• ePaper
Tuesday, May 26, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MANZESE, VINGUNGUTI, BUGURUNI KUISHI ‘KISHUA’

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
December 9, 2025
in Habari, Kitaifa
0
MANZESE, VINGUNGUTI, BUGURUNI KUISHI ‘KISHUA’

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo

0
SHARES
15
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na ELIZABETH JOHN

SERIKALI imejipanga kuhuisha majengo na kupanga upya miji mikubwa, hatua inayolenga kuongeza thamani ya makazi, kuboresha matumizi ya ardhi na kuvutia uwekezaji katika kipindi cha pili cha miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, alisema mpango huo utahusisha ubia kati ya wananchi na sekta binafsi; kubomoa nyumba chakavu, kujenga majengo mapya ya ghorofa na kuwapa wakazi sehemu za makazi na biashara ndani ya miradi hiyo.

MAENEO WATAKAYOULA

Akizungumza na wanahabari, Profesa Mkumbo alisema maeneo matatu ya kuanzia ni Vingunguti, Buguruni na Manzese kwa mkoa wa Dar es Salaam huku mchakato wa kuwavutia wawekezaji ukitangazwa rasmi.

Profesa Mkumbo aliwahikishia wananchi kunufaika moja kwa moja kupitia mfumo wa kupata nafasi kwenye ghorofa za makazi na biashara katika majengo mapya.

Waziri Mkumbo alisema mageuzi ya miji ni sehemu ya mkakati mpana wa kufungua fursa za uchumi, kuongeza ajira na kuboresha ubora wa maisha katika maeneo ya mijini.

Alieleza kuwa matumaini ya serikali ni kuona miji ya Dar es Salaam na baadaye mingine nchini ikiwa na makazi yaliyopangwa vizuri na miundombinu ya kisasa.

Alisema serikali inaelekeza nguvu katika kufungua maeneo mapya ya utalii tofauti na yale yanayofahamika kama Ukanda wa Kaskazini, huku akitaja Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kama moja ya maeneo makubwa yenye uzuri wa kipekee, lakini ambayo hayajafunguliwa kikamilifu. Pia alieleza kuwa utalii wa fukwe haujatumiwa ipasavyo licha ya Tanzania kuwa na mwambao mrefu uliojaa vivutio.

Profesa Mkumbo alisema serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi ya ndani na nje kuongeza uwekezaji katika utalii, ujenzi na miundombinu, hatua itakayochochea ukuaji wa mapato ya taifa na kupanua ajira kwa vijana.

FURSA MPYA KWA VIJANA

Pia, vipaumbele na fursa mpya kwa vijana katika uwekezaji na ajira ndani ya miaka mitano ijayo vimetajwa kuwa miongoni mwa nguzo kuu zitakazotekelezwa na serikali katika kuimarisha uchumi wa Taifa kuelekea Dira 2050.

Waziri Mkumbo, alisema juhudi hizo zitajikita katika kuongeza miradi ya uwekezaji, kupanua maeneo ya kiuchumi na kufungua njia kwa vijana kuingia katika sekta za viwanda, kilimo na teknolojia.

Alisema ofisi hiyo iliyoanzishwa Julai 2023, ina jukumu la kuratibu uandaaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa pamoja na kuisimamia Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi (TISEZA).

Alisema mkazo mkubwa kwa sasa umewekwa katika kubuni fursa mpya zitakazopunguza changamoto ya ajira kwa vijana nchini.

Kuhusu mwenendo wa uwekezaji katika miaka ya karibuni, alisema mafanikio hupimwa kwa kuangalia idadi ya miradi iliyosajiliwa, ajira zinazozalishwa na mtaji unaovutwa.

“Kwa kipindi cha 2021 hadi 2025, miradi hiyo imeongezeka kutoka 252 hadi kufikia 901 kwa mwaka, huku mtaji ukipanda kutoka Dola bilioni 3.7 mwaka 2021 hadi Dola bilioni 9.3 mwaka 2024.

“Kwa miaka mitano ijayo, serikali inaelekeza nguvu katika kuimarisha Kituo cha Mahala Pamoja chenye taasisi 14 kupunguza urasimu kwa wawekezaji.Kituo hicho kitaendelea kutoa huduma za usajili wa makampuni, vibali vya kazi, vibali vya ukaazi, taratibu za ardhi, uchukuaji wa vyeti vya ubora, taratibu za umeme na vivutio vya kikodi,” alisema.

Alisema kuanzia Januari 2026, serikali itaanzisha Jukwaa la Kitaifa la Uwekezaji litakalokutanisha mawaziri wa sekta husika na wawekezaji ili kujadiliana changamoto, kufanya tathmini ya maendeleo na kuboresha mazingira ya uwekezaji. Jukwaa hilo litakuwa chanzo cha maamuzi ya haraka kuhusu utekelezaji wa sera.

Kwa mujibu wa Waziri Mkumbo,  katika kipindi hicho, uteuzi wa miradi ya uwekezaji utafanyika kwa kuzingatia vigezo vitano, uwezo wa kuzalisha ajira, kuongeza mauzo nje, kuchochea sekta nyingine, kuongeza thamani ya bidhaa na kuongeza mapato ya serikali.

“Maeneo 10 yamepewa kipaumbele, ikiwemo kilimo na uchakataji, uzalishaji wa bidhaa muhimu kama mafuta ya kupikia na ngano, ufugaji, uvuvi, utalii, ujenzi wa majengo, madini, misitu, nishati na huduma za fedha.

“Kwa upande wa vijana, serikali imeandaa mpango mahsusi unaojumuisha kuanzishwa kwa kituo maalum cha kuwezesha wawekezaji vijana (Youth Investors Resource Centre) na programu ya vijana kuanzisha viwanda. Kupitia mpango huo, vijana watapewa ardhi, kuunganishwa na wauzaji wa mitambo, wazalishaji wa malighafi na taasisi za fedha kama CRDB, TCB na Benki ya Azania,” alisema.

Alisema Maeneo maalumu yametengwa kwa ajili ya uwekezaji wa vijana, yakiwemo Dodoma (Nala, ekari 100), Pwani (Kwala, ekari 20), Mara (Bunda, ekari 100), Ruvuma (Songea, ekari 100) na Bagamoyo (ekari 20), hiyo inalenga kuongeza idadi ya vijana wanaojihusisha na uundaji wa viwanda vidogo na vya kati.

Alisistiza kuwa, serikali inakusudia kusogeza huduma za uwekezaji katika kila mkoa ifikapo mwaka 2028 kupunguza umbali na gharama za kupata huduma za TISEZA.

“Kwa kushirikiana na sekta binafsi, kutajengwa ‘industry shades’ za kukodishwa kwa gharama nafuu ili kutoa fursa kwa Watanzania walio wengi kuingia katika mnyororo wa thamani wa viwanda.

“Katika kuboresha mazingira ya biashara, maandalizi ya MKUMBI II yanaendelea na utazinduliwa kabla ya Julai 2026. Mkakati huo utakuwa sehemu ya utekelezaji wa Dira 2050 na utaweka mazingira rafiki zaidi kwa wawekezaji wa ndani na nje,” alisema.

Kwa upande wa mipango ya maendeleo ya Taifa, NPC inaendelea kuandaa Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP I – Dira 2050), Mpango wa Maendeleo wa Mwaka Mmoja wa 2026/27, pamoja na mfumo mpya wa ufuatiliaji na upimaji wa matokeo (RBMELA Framework).

Profesa Mkumbo alisema katika upande wa mashirika ya umma, muswada mpya wa sheria ya uwekezaji wa umma uko hatua za mwisho kukamilika. Sheria hiyo itasisitiza tija ya kiuchumi, uwazi wa usimamizi, ushiriki wa Watanzania katika umiliki kupitia soko la hisa na uanzishwaji wa chanzo maalumu cha fedha kwa ajili ya uwekezaji wa umma.

Alisisitiza kuwa ifikapo mwaka 2030, serikali inatarajia kuona ongezeko la miradi ya uwekezaji, kupanuka kwa fursa za ajira na kuvutia mtaji wa angalau dola za Marekani bilioni 50.

Aidha, alisema kila wizara na taasisi zitaonekana katika mwelekeo mpya wa ufuatiliaji kwa kutumia viashiria vya matokeo.

Aliongeza kuwa, serikali ya Awamu ya Sita inaamini mageuzi haya yataimarisha utendaji wa mashirika ya umma, kuboresha huduma kwa wananchi na kujenga msingi wa uchumi shindani unaowezesha vijana na Watanzania wote kujipatia kipato kupitia miradi ya uwekezaji. 

Previous Post

RAIS DK. SAMIA AWATAKIA HERI WATANZANIA MIAKA 64 YA UHURU

Next Post

CHAMBUA: DUBE KAMA MAYELE

Next Post
CHAMBUA: DUBE KAMA MAYELE

CHAMBUA: DUBE KAMA MAYELE

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWINYI ATANGAZA NEEMA WAZEE ZANZIBAR

DK. MWINYI ATANGAZA NEEMA WAZEE ZANZIBAR

8 months ago
SITAWAANGUSHA

SITAWAANGUSHA

1 month ago

Popular News

  • NEEMA YA AJIRA MAMBO YA NDANI

    NEEMA YA AJIRA MAMBO YA NDANI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SIMBA ACHEFUKWA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KOCHA SERENGETI BOYS AFUNGUKA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MWIGULU AKERWA WANAOPORA HAKI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TUCTA YATAKA WAANDISHI KUHAMASISHA WAAJIRI KURIPOTI MATUKIO WCF

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?