• ePaper
Thursday, June 25, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. MWINYI AELEZA FAIDA YA KULINDA TUNU YA AMANI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
April 4, 2026
in Habari, Kitaifa
0
RAIS DK. MWINYI AELEZA FAIDA YA KULINDA TUNU YA AMANI
0
SHARES
13
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU, Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha na kulinda tunu ya amani iliyopo nchini.

Pia, Rais Dk. Mwinyi amehimiza kuendelezwa mshikamano, kuimarishwa upendo na kuondoa aina zote za ubaguzi katika jamii.

Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo, baada ya kushiriki ibada ya Sala ya Ijumaa iliyoambatana na dua maalumu ya kuiombea nchi, viongozi wakuu wa kitaifa na waliotangulia mbele ya haki.

Amesema umoja, mshikamano wa wananchi ni nguzo muhimu ya kudumisha utulivu wa taifa na kila mmoja ana wajibu wa kuchangia kwa vitendo kulinda misingi hiyo.

Dua hiyo iliandaliwa na Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Juma Malik Akil, imefanyika katika Msikiti wa Mzee Ali Hassan Mwinyi uliopo Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi aliwataka waumini kujiepusha kujiingiza katika makundi yenye viashiria vya migawanyiko au chuki, akisisitiza dini inahimiza amani, uvumilivu na kuheshimiana miongoni mwa wananchi.

Ameeleza mafanikio ya kudumisha amani na utulivu nchini, hususan kipindi cha uchaguzi uliopita, ni kielelezo cha nguvu ya umoja na mshikamano uliopo miongoni mwa wananchi, ambapo hali ya utulivu ilidumu katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi kutokana na ushirikiano na uelewano huo.

Aidha, amesema ni wajibu wa kila muumini kuwaombea wazee, ndugu na jamaa waliotangulia mbele ya haki, akieleza miongoni mwa mambo yenye manufaa kwa marehemu ni dua za wale waliobaki hai.

Dua hiyo ilihudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mariam Mwinyi, viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, viongozi wa dini, ndugu, jamaa na marafiki.

Katika hatua nyingine, Rais Dk. Mwinyi, akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa serikali na waumini, walizuru kaburi la Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kumwombea dua maalumu.

Previous Post

UTEUZI WA PROFESA KABUDI GUMZO NCHINI

Next Post

MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

Next Post
MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

MCHENGERWA ASHUSHA MAAGIZO KWA WAGANGA WAKUU WA MIKOA, WILAYA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

RAIS DK. SAMIA AWAFUNDA MAJAJI ALIOWAAPISHA

RAIS DK. SAMIA AWAFUNDA MAJAJI ALIOWAAPISHA

4 weeks ago
UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

UCHAGUZI WA WAJUMBE EALA WAANZA RASMI

2 months ago

Popular News

  • YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE

    YANGA, AZAM FC HAIJAISHA HADI IISHE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA MIAKA 30 TRA, YAGUSA WABUNGE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • HATUTAVUMILIA UHUJUMU WA MIRADI – NDEJEMBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA KUZINDUA JENGO LA BILIONI 17/- KCMC

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BODABODA WAKINGIWA KIFUA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?