• ePaper
Saturday, November 15, 2025
Subscribe
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
No Result
View All Result
Home Burudani

RONALDO KUTUNDIKA DALUGA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
November 12, 2025
in Burudani, Kimataifa, Michezo
0
RONALDO KUTUNDIKA DALUGA
0
SHARES
3
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RIYADH, Saudi Arabia

STAA Cristiano Ronaldo, amethibitisha kwamba atastaafu kucheza soka baada ya kumalizika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026.

Mkongwe huyo raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 40, amesema anatarajia kustaafu soka baada ya mwaka mmoja au miwili ijayo.

Msimu ujao wa michuano ya Kombe la Dunia, unatarajiwa kufanyika katika nchi za Canada, Mexico na Marekani ambapo Ronaldo utakuwa msimu wake wa sita.

Amesisitiza michuano ya Kombe la Dunia msimu ujao ndiyo itakuwa mara yake ya mwisho kushiriki, hivyo atastaafu na kuwaachia vijana kuendelea pale atakapoishia.

“Baada ya kumalizika msimu ujao wa Kombe la Dunia nitakuwa nimeshafikisha miaka 41, hivyo nitalazimika kustaafu kucheza soka.

“Michuano  ijayo ya Kombe la Dunia ninatarajia itakuwa na ushindani mkubwa, baada ya hapo nitastaafu kucheza soka na kuwaachia vijana waendelee pale nitakapoishia,” alisema.

Ronaldo anayeichezea Al-Nassr ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia, ameshafunga mabao 143 katika timu yake ya taifa ya Ureno.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na Juventus alisisitiza baada ya kumalizika michuano ya Kombe la Dunia, atatundika daluga na kuendelea kufanya shughuli zingine nje ya soka.

“Acha niwe mkweli, baada ya mwaka mmoja au miwili ijayo nitalazimika kustaafu soka kwani umri wangu utakuwa umefikia hatua hiyo, lakini nitaendela kuwa karibu na mchezo huo kila muda nitakaotakiwa kutoa msaada,” alisema.

Ronaldo alishaisaidia Ureno kubeba Kombe la Euro 2016 na kutwaa mara tano tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d’Or.

Tayari kikosi cha Kocha Roberto Martinez, kimeshafuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia msimu ujao.

Previous Post

MWAKINYO KUPANDA ULINGONI

Next Post

NYOTA TAIFA STARS  MZUKA UMEPANDA

Next Post
NYOTA TAIFA STARS  MZUKA UMEPANDA

NYOTA TAIFA STARS  MZUKA UMEPANDA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

JKT TZ, SIMBA BALAA LIPO HAPA

JKT TZ, SIMBA BALAA LIPO HAPA

1 week ago
BALOZI NCHIMBI AMSIFU DK. SAMIA KUIMARISHA UHUSIANO

BALOZI NCHIMBI AMSIFU DK. SAMIA KUIMARISHA UHUSIANO

2 months ago

Popular News

  • YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    YANGA, SIMBA KAZI KAZI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • KETE YA KWANZA KWA GAMONDI STARS LEO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TRA YAHAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA WA KARIAKOO USALAMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MAAGIZO MATATU KWA DK. NCHEMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • NI MARIDHIANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
error: Content is protected !!
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2025 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.