• ePaper
Friday, November 14, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Habari

DK. SAMIA AWAPA KICHEKO KARAGWE

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
October 16, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
DK. SAMIA AWAPA KICHEKO KARAGWE

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MUSSA YUSUPH,

Karagwe

MGOMBEA Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ameyataja maeneo makuu matatu ambayo serikali yake, itajikita katika kuhudumia wananchi kama ilivyoelekezwa kupitia Ilani ya Uchaguzi (2025 – 2030).

Dk. Samia ameyataja maeneo hayo ni kusogeza huduma za kijamii, uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuimarisha sekta za uzalishaji (kilimo, viwanda na miundombinu).

Akizungumza na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kayanga wilayani Karagwe mkoani Kagera, Dk. Samia, alisema maeneo hayo matatu ndiyo msingi wa maendeleo kwa wananchi.

HUDUMA ZA KIJAMII

Alisema serikali yake, pindi itakapopewa ridhaa ya kuliongoza taifa, itaongeza kasi kusogeza huduma za afya, maji, elimu na umeme kwa wananchi.

“Katika afya, tutandelea kujenga vituo vya afya, zahanati na kukamilisha hospitali za wilaya kule ambako hatujamalizia. Tutaendelea kutoa huduma za dawa, vifaatiba na vitendeakazi vyote,” alieleza.

Kuhusu elimu, alisema serikali itaendelea kujenga miundombinu ya elimu na vyuo vya ufundi, kuwawezesha vijana kujiajiri au kuajiriwa.

“Kwa nini tunajenga VETA, kwa sababu, tunaangalia mbele nchi yetu viwanda vinakuja, uwekezaji unakuja, miradi mikubwa kama bomba la mafuta inahitaji wafanyakazi. 

“Tunamalizia mazungumzo, mradi mkubwa wa Mchuchuma na Liganga kuchimba chuma na makaa ya mawe, tunataka mafundi na watu wa fani mbalimbali. Maendeleo ya bandari zetu, reli tunazozijenga zote zinataka mafundi wa aina mbalimbali,” alisisitiza.

Pia, alisema serikali imeendelea kutoa fedha kugharimia miradi ya maji na kujenga skimu za umwagiliaji, wakulima wazalishe mazao yao mara mbili kwa mwaka.

Vilevile, alieleza kuwa serikali imejidhatiti kutatua kadhia ya umeme kwa kupeleka nishati hiyo vijiji vyote.

Alisema nishati hiyo, imewawezesha vijana kufanya shughuli zao saa 24 badala ya saa 12 wakati umeme ulipokuwa haupatikani.

UWEZESHAJI WANANCHI

Katika eneo hilo la pili, Dk. Samia, alisema tayari serikali imetoa ruzuku kwa wakulima hatua ambayo imeongeza uzalishaji mazao na ongezeko la mapato.

“Kama ruzuku isingetolewa, wakulima wangewajibika kutoa fedha kununua mbolea. Wasingeweza kununua mbolea nyingi, wangenunua kidogo, wangetumia shambani kidogo na mazao yangekuwa kidogo.

“Kwa sababu tunawatoza nusu bei wanapata mbolea nyingi, wanavuna mazao mengi, wanauza mazao mengi na wanapata pesa nyingi,” alieleza.

Pia, alisema serikali itaendelea kuwawezesha wananchi kupitia miradi ya TASAF, utoaji mikopo ya asilimia 10 pamoja na kuanzisha mfuko wa wajasiriamali wadogo.

SEKTA YA UZALISHAJI

Katika eneo hilo la tatu, Dk. Samia alisema serikali yake itahakikisha inakwenda kuendelea kujenga barabara kwa kiwango cha lami maeneo mbalimbali nchini.

Pia, alisema katika mkoa huo, serikali itakwenda kujenga uwanja mkubwa wa ndege eneo la Missenyi kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.

Alisema serikali inaendelea kujenga bandari mbili mkoani humo (Bukoba na Kemondo) kuongeza kasi ya uchukuzi.

Akizungumzia viwanda, alisema ilani ya CCM imeelekeza kuweka kongani za viwanda kila wilaya kwa madhumuni ya kuongeza thamani mazao yanayozalishwa katika maeneo hayo.

DK. BASHIRU

Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Balozi Dk. Bashiru Ali, alisema ngome ya CCM ni wananchi kutoka maeneo ya vijijini, ndiyo maana ilani ya CCM imeweka msisitizo wa maendeleo vijijini.

Alisema CCM kinaendelea kuaminika na kuaminiwa katika ngoma yake ambao ni wakulima, wafugaji, wafanyakazi na wachimbaji wadogo.

Dk. Bashiru alieleza leo wananchi wa Mkoa wa Kagera, wamejipanga kuvunja rekodi ya mahudhurio katika mkutano mkubwa wa kampeni utakaofanyika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

WENJE AFUNGUKA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Ezekia Wenje, alisema namna Dk. Samia alivyotekeleza matakwa yaliyowasilishwa na wadau wa vyama vya siasa ikiwemo CHADEMA.

Alieleza kuwa, baada ya Dk. Samia kuingia madarakani, aliwaita wadau wa siasa wakiwemo CHADEMA, kujadiliana namna bora ya kuimarisha demokrasia nchini.

“Mara tu ulipoingia madarakani, ulituita mezani kuja kuzungumza. Tukaja na mahitaji yetu, kwanza tukaomba tuliokimbia nchi utukubalie kurejea bila masharti.

“Tulikuwa na watu wengi waliokamatwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Tulikuomba waliokamatwa baada ya uchaguzi wote waachiwe na uliwaachia. Tulikuomba mikutano ya hadhara ifunguliwe, uliruhusu kufunguliwa, lakini kwa bahati mbaya tukaanza kukutukana,”alisema.


ONGEZEKO BEI YA KAHAWA

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge Jimbo la Nzega Mjini na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, alisema miaka minne iliyopita bei ya kahawa ilikuwa kati ya sh. 700 hadi 1,200.

Alisema mbali na bei hiyo, pia mkulima alikuwa akikatwa makato zaidi ya 40, suala ambalo serikali ikaamua kuchukua hatua.

Bashe, alisema serikali ikaamua kubadilisha mfumo wa uuzaji, kisha kufuta tozo zote hatua ambayo imeboresha zao hilo ikiwemo ongezeko la bei.

UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

Mgombea Ubunge Jimbo la Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, alisema kabla ya Dk. Samia kuingia madarakani, kulikuwa na ahadi ya miradi miwili ya maji katika mkoa huo.

Alisema Dk. Samia alitoa sh. bilioni 300 kuimarisha upatikanaji maji hatua ambayo imewezesha kiwango cha upatikanaji maji kutoka asilimia 59 hadi asilimia 79.

UKIANDAMANA UTAKUMBANA NA KISIKI

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, alieleza kuwa, tangu alipopewa dhamana ya kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara kudumisha amani.

Alisema atakayethubutu kuandamana Oktoba 29 mwaka huu, atakumbana na kisiki, alitoa wito kwa vijana kuendelea kudumisha amani na kujenga nchi.

WAGOMBEA UBUNGE

Mgombea Ubunge Jimbo la Kyerwa, Khalid Nsekela, alisema zaidi ya sh. bilioni 84, zimetolewa katika jimbo hilo, kugharimia miradi ya maendeleo, ikiwemo ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.

Alisema wananchi wa jimbo hilo, wanamshukuru Dk. Samia kwa kupaisha bei ya kahawa kutoka sh. 1,000 kwa kilo hadi zaidi ya sh. 5,000 kwa kilo moja.

Naye, Mgombea Ubunge Jimbo la Ngara, Dotto Bahemu, alisema wananchi wa eneo lake, wanajitambua kumchagua kiongozi aliyewathibitishia kwa vitendo utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Alisema Dk. Samia ametoa sh. bilioni 81 kutekeleza miradi ya maendeleo, akitolea mfano ujenzi wa hospitali ya wilaya, ambayo itakuwa ya pili katika jimbo hilo.

Previous Post

STEVEN WASIRA: TAIFA HILI HALIJAWAHI KUGAWANYIKA

Next Post

PANTEV KICHEKO SIMBASC

Next Post
PANTEV KICHEKO SIMBASC

PANTEV KICHEKO SIMBASC

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. SAMIA AVUNJA NGOME YA UPINZANI MKOANI LINDI

DK. SAMIA AVUNJA NGOME YA UPINZANI MKOANI LINDI

2 months ago
CCM YATAJA SABABU MBILI KUOMBA KURA SONGWE

CCM YATAJA SABABU MBILI KUOMBA KURA SONGWE

2 months ago

Popular News

  • DK. MWIGULU ATUMA SALAMU KWA WALA RUSHWA, WAZEMBE

    DK. MWIGULU ATUMA SALAMU KWA WALA RUSHWA, WAZEMBE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NYOTA TAIFA STARS  MZUKA UMEPANDA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RONALDO KUTUNDIKA DALUGA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • JINA LA WAZIRI MKUU MTEULE KUWASILISHWA BUNGENI LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWAKINYO KUPANDA ULINGONI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.