• ePaper
Sunday, May 31, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

DK. SAMIA AMELETA MIRADI MIKUBWA LINDI – MAJALIWA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 7, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA AMELETA MIRADI MIKUBWA LINDI – MAJALIWA

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

0
SHARES
5
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amezindua kampeni za ubunge wa Jimbo la Mchinga zilizofanyika katika Kijiji cha Rutamba, mkoani Lindi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Majaliwa amesema Ilani ya chaguzi ya mwaka 2025/2030 imejielekeza kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kote nchini ikiwemo katika jimbo hilo.

“Katika kipindi kilichoisha Rais Dk. Samia ameleta hapa miradi mikubwa, ya kati na midogo, anafanya hivi kwa kutambua wananchi wanapaswa kuhudumiwa, hata ilani hii imeonesha maeneo mengine yatakayotekelezwa katika mkoa huu wa Lindi,” amesema.

Amesema wana-Lindi wanapaswa kumchagua mgombea urais kupitia CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan aendelee kutekeleza miradi ya gesi, bandari ya uvuvi Kilwa, ujenzi mpya wa barabara ya Dar es Salaam-Lindi, kuboresha uwanja wa ndege wa Lindi, ujenzi wa reli ya kanda ya kusini na kuunganisha mkoa huo katika gridi ya taifa upate umeme wa uhakika.

Amesema Rais Dk. Samia amepeleka mabilioni ya fedha kutekeleza miradi ya maendeleo mkoani Lindi, na Ilani ya chaguzi ya 2025/2030 imeendelea kusheheni miradi ambayo itatekelezwa mkoani humo, hivyo ni sababu kubwa kwa wananchi kumchagua Dk. Samia aendelee kuongoza.

“Ilani ya uchaguzi imeonesha kutaanza kujengwa kwa kiwango cha lami barabara ya Ngongo-Ng’apa, Mandawa hadi Chikundi, barabara hii itakuwa mkombozi kwa wakazi wa maeneo haya na itafungua uchumi kwa wana-Lindi,” ameeleza.

Majaliwa ameongeza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, jimbo hilo limefanikiwa kuwa na magari ya wagonjwa manne pamoja na ujenzi wa vituo vya afya na zahanati ambazo zimesaidia kuboresha huduma za afya.

“Mheshimiwa Salma Kikwete amejikita katika kuwahudumia wananchi, kwa namna jimbo hili lilivyokaa linahitaj mtu mahiri na mwenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wake, hakika mheshimiwa Salma ameonesha ameweza, mchagueni tena,” alisema.

Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo, Salma Kikwete alisema katika katika kipindi chake amefanikiwa kushirikiana na wana-Mchinga kutafuta majibu ya changamoto za jimbo hilo.

“Tumepata mafanikio makubwa katika kukabiliana na changamoto zetu, hali ilivyo leo (jana) siyo sawa na tulikotoka, tumepata mafaniko sekta ya afya, nishati, elimu, maji, miundombinu na uwezeshaji wananchi kiuchumi, nikipata ridhaa tena tutafanya makubwa zaidi,” aliahidi.

Alisema kwa kipindi cha miaka mitano amefanikiwa kutekeleza mradi wa maji kutoka Ng’apa ambao utawezesha kuvifikia vijiji vingi vya imbo la Mchinga.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete alisema Rais Dk. Samia ameonesha anatosha katika nafasi ya urais, kwa kuwa katika kipindi kifupi amefanya mambo mengi, hivyo anastahili kupewa tena nafasi aendelee kuongoza.

“Alipata urais katika wakati ambao hakutarajia, lakini amefanya kazi nzuri, tutanufaika maradufu, tukimpa nafasi, nimeangalia orodha ya mambo yaliyo katika ilani kwa hakika amejipanga,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wagombea ubunge mkoa wa Lindi, mgombea ubunge Jimbo la Mtama, Nape Nnauye alisema wananchi wa kusini watamchagua Dk. Samia kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwa mkoa huo ukiwemo utoaji ruzuku ya pembejeo za kilimo.

Previous Post

DK. SAMIA AKOSHWA NA MAELFU YA WANANCHI WALIOJITOKEZA UWANJA WA SAMORA

Next Post

KOCHA TAIFA STARS UHAKIKA KWA NIGER

Next Post
KOCHA TAIFA STARS UHAKIKA KWA NIGER

KOCHA TAIFA STARS UHAKIKA KWA NIGER

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

TANZANIA YAJINADI KIMATAIFA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

1 month ago
‘POLICE SERVICE’ GUMZO

‘POLICE SERVICE’ GUMZO

5 months ago

Popular News

  • SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    SERENGETI BOYS KILA KONA, RAIS SAMIA AWAPA MILIONI 500/-

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAS: UTUNZAJI MAZINGIRA AJENDA YA KIPAUMBELE KWA MKOA WA MWANZA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • UPELE UMEPATA MKUNAJI STARS

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ‎ RAIS DK. SAMIA: POLISI MSIDHARAU TAARIFA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWIGULU ATETA NA WAZIRI MKUU WA CONGO BRAZZAVILLE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?