Na MWANDISHI WETU
WAAMUZI wanne wa Tanzania wameteuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (CAF), kuchezesha mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFC) kati ya ASCK ya Togo na RS Berkane kutoka Morocco.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), waamuzi hao ni Ahmed Arajiga, Mohamed Mkono, Kassim Mpanga na Ramadhan Kayoko.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Septemba 21 mwaka huu katika Uwanja wa Kegue de Lome nchini Togo.