• ePaper
Wednesday, October 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. SAMIA : KASI YA MAENDELEO HAITASINANA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 11, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA : KASI YA MAENDELEO HAITASINANA
0
SHARES
1
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

TABORA

MWENDO ni uleule, huo ndiyo msisitizo wa Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan alipowahakikishia Watanzania pindi atakapopewa ridhaa ya kuendelea kuliongoza Taifa, kasi ya maendeleo haitosimama.

Dk. Samia, amesema serikali yake, haitopunguza kasi ya kuhudumia wananchi katika sekta za maendeleo ya jamii kama elimu, afya, umeme na maji.

Amesisitiza kuwa, katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Serikali ya CCM, itakwenda kutekeleza miradi ya sekta hizo kwa kishindo, lengo ni kulinda utu na heshima ya Mtanzania.

Akizungumza na maelfu ya wananchi katika mkutano wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu zilizofanyika Kata ya Ilolanguru, wilayani Uyui mkoani Tabora jana, Dk. Samia, alisema mahitaji ya huduma hizo kwa wananchi, yameongezeka.

“Katika sekta za maendeleo ya jamii, elimu, afya, umeme na maji, serikali itakwenda na mwendo uleule kwa sababu, tunajua jinsi watu wetu wanavyokuwa na mahitaji yanaongezeka. 

“Katika maji, kadri tunavyoongezeka, mahitaji nayo yanaongezeka. Afya na elimu ni vivyo hivyo. Tutaendelea kujenga madarasa…tutajenga vyuo vya VETA, kuwapa vijana wetu ujuzi wa fani mbalimbali.

“Kubwa zaidi, tunakusudia kuweka viwanda vidogo, ambavyo vitawafanya vijana wetu waongeze thamani kwa kuchakata mazao yanayozalishwa wilayani, kutengeneza ajira kwa vijana,” alibainisha.

UYUI YANEEMEKA SEKTA YA ELIMU

Akizungumzia maendeleo katika elimu wilayani Uyui, Dk. Samia, alisema serikali imetekeleza ahadi ya kuongeza idadi ya walimu.

“Ninafurahi tumeajiri walimu 412, ambao wameletwa ndani ya wilaya hii. Na watumishi wa afya 161. Tunapoendelea mbele, najua bado mahitaji ya watumishi yapo.

“Niliahidi ndani ya siku 100 mtakaponipa ridhaa kuendelea kuongoza nchi hii, tutaajiri katika sekta ya afya watumishi 5,000, bila shaka watafika na Uyui,” alieleza.

Pia, alisema kuwa, katika siku hizo 100, serikali yake, itaajiri watumishi 7,000 ambapo wilaya hiyo, itanufaika.

Alisema katika sekta ya afya, ndani ya wilaya hiyo, serikali imeleta sh. bilioni 8.2, ambazo zimetumika kujenga vituo vya afya na kuboresha hospitali ya wilaya.

Alisema fedha hizo, zimetumika kujenga vituo vya afya sita na zahanati mpya 17.

Dk. Samia, alisema serikali imeleta magari matatu ya kuhudumia wagonjwa, ambayo yanaendelea kufanyakazi kuhudumia wananchi.

“Nafahamu wilaya ni kubwa, hivyo mahitaji ya ujenzi wa vituo vya afya na zahanati bado yapo. Tumejielekeza kusaidia pale ambapo nguvu za wananchi zimeanza na serikali itakuja kumalizia,” alieleza.

Kuhusu sekta ya elimu, alieleza kuwa, serikali imeongeza shule saba za sekondari kufikia 34 kutoka 27 za awali.

Pia, alisema idadi ya wanafunzi, imeongezeka kutoka 12,000 hadi 17,500.

Alisema serikali imeongeza shule za msingi 28 kutoka 124 hadi 182 na kuendelea kutoa elimu bila malipo, kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.

“Tumejenga madarasa ya chekechea. Hii ni programu maalumu ya maendeleo ya mtoto, tunaweka madarasa haya kwa sababu, mama na baba zao, hawakuanza shule mapema,” alisema.

Alieleza kuwa, hiyo ndiyo sababu kwa shule mpya zinazojengwa nchini, yamejengwa madarasa ya chekechea watoto waanze kukuza akili zao mapema.

Alisema serikali imetekeleza programu za kuimarisha sekta za kilimo na mifugo.

“Tumejenga skimu za umwagiliaji, zikiwemo Goweko, Unyanyama na kuendelea kutoa ruzuku ya mbolea, mbegu na dawa za chanjo kwa wafugaji.

“Tunapoendelea mbele, tutaendelea na ujenzi wa majosho na mabwawa ya mifugo,” alibainisha.

Kuhusu sekta ya maji, alisema wilaya hiyo, kulikuwa na miradi 15 ambayo imeongeza upatikanaji maji hadi asilimia 67.

Hata hivyo, alisema bado kuna baadhi ya maeneo ambayo hayajapata maji, ila kupitia mradi wa Ziwa Victoria serikali itajenga tanki kubwa la lita milioni moja katika Kata ya Ilolanguru.

Alisema ujenzi wa tanki hilo, litahudumia wananchi wa Ilolanguru pamoja na Kata za Kalola, Isila, Ndono na Mabana.

Pia, alisema ipo miradi ya maji Kigwa, Kizengi na bwawa la Igombe ambayo imefikia hatua mbalimbali za utekelezaji wake.

“Ahadi yangu kwenu ni kuimarisha miradi hiyo ili wananchi wa maeneo hayo waweze kupata maji safi na salama.

“Mwaka 2022 nilipokuwa hapa mlinieleza kuhusu uhitaji wa daraja la Mto Roya, sasa nataka niwajulishe tumekamilisha usanifu, michoro na gharama ya daraja hilo.

“Tumetenga fedha ndani ya mwaka huu wa fedha kwa hiyo tunatafuta mkandarasi daraja lianze kujengwa. Tutakapojenga tutasaidia wananchi kuvuka kwa raha wakati wa masika,” alisema.

Akizungumzia madeni ya wakulima wa tumbaku, alianza kuwapongeza kwa kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

Alisema kupitia mbolea na pembejeo za ruzuku wameongeza uzalishaji wa tumbaku hivyo kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazouza tumbaku nyingi duniani.

Aliwahakikishia wakulima kwamba, serikali bado ipo katika mazungumzo na kampuni za PCL na Volecel ambazo hazijalipa fedha za wakulima.

“Niwahakikishie zitalipwa, kupitia Waziri wa Kilimo, huwa ninataka ripoti kila baada ya muda aniambie mazungumzo yamefikia wapi ili wakulima walipwe fedha zao,”alisema.

Pia, alisema serikali imeendelea kufanyakazi kubwa katika kuhakikisha barabara za vijijini, zinaboreshwa kwa kiwango cha changarawe, zipitike mwaka mzima.

Alitaja maeneo ambayo barabara za wilaya hizo zitakwenda kuboreshwa ni Ilolanghulu – Isenga – Kasisi A na Ndono – Fuluma – Makazi.

AHUTUBIA MAELFU KALIUA NA URAMBO

Katika mkutano mwingine uliofanyika wilayani Kaliua, Dk. Samia, alisema serikali ya CCM ni sikivu kwa wananchi.

“Ili tuweze kuyafanyia kazi, ninawaomba sana Wanakaliua kila aliyejiandikisha katika daftari la kupigakura, tutoke kwa wingi tukakipigie kura Chama Cha Mapinduzi ili tuweze kutekeleza haya mnayotaka.

“Kwa upande wetu, hatuna wasiwasi kuyatekeleza kwa sababu, tulishatoa mfano miaka mitano iliyopita, tumetekeleza mmeona na mbele hapo tutakwenda kutekeleza ili kuinua utu na heshima ya Mtanzania,”alisema.

Katika mkutano wake uliofanyika wilayani Urambo, Dk. Samia alisema kwa mara ya kwanza Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kupitia CCM umetoa mgombea Urais.

“Kwa mara ya kwanza katika nchi yetu miaka yote, wagombea Urais wanatokea jumuiya ya umoja wa vijana na jumuiya ya wazazi. Maana yake wanaume wanakuwa umoja wa vijana hadi umoja wa wazazi.

“UWT haikuwahi kutoa mgombea Urais, huu ni mwaka wa kwanza ni mara ya kwanza kwa UWT kutoa mgombea Urais kwanini nasema hivyo? Kinamama muungane kuanzia sasa, kitenge kiunoni na kiatu mguuni twende tukasake kura za mgombea wetu wa Urais,”alisema.

Previous Post

TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

Next Post

DK. MWINYI AFUNGUKA MALENGO SERA YA NISHATI

Next Post
DK. MWINYI AFUNGUKA MALENGO SERA YA NISHATI

DK. MWINYI AFUNGUKA MALENGO SERA YA NISHATI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

WASIRI : CCM INAFANYA KAZI KUBWA YA KULETA MAENDELEO

WASIRI : CCM INAFANYA KAZI KUBWA YA KULETA MAENDELEO

4 weeks ago
KIHONGOSI AWATAKA VIJANA KUTOKUBALI KUVURUGA AMANI

KIHONGOSI AWATAKA VIJANA KUTOKUBALI KUVURUGA AMANI

4 days ago

Popular News

  • SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    SIMBA NI MWENDO WA MABAO LIGI KUU

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JESCA: DK. SAMIA NI KIONGOZI JASIRI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAFANIKIO YA WATANZANIA YAKO KATIKA MATENDO – DK. MIGIRO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. SAMIA AAHIDI UCHUMI JUMUISHI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DK. MWINYI AAHIDI KUJENGA HOSPITALI MAALUMU YA SARATANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.