• ePaper
Sunday, March 8, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

BALOZI NCHIMBI AMSIFU DK. SAMIA KUIMARISHA UHUSIANO

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
September 2, 2025
in Habari, Kitaifa, Siasa, Uchaguzi
0
BALOZI NCHIMBI AMSIFU DK. SAMIA KUIMARISHA UHUSIANO
0
SHARES
0
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na NJUMAI NGOTA,

Itilima

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema Mgombea Urais wa Chama, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameimarisha diplomasia ya kiuchumi na uhusiano mzuri na nchi jirani za kikanda na kimataifa katika miaka minne ya uongozi wake.

Alipoapishwa kuwa Rais Machi 19, 2021, Dk. Samia, aliahidi kulinda umoja, amani, utulivu na amehakikisha nchi inaendelea kuwa nchi moja yenye mshikamano.

Aidha, amewapeleka mabalozi katika nchi mbalimbali, wenye weledi na uzoefu mkubwa kuiwakilisha nchi kimataifa.

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ameyasema hayo eneo la Nyakabindi, wilayani Itilima, mkoani Simiyu, katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Amesema Dk. Samia, katika kipindi cha uongozi wake wa miaka minne, amefanya maendeleo makubwa, hizo ndiyo sababu zinazomfanya aendelee kuaminiwa kutokana na mageuzi makubwa ya maendeleo, aliyofanya sekta mbalimbali, zikiwemo za uchumi.

Balozi Dk. Nchimbi, ametaja baadhi ya sababu hizo ni kutekeleza ahadi ilizozitoa Chama na kuzitekeleza kwa vitendo na kuimarisha amani na mshikamano wa kitaifa

Mgombea huyo amesema Dk. Samia, amekidhi matarajio ya Watanzania, ndiyo maana wanatembea kifua mbele kujivunia alama kubwa za maendeleo zilizofanyika kipindi kifupi cha uongozi wake.

Pia, Dk. Samia, amesimamia miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo ya kumalizia ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere kwa asilimia 100. Alilikuta asilimia 30 na kukamilisha ujenzi wa daraja la Kigongo–Busisi, mkoani Mwanza.

Balozi Nchimbi amesema Dk. Samia, ameboresha afya ya mama na mtoto kwa kujengwa na kuimarishwa vituo vya afya, zahanati na madaktari bingwa wanapatikana kila mkoa.

Kwa mujibu wa mgombea mwenza huyo wa CCM, hivi sasa, mgonjwa halazimiki kusafirishwa kwenda Dar es Salaam na huduma za kitaalamu zinapatikana mikoa yote.

Ameeleza baadhi ya mataifa, yameona matokeo ya mageuzi hayo, hivyo ni wajibu wa Watanzania, kuendelea kumwamini na kumchagua aendeleze kasi ya maendeleo.

MAFANIKIO YA ITILIMA

Balozi Dk. Nchimbi, ametaja baadhi ya mafanikio wilayani Itilima ni pamoja na kuongezeka huduma za jamii, zikiwemo seka za afya, elimu, maji na umeme.

Mafanikio mengine ni hospitali ya wilaya, vituo vya afya vinne, ongezeko la zahanati kutoka 34 hadi 43, shule za msingi kutoka 95 hadi 107 na sekondari kutoka 30 hadi 38.

Amesema hivi sasa, ufaulu wa elimu ya msingi umepanda kutoka asilimia 57 hadi 91 na sekondari kufikia asilimia 97.

ILANI MPYA 2025-2030

Balozi Dk. Nchimbi, ametaja baadhi ya vipaumbele vitakavyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo wilayani humo ni kujengwa vituo vya afya vitatu, shule za msingi 10, sekondari mpya saba na madarasa 102.

Pia, kuimarishwa miradi ya maji, kuanzishwa kilimo cha umwagiliaji na kuboreshwa miundombinu ya barabara na mazingira ya biashara.

UJUMBE WA MPINA

Akiwa Meatu, Dk. Nchimbi, amemtumia ujumbe aliyekuwa Mbunge wa Kisesa, Luhanga Mpina, asipokipigia kura Chama tawala katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu, atakiuka ahadi yake.

Pia, amemshauri arudishe kadi ya ACT-Wazalendo, atakapofanya hivyo, yeye atakamkabidhi kadi ya CCM.

Kabla ya Mpina kuhamia ACT-Wazalendo, aliwahi kuwaambia wananchi wa Kisesa Balozi Dk. Nchimbi ni kaka yake.

MSIGWA ANENA

Msigwa amesema kutokana na ubabaishaji wa vyama vya upinzani, aliamua kujiunga na CCM ambayo utekelezaji wake wa Ilani ni mzuri.

“Ndugu zangu, msione matashititi, bali ni kupoteza muda, chama pekee kinachoshughulika na matatizo ya watu ni Chama Cha Mapinduzi, kinafanyayia kazi barabara zenu, hospitali, ngozi zenu, pamba na zahanati.

“Mpina nilikuwa naye bungeni mwaka 2010, tukaondoka tukamwacha, naamini atasikia wito wa kaka yake, atarudi, watu wa Kisesa unganeni na Chama Cha Mapinduzi.

Msigwa amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amefanya mambo makubwa kwa taifa kwa kuongeza barabara za lami, hospitali, vifaatiba, ajira na madaraja yamejengwa,”amesema.

KAKA WA MPINA ANENA

Juma Mpina ambaye ni kaka wa Luhaga, aliungana na Dk. Nchimbi, kumtaka mbunge huyo wa zamani wa Kisesa, kurejea Chama Cha Mapinduzi.

Previous Post

CCM YACHANJA MBUGA

Next Post

DK. MWINYI: SITAKI KUACHA DENI

Next Post
DK. MWINYI: SITAKI KUACHA DENI

DK. MWINYI: SITAKI KUACHA DENI

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MAKONDA ASISITIZA KUTOVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE AFCON

MAKONDA ASISITIZA KUTOVUMILIA WAKANDARASI WAZEMBE AFCON

1 month ago
TAIFA STARS KUTUA MOROCCO KWA KISHINDO

TAIFA STARS KUTUA MOROCCO KWA KISHINDO

3 months ago

Popular News

  • SALOME AIBANA KAMPUNI YA DONGFANG KWA KASI ISIYORIDHISHA MRADI WA UMEME MALAGARASI

    SALOME AIBANA KAMPUNI YA DONGFANG KWA KASI ISIYORIDHISHA MRADI WA UMEME MALAGARASI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • MASAUNI AZINDUA BODI YA KABONI, AIPA MAAGIZO MATANO

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • FCC, TCRA KUCHUNGUZA GHARAMA ZA BANDO NCHINI 

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. SAMIA AIPA HESHIMA DIPLOMASIA YA TANZANIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ULINZI, USALAMA KUIMARISHWA AFCON

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?