• ePaper
Friday, October 9, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 11, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
TRILIONI 1.7/- ZANUFAISHA MIRADI MKOANI SINGIDA
0
SHARES
23
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Singida

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imepeleka jumla ya sh. trilioni 1.7 za miradi ya maendeleo mkoani Singida tangu mwaka 2021.

Pia, imewezesha wananchi zaidi ya 500,000 kupata msaada wa kisheria kupitia programu ya ‘Mama Samia Legal Aid’ kwa kufuatilia madai yao na kutatua migogoro ya ardhi.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika, Uwanja wa Bombadia, Singida Mjini, Dk. Samia, alisema uwekezaji unaofanyika nchi nzima ni kujali utu wa mtu.

“CCM inaweka ilani yake, kuweka uwekezaji kwa kutumia fedha nyingi kama zinavyotajwa, kujali na kuinua utu wa mtu. Tunataka kila Mtanzania tujali utu wake.

Alisisitiza: “Tujali afya yake, tujali elimu yake, tujali usalama wake, tujali kila kitu kinachomgusa Mtanzania hata uchumi na ustawi wake.”

Alisema yote yanayofanyika ni katika kujali utu wa Mtanzania, hivyo aliwaomba Watanzania kuipa ridhaa CCM ili kikafanye makubwa zaidi yanayomjali Mtanzania.

Akizungumzia maendeleo katika mkoa huo, alisema serikali imejenga hospitali nne, vituo vya afya 22 na zahanati 63 lengo ni kusogeza huduma kwa wananchi.

“Najua kuna upungufu wa wafanyakazi, lakini nimeahidi tutakapoingia madarakani mkitupa ridhaa siku 100 za kwanza, tunakwenda kuajiri wafanyakazi wengi katika sekta ya afya na elimu.

“Katika suala la maji, tumepandisha asilimia ya upatikanaji maji, bado mradi wa maji miji 28 unatekelezwa Singida Mjini, Manyoni na Kiomboi.

“Mradi mkubwa utakaomaliza kero ya maji ni ule utakaotoa maji Ziwa Victoria kupita Singida kwenda Dodoma ambao tunaoufanyiakazi na dhamira yetu mkitupa ridhaa tuufanyiekazi kweli kweli ili uje kuondosha kero ya maji,”alisema.

Previous Post

‘MIFUMO YA UUZAJI MAZAO YA WAKULIMA, WAIMARISHWA’

Next Post

DK. SAMIA : KASI YA MAENDELEO HAITASINANA

Next Post
DK. SAMIA : KASI YA MAENDELEO HAITASINANA

DK. SAMIA : KASI YA MAENDELEO HAITASINANA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. NCHIMBI ATOA  AHADI KWA  DK. SAMIA

DK. NCHIMBI ATOA AHADI KWA DK. SAMIA

1 year ago
MTWARA KUCHELE! NCHIMBI AAHIDI MAMBO MAKUBWA

MTWARA KUCHELE! NCHIMBI AAHIDI MAMBO MAKUBWA

1 year ago

Popular News

  • WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    WABUNGE AFRIKA WAUNGA MKONO AJENDA YA RAIS DK. SAMIA YA AFYA YA MAMA NA MTOTO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • BRITISH AIRWAYS KUREJEA TANZANIA, KUANZA SAFARI MEI 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA AICHIMBA YANGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMULIZI MKASA WA MWANAMKE ANAYEDAIWA KUUAWA KWA RISASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TPA YAELEZA SIRI UTOAJI HUDUMA BORA BANDARINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Not enough quota to unlock this post
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?