• ePaper
Thursday, May 7, 2026
  • Login
No Result
View All Result
Uhuru Publication
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Hadithi
  • Login
No Result
View All Result
ePaper
Uhuru Publication
Home Habari

MAMBO SAFI RELI ZA KISASA MIJINI

Abdurahman Jumanne by Abdurahman Jumanne
February 2, 2026
in Habari, Kitaifa
0
MAMBO SAFI RELI ZA KISASA MIJINI
0
SHARES
6
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

Na FRED ALFRED, Dodoma

SERIKALI imekamilisha upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli ya kisasa za mijini katika Jiji la Dar es Salaam na Dodoma.

Hatua hiyo, inalenga kupunguza msongamano wa usafiri wa umma na kuongeza tija katika miji mikuu ya kiutawala na kibiashara nchini.

Kauli hiyo, ilitolewa jijini hapa jana na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, alipozungumza na waandishi wa habari, kuhusu mafanikio yaliyopatikana ndani ya siku 100 za uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Profesa Mbarawa, alisema Rais Samia, amewezesha kupatikana fedha za msaada kwa usanifu wa kina wa mradi huo, hatua itakayofungua rasmi utekelezaji wake.

“Tumehitimisha upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli ya kisasa kati ya Dar es Salaam na Dodoma. Hatua hii, imefungua fursa ya kupata fedha za msaada za usanifu wa kina, hatimaye utekelezaji wa mradi huu muhimu unaolenga kupunguza msongamano wa usafiri wa umma na kuongeza tija,” alisema Profesa Mbarawa.

BANDARI YA BAGAMOYO

Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa alisema serikali imekamilisha maandalizi ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa awamu ya kwanza.

Alisema bandari hiyo ya kimkakati, itapunguza msongamano wa Bandari ya Dar es Salaam na kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji wa baharini katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Awamu ya kwanza, itahusisha ujenzi wa gati lenye urefu wa kilometa 1.32 kwa ajili ya kuhudumia meli kubwa za kisasa (Mega Max). Bandari hii, itakuwa nguzo muhimu katika kuimarisha uchumi wa nchi,” alisema waziri huyo.

Vilevile, alisema wizara imekamilisha mchakato wa kuanza upanuzi mkubwa wa Bandari ya Dar es Salaam, unaolenga ujenzi wa magati 10 na matanki 15 ya mafuta.

Alisema ujenzi wa magati mawili ya awali yenye urefu wa meta 500 unatarajiwa kuanza Juni mwaka huu, huku ujenzi wa matanki ukiendelea kutekelezwa.

“Uboreshaji huu utaongeza uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam kuhudumia shehena hadi tani milioni 50 kwa mwaka, kutoka tani milioni 32 za sasa,” alisema Profesa Mbarawa.

SEKTA YA ANGA

Akizungumzia sekta ya anga, Profesa Mbarawa alisema serikali imeendelea kupanua na kuboresha huduma za usafiri wa anga kupitia Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Alisema katika kipindi hicho, ATCL imeongeza vituo vipya vya safari katika miji ya Victoria Falls nchini Zimbabwe, Cape Town (Afrika Kusini) na Accra (Ghana) na kufikisha jumla ya vituo 32.

Alifafanua kati ya vituo hivyo, 15 vya ndani ya nchi, 14 ndani ya bara la Afrika na vitatu vya kimataifa nje ya Afrika.

“Ufunguzi wa vituo vipya, umeimarisha muunganiko wa safari na kuongeza ufanisi pamoja na urahisi kwa wananchi kupata huduma za usafiri wa anga,” alisema Profesa Mbarawa.

Previous Post

ULEGA AAGIZA KUVUNJWA MKATABA WA MKANDARASI

Next Post

RAIS DK. SAMIA ATAJWA CHAPA IMARA TANZANIA

Next Post
RAIS DK. SAMIA ATAJWA CHAPA IMARA TANZANIA

RAIS DK. SAMIA ATAJWA CHAPA IMARA TANZANIA

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recommended

DK. MWIGULU AWAONYA MADEREVA WA SERIKALI

DK. MWIGULU AWAONYA MADEREVA WA SERIKALI

5 months ago
SIMBA KASI ILE ILE

SIMBA KASI ILE ILE

2 weeks ago

Popular News

  • RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    RAIS DK. SAMIA AKEMEA VIONGOZI ‘KUVIMBA’

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • DEMOKRASIA ISIZICHAFUE NCHI ZETU – RAIS DK. SAMIA

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • ZIARA YA RAIS KAGAME, RUTO KUIMARISHA DIPLOMASIA KIUCHUMI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • RAIS RUTO AIPONGEZA NSSF TANZANIA KWA UWEKEZAJI WA DOLA ZAIDI YA MILIONI 51 NAIROBI

    0 shares
    Share 0 Tweet 0
  • TANZANIA KAMILI AFCON 2027

    0 shares
    Share 0 Tweet 0

Stay Update, Subscribe Now!

Check your inbox or spam folder to confirm your subscription.

Ukurasa Rasmi wa Televisheni ya Gazeti la Uhuru.

Facebook-f Instagram X-twitter Youtube tiktok
Quick Links
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalum
  • Kolamu
  • Makala
Services
  • ePaper
Contact Information
  • Dar es Salaam,Tanzania
  • info@upl.co.tz
  • +255 783 925 742
Uhuru Publications , 2025 © All Rights Reserved
  • Terms & Conditions
  • Privacy Policy
  • FAQ
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Michezo
  • Uchaguzi
  • Burudani
  • Toleo Maalumu
  • Kolamu
  • Makala
  • Contact
  • Hadithi

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Are you sure want to unlock this post?
Unlock left : 0
Are you sure want to cancel subscription?