• ePaper
Wednesday, March 18, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

SUMAYE: DK. SAMIA NDIYE KIONGOZI MWENYE UPEO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 6, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
SUMAYE: DK. SAMIA NDIYE KIONGOZI MWENYE UPEO

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye

0
SHARES
4
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH

WAZIRI Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, amesema Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye upeo wa juu na uvumilivu wa kisiasa.

Sumaye, ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Mjini Babati mkoani Manyara, alisema wapinzani wanatamani kianguke jambo ambalo halitowezekana.

“Rais Samia ni mvumilivu. Huyu mama (Dk. Samia) ni mvumilivu sana, ninyi ni mashahidi, wanamsemasema kwa mengi, lakini Mheshimiwa Samia nikwambie, anayepigwa vita siyo Samia, inayopigwa vita ni CCM.

“Wanaokichukia Chama hiki hasa kutoka nje ya nchi, miaka yote wametamani CCM ianguke.

“Kwa hiyo, kinachotafutwa ni CCM kuanguka, sasa wanakuta hii CCM haitikisiki, wanaamua kumshambulia mgombea,” alisema.

Alieleza kuwa, wapinzani wa CCM, wamekuwa wakipuuza nguvu ya chama hicho, badala yake wanamlenga mgombea wake, lakini wananchi watatoa majibu sahihi kupitia sanduku la kura Oktoba 29 mwaka huu.

Kwa upande wake, Mbunge mstaafu Jimbo la Simanjiro, Christoper Ole Sendeka, alitoa wito kwa watia nia, waliokosa uteuzi kugombea ubunge katika mchakato wa kura za maoni, kuvunja makundi.

Alieleza kuwa, wanaCCM wanapaswa kuheshimu maamuzi ya vikao vya uteuzi kwa kuwaunga mkono wagombea walioteuliwa kukiwezesha Chama kupata ushindi.
“Nataka niwaambie viongozi wa Mkoa wa Manyara kama kura zako hazikutosha ameteuliwa mwenzako, mimi nimeonesha mfano kuumunga mkono James Milya na kuwa mratibu wa kampeni zake katika Jimbo la Simanjiro,” alisema.

Naye, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Arusha, Cecilia Paresso, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Manyara, kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kuwachagua wagombea wa CCM.

Alitoa wito kwa wananchi, kuwaogopa matapeli wa kisiasa wanaopotosha ukweli kuhusu uchaguzi mkuu kwa sababu, nchi inaongozwa kwa kufuata misingi ya kidemokrasia.

Previous Post

MWINYI AFICHUA SIRI UUNDAJI SERIKALI YA UMOJA KITAIFA

Next Post

MAELFU WAMSUBIRI DK. SAMIA MWANZA

Next Post
MAELFU WAMSUBIRI DK. SAMIA MWANZA

MAELFU WAMSUBIRI DK. SAMIA MWANZA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

UWEKEZAJI NSSF WA MZIZIMA TOWERS KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA NA UTALII DAR

UWEKEZAJI NSSF WA MZIZIMA TOWERS KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA NA UTALII DAR

18 hours ago
TUZO YA CAF KWA RAIS DK. SAMIA NI HESHIMA

TUZO YA CAF KWA RAIS DK. SAMIA NI HESHIMA

4 months ago

Popular News

  • MANDONGA AJA KIVINGINE

    MANDONGA AJA KIVINGINE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YATUMIA BILIONI 64/- KUBORESHA UWANJA WA NDEGE IRINGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AWAWEKA MTEGONI VIGOGO WILAYA, HALMASHAURI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ALAMA TATU KUMUENZI JPM

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA – DK. YONAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?