dk. SamiaSuluhu Hassan imeendelea kutekeleza kwa vitendo dhamira yake ya kuboresha na kuimarisha sekta ya uchukuzi kwa lengo la kuifungua nchi.

Ndani ya siku 100, Rais Dk. Samia amegusa mambo sita katika sekta ya uchukuzi, likiwemo la uwekezaji mkubwa katika reli, bandari, viwanja vya ndege na  usalama wa usafiri wa majini.

Hatua hizo zimeendelea kuifanya Tanzania kuwa kitovu muhimu cha usafirishaji katika ukanda wa Afrika mashariki na kati.

MABORESHO RELI TAZARA

Katika kipindi hicho cha siku 100,serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imepiga hatua kubwa kuimarisha usafiri wa reli ya TAZARA, ambayo kwa muda mrefu uendeshaji wake umekuwa wa kusuasua.

Alisema katika kufufua reli hiyo, Serikali imekamilisha hatua zote muhimu zinazotakiwa zikiwemo kuhitimisha majadiliano na wawekezaji husika.

“Mkataba wa ufufuaji na uboreshaji mkubwa wa Reli ya TAZARA ulisainiwa Septemba 29 mwaka jana, baina ya Serikali za Tanzania na Zambia kwa kushirikiana na Kampuni ya CCECC ya China,”alifafanua.

Aliongeza kuwa:”Mradi huu utaiwezesha Reli ya TAZARA kuongeza ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam, kuimarisha biashara na usafirishaji kati ya Tanzania na nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kufungua fursa za kiuchumi na ajira katika mikoa yote inayopitiwa na reli hiyo.”

RELI ZA MIJINI

Vilevile, alisema serikali imekamilisha upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa za mijini katika Jiji la Dar es Salaam na Dodoma.

Alisema hatua hiyo imewezesha kupatikana kwa fedha za msaada (grant), kwa ajili ya usanifu wa kina, hatua itakayofungua njia ya utekelezaji wa mradi huo unaolenga kupunguza msongamano wa usafiri wa umma na kuongeza tija katika miji mikuu ya kiutawala na kibiashara nchini.

Profesa Mbarawa alisema katika kipindi cha siku 100 Shirika limesafirisha abiria takribani 838,870,ambaoa silimia 89 niwa SGR na asilimia 21 wa MGR.

Alisema, kwa upande wa mizigo tani 85,735 zimesafirisha katika kipindi husika. 

“Huduma ya SGR imesafirisha viongozi mbalimbali, watalii kuelekea maeneo mbalimbali mfano Mikumi, Ruaha na Udzungwa kufanya shughuli mbalimbali za kitalii, wafanyabiashara, wananchi na makundi ya wanafunzi katika kipindi cha likizo ambao wamekuwa wakielekea maeneo mbalimbali ya kujifunza,”alifafanua WaziriMbarawa.

Aliongeza kuwa:”Hii ni hatua kubwa na mafanikio ya kihistoria, ambayo nimiongoni mwa mambo makubwa yaliyofanywa chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia.”

Katika hatua nyingine,alisema shirika limepokea vichwa vya treni viwili na mabehewa 50 ya usafirishaji wa mizigo kwanjia ya MGR. 

Alisema vitendea kazi hivyo vinalenga kuongeza uwezo wausafirishaji washirika na kukuzabiashara ya usafirishaji wa mizigo na kuongeza kwamba, Serikali kupitia TRC imeendelea na ujenzi wareli ya SGR kwa awamu ya kwanza inayotoka Dar es Salaam hadi Mwanza, yenye jumla ya kilometa 1,219 za njiakuu na kilometa 377 zakupishana.

“Utekelezaji wa awamuhii umegawanyika katika vipande vitano; ambavyo ni Dar es Salaam-Morogoro kilometa 300, Morogoro-Makutupora kilometa 422, Makutupora-Tabora kilometa 368,Tabora-Isaka kilometa 165 na Isaka-Mwanza kilometa 341.

Aliongeza kuwa:”Utekelezaji wa kipande cha Dar es Salaam hadi Dodoma umekamilika na uendeshaji wake unaendelea,ambao kipande cha kuingia bandarini kimefikia asilimia 99.93.”

UENDELEZAJI WA BANDARI

Profesa Mbarawa alisema serikali imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika bandari na usafiri majini kama nguzo muhimu ya biashara ya ndani, kikanda na kimataifa.

Alieleza kuwa, katika kipindi cha siku 100 za Awamu ya Sita, wizara imekamilisha taratibu za kuanza upanuzi mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam wenye lengo la kujenga magati 10 na matenki 15 ya mafuta.

Profesa Mbarawa alisema ujenzi wa magati mawili ya awali yenye urefu wa mita 500 utaanza Juni mwaka huu, huku ujenzi wa matenki ukiendelea kutekelezwa kwa mafanikio makubwa.

“Uboreshaji huu utaongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia shehena hadi tani milioni 50 kwa mwaka, ndani ya kipindi kifupi, kutoka takribani tani milioni 32 za sasa,”alisema.

Kwa mujibu wa Profesa Mbarawa, serikali imeanza maandalizi ya ujenzi wa Bandari kubwa na ya kisasa ya Bagamoyo.

Alisema  awamu ya kwanza ya mradi huo itahusisha ujenzi wa gati lenye urefu wa kilometa 1.32, kuhudumia meli kubwa za kisasa.

“Bandari hii ni ya kimkakati katika kupunguza msongamano wa Bandari ya Dar es Salaam na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji wa baharini katika ukanda wa Afrika Mashariki,”alisema.

Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa alisema serikali imeanza utekelezaji wa Mradi wa Kurasini Logistics Terminal, unaolenga kupunguza msongamano wa shehena katika Bandari ya Dar es Salaam na kuongeza miundombinu muhimu ya kuhudumia shehena inayoharibika haraka.

Alisema mradi huo unahusisha ujenzi wa kituo cha kisasa cha kuhifadhi makasha kwa muda katika eneo la mita za mraba 210,000, chenye uwezo wa kuhifadhi hadi makasha 700,000.

USAFIRI WA MAJINI

Profesa Mbarawa alisema serikali  imeweka kipaumbele kikubwa katika kulinda maisha ya wananchi, mali zao kupitia kuimarisha mifumo ya utafutaji na uokoaji.

Alifafanua kuwa, lengo ni kuhakikisha hakuna mwananchi anayepoteza maisha wakati akijitafutia riziki yake ndani ya maji na hata tatizo likitokea kunakuwa na namna ya kumuokoa mhusika.

“Katika kipindi cha ndani ya siku 100; katika eneo hili serikali imekamilisha  ujenzi wa Kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokoaji cha Kikanda (Maritime Rescue Coordination Centre– MRCC), katika Ziwa Victoria Mwanza. Kituo hiki kitaimarisha usalama wa usafiri wa majini katika Ziwa Victoria kwa kutumia mifumo ya kisasa ya mawasiliano, TEHAMA na vifaa vya uokoaji,”alisema.

Aliongeza kuwa:”Wizara imenunua boti maalumu ya wagonjwa  kwa ajili ya Ziwa Victoria, ambayo tayari imewasili na iko tayari kutoa huduma na hii ni kama hospitali inayotembea majini.”

Alisema hiyo ni hatua ya kihistoria itakayoboresha huduma za afya na uokoaji kwa wananchi waishio visiwani na maeneo ya mwambao wa ziwa.

Vilevile, alisema serikali imenunua boti nne za utafutaji na uokoaji na kuanza kutumika katika Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria na Ukanda wa Bahari ya Hindi (Tanga), hatua inayoongeza uwezo wa Taifa letu katika kukabiliana na majanga ya majini.

VIWANJA VYA NDEGE

Kuhusu sekta ya anga, Profesa Mbarawa alisema serikali imekamilisha ujenzi wa Jengo la Viongozi katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere – Terminal I na jengo hilo limezinduliwa rasmi Januari 16 mwaka huu.

Alisema jengo hilo la kisasa na la kwanza kwa Ukanda wa Afrika Mashariki, lina uwezo wa kuhudumia wakuu wa nchi watano kwa wakati mmoja, hivyo uwepo wake utaimarisha heshima na hadhi ya Tanzania kimataifa.

“Maandalizi ya awali ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Serengeti na Kiwanja kipya cha Mkoa wa Kagera yameanza. Pia, maandalizi ya mradi wa ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege na ujenzi wa Jengo la Watu Mashuhuri Kiwanja cha Ndege cha KIA yanaendelea,” aliongeza.

Aliongeza kuwa:”Miradi hii ni muhimu katika kukuza utalii, biashara na uunganishwaji wa maeneo ya kimkakati ya nchi na masoko ya kikanda na kimataifa.”

Vilevile, alisema kwa upande wa usafirishaji wa abiria, serikali imeendelea kuboresha na kupanua wigo wa utoaji huduma kupitia Kampuni ya Ndege (ATCL).

Profesa Mbarawa alisema katika kipindi hiki ATCL imeongeza vituo vya huduma vya Victoria Falls (Zimbabwe), Cape Town (Afrika Kusini) na Accra (Ghana) na kuifanya kampuni kuwa na jumla ya vituo 32, kati ya hivyo vituo 15 ni vya ndani ya nchi, 14 vya ndani ya Bara la Afrika na vituo vitatu  ni vya kimataifa.

“Ufunguzi wa vituo vipya umesaidia kuwa na muunganiko wa safari, hivyo kuleta ufanisi na urahisi wa wananchi kuendelea kupata huduma na kufanya shughuli zao za maendeleo,”alifafanua.

Aliongeza kuwa:”Katika kipindi hiki Wizara imehakikisha kuwa ndege zote 16 zilizopo zinafanya kazi kuendelea kutoa huduma.”

KUIUNGANISHA NCHI KIKANDA

Profesa Mbarawa alisema miradi yote ina lengo kuu la kuiunganisha Tanzania kikanda na kimataifa katika nyanja za uchukuzi, kwa kuwa lango kuu la biashara na usafirishaji kwa nchi zisizo na bandarina kuongeza ushindani wa uchumi.

Alisema Tanzania imeendelea kuhudumia nchi zisizo na bandari kwa ufanisi, ambazo ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Zimbabwe na Malawi.

“Kupitia maboresho ya reli, bandari, viwanja vya ndege na usalama wa majini, Tanzania inaendelea kujijenga kama kitovu cha lojistiki katika Afrika Mashariki na Kati, hali itakayoboresha utoaji wa huduma za uchukuzi na kuongeza mapato, ajira na ustawi wa wananchi,” alifafanua.

Previous Post

ULEGA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAKANDARASI NCHINI

Next Post

WADAU WAMPA TANO RAIS DK. SAMIA KUIHESHIMISHA TAIFA STARS

Next Post
WADAU WAMPA TANO RAIS DK. SAMIA KUIHESHIMISHA TAIFA STARS

WADAU WAMPA TANO RAIS DK. SAMIA KUIHESHIMISHA TAIFA STARS

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AIJAZA NOTI YANGA

RAIS DK. SAMIA AIJAZA NOTI YANGA

2 weeks ago
MCHUJO MKALI  KOCHA SIMBA

MCHUJO MKALI  KOCHA SIMBA

5 months ago

Popular News

  • TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • VYALENGA KUIJENGA JAMII KIUCHUMI NA KIROHO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KUVUMILIANA MUHIMU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • WAZIRI SANGU ABAINISHA HIFADHI SKIMU INAVYOENDA KUBADILI MAISHA YA WATANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA: WAAJILI WATEKELEZE NYONGEZA YA KIMA CHA MISHAHARA SEKTA BINAFSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?