Na MUSSA YUSUPH,
Geita
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Asha- Rose Migiro, amesisitiza kuwa, mafanikio ya Watanzania, hayapo katika maneno bali ni matendo.
Dk. Migiro, aliyasema hayo katika mkutano wa kampeni, uliohutubiwa na Mgombea Urais kupitia CCM, Dk. Samia Suluhu Hassan, uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Bukombe.
Alieleza kuwa, kwa kipindi kirefu, wananchi wa Bukombe wameshuhudia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika afya, elimu na miundombinu, hatua inayothibitisha CCM ikiahidi inatekeleza.
Alisema Dk. Samia, amefungua fursa kwa vijana na kuleta mageuzi ya kiuchumi, kupitia uwekezaji na ujenzi wa miradi ya kimkakati.
“Amefanya kazi kuhakikisha maendeleo hayapo mijini pekee, bali hata vijijini. Kwa kutambua nguvu kubwa zaidi, inapaswa kuelekezwa vijijini ndipo nguvu kazi kubwa ya wananchi wanaishi.
“Hapo ndipo lengo kuu la Dk. Samia, kuelekeza nguvu kubwa mahali ambako Watanzania wengi, wanapatikana na huo ndiyo utu.
“Tuna kila sababu kusema Oktoba 29 hakuna mbadala ni Samia,” alieleza