• ePaper
Thursday, April 16, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

RAIS DK. SAMIA ATAJWA CHAPA IMARA TANZANIA

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 4, 2026
in Habari, Kimataifa, Kitaifa
0
RAIS DK. SAMIA ATAJWA CHAPA IMARA TANZANIA

RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan

0
SHARES
7
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na MWANDISHI MAALUMU, DUBAI

KATIBU Mkuu wa Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UN Tourism), Shaikha Al Nuwais, ameisifu Tanzania kama mojawapo ya nchi vinara wa utalii duniani.

Pia, alimtaja Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuwa chapa imara ya kimataifa ya Tanzania, akirejea athari chanya za filamu ya ‘Tanzania The Royal Tour’ katika kuvutia watalii.

Aidha, alithibitisha utayari wa UN Tourism, kuunga mkono azma ya Tanzania kuongeza idadi ya watalii hadi kufikia milioni nane na kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika Pato la Taifa, kutoka asilimia 17 hadi asilimia 24.

Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu iliyotolewa, ilieleza kuwa, ushirikiano huo unaunga mkono moja kwa moja, vipaumbele vya Tanzania vya kuifanya sekta ya utalii kuwa kichocheo kikuu cha ukuaji wa uchumi.

Pia, kuvutia uwekezaji wenye tija katika miundombinu ya utalii, kuunda ajira hususan kwa vijana, wanawake, kuimarisha mifumo ya utalii rafiki kwa mazingira na inayotumia teknolojia na kuinua chapa na ushindani wa Tanzania kimataifa.

Taarifa ilieleza kuwa, mazungumzo ya pande hizo, yanaakisi mkakati mpana wa Tanzania wa diplomasia ya kiuchumi, inayolenga matokeo halisi badala ya ishara, kupanua wigo wa ushirikiano wa kimataifa, ikiwemo Afrika, Karibiani, Asia na taasisi za kimataifa.

Aidha, kuoanisha ushirikiano wa kimataifa na vipaumbele vya taifa, ikiwemo Dira 2050, uwekezaji, mageuzi ya utalii na uthabiti wa kijamii na kuimarisha taswira ya Tanzania kama nchi tulivu, inayofanya mageuzi na mshirika wa kuaminika, mabadiliko ya kidijitali katika sekta ya utalii yanayohusisha ujenzi wa chapa, masoko ya kidijitali na mipango inayotumia takwimu.

Maeneo mengine ni pamoja na utofauti wa bidhaa za utalii, ukiwemo utalii wa michezo (kwa kuzingatia AFCON 2027), utalii wa utamaduni, utalii wa vyakula, miradi mikubwa ya kimkakati ya utalii inayoendelea kufanyiwa mapitio, ujenzi wa uwezo na msaada wa kitaalamu na utayari wa Tanzania kuwa mwenyeji wa Ofisi ya Kanda ya UN Tourism.

Rais Dk. Samia, alimpongeza Shaikha Al Nuwais, kuchaguliwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UN Tourism) na kuthibitisha dhamira ya Tanzania ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na shirika hilo.

Jana, Rais Samia, alifanya mikutano miwili ya ngazi ya juu ya mazungumzo ya pande mbili mwanzoni mwa Mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Serikali Duniani, unaofanyika eneo la Madinat Jumeirah, Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Taarifa hiyo, ilisema mazungumzo hayo, yalilenga kuimarisha ushirikiano wa kimkakati, kuendeleza diplomasia ya kiuchumi na kuoanisha ushirikiano wa kimataifa na vipaumbele vya maendeleo ya Tanzania.

Ilisema mkutano na Gaston Browne, Waziri Mkuu wa Antigua na Barbuda, walijadili masuala mbalimbali yaliyolenga kuimarisha ushirikiano kati ya Afrika na Karibiani, hususan kupitia mfumo wa Jumuiya ya Madola.

Viongozi hao, walikumbushia historia ya uhusiano wa pamoja na kusisitiza umuhimu wa juhudi za makusudi, zenye mwelekeo na muundo wa wazi za kuziunganisha upya “bara mama na ardhi ya asili” kupitia ushirikiano wa kisasa wa kiuchumi, kisiasa na kijamii baina ya wananchi.

Waziri Mkuu Browne, aliipongeza Tanzania kwa uongozi na uwazi katika kushughulikia changamoto za kiusalama baada ya uchaguzi, akibainisha kuanzishwa Tume Huru ya Uchunguzi ni ishara ya dhamira ya uwajibikaji na kuheshimu utawala wa kikatiba.

Rais Dk. Samia alimweleza Waziri Mkuu kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali, zikiwemo kuanzishwa Tume ya Uchunguzi, mipango ya kuunda Tume ya Maridhiano ya Kitaifa na maandalizi ya marekebisho ya Katiba.

Viongozi hao walikubaliana kuendeleza ushirikiano katika maeneo ya Ujumuishaji wa Afrika na Karibiani kupitia mfumo wa Jumuiya ya Madola, biashara, uwekezaji na utalii, ikiwemo ushirikiano wa kitaalamu wenye muundo maalumu.

Pia, muunganisho wa usafiri wa anga kwa kuimarisha safari zilizopo kati ya Afrika na Karibiani, ushirikiano wa kiusalama na uhamishaji wa teknolojia, elimu na rasilimali watu, ikiwemo kuunga mkono Mpango wa Masomo wa Jumuiya ya Madola wa Julius Nyerere na Mabadilishano ya kijamii na ushirikiano wa kitamaduni kati ya wananchi.

Aidha, iliafikiwa makubaliano ya kuunda timu za kitaalamu za pamoja kutoka pande zote mbili, kutekeleza maeneo hayo ya ushirikiano.

Browne alimwalika rasmi Rais Samia, kushiriki Mkutano ujao wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) na kutangaza nia ya kuitembelea Tanzania Juni au Julai, mwaka huu.

Ushirikiano huo, unaendeleza maslahi ya kimkakati ya Tanzania ya kupanua ushirikiano wa kusini kwa kusini zaidi ya washirika wa jadi.

Vilevile, kuiweka Tanzania kama kiunganishi kati ya Afrika na Karibiani, kutumia majukwaa ya Jumuiya ya Madola katika uwekezaji, elimu, uhamaji na kuimarisha imani ya kimataifa kuhusu utawala, uthabiti na mwelekeo wa mageuzi nchini.

Rais Samia alithibitisha utayari wa Tanzania kuunga mkono Uenyekiti wa Jumuiya ya Madola wa Antigua na Barbuda, akisisitiza Tanzania ni nchi inayotekeleza makubaliano kwa vitendo.

Previous Post

MAMBO SAFI RELI ZA KISASA MIJINI

Next Post

NEEMA ZAIDI SEKTA KILIMO

Next Post
NEEMA ZAIDI SEKTA KILIMO

NEEMA ZAIDI SEKTA KILIMO

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

MKWASA, MOGELLA, PAWASA WAIPA MCHONGO YANGA

MKWASA, MOGELLA, PAWASA WAIPA MCHONGO YANGA

2 months ago
WAFANYABIASHARA MSIWAUMIZE WANANCHI-DK. MWIGULU

WAFANYABIASHARA MSIWAUMIZE WANANCHI-DK. MWIGULU

3 months ago

Popular News

  • PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    PROFESA IBRAHIM ATIA NENO TUME YA JAJI CHANDE

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SERIKALI YAFUTA LESENI 40 ZA UTAFITI  WA MADINI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TIMU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, WIZARA YA MAJI KUCHUANA MEI MOSI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • SIMBA, FOUNTAIN GATE SIKU YA HESHIMA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS DK. MWINYI AKAGUA MJI WA AFCON FUMBA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?